Wassira, Bulaya wazozana bungeni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira, Bulaya wazozana bungeni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwinukai, Jun 20, 2012.

 1. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Waandishi Wetu, Dodoma| Mwananchi | 19, Juni 2012

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Esther Bulaya, juzi walizozana katika kile kinachoonekana kuwa ni kuwania madaraka katika Jimbo la Bunda mkoani Mara, katika uchaguzi mkuu 2015.

  Sakata hilo lilitokea nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao juzi usiku, ambapo Wassira alimfuata Bulaya na kumhoji kwamba kwanini alitoa maneno ya kuipinga bajeti ya Serikali.

  Wassira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda (CCM) alimwambia Bulaya: "Mimi ndiye Mbunge wa Bunda, wewe huwezi kujifanya ndiye uliyetumwa na wananchi kuja kusema maneno ya uwongo hapa, eti unaipinga bajeti ya Serikali, ni nani aliyekutuma?"

  Waziri huyo alikwenda mbali na kumwambia mbunge huyo kijana kwamba, "wewe tunakufahamu una pande mbili (upinzani na CCM) na kila siku unashirikiana na Halima Mdee (Kawe-Chadema), tunakujua kwamba uko CCM na Chadema."

  Kutokana na kauli hizo, Bulaya alijibu mapigo akimwambia Wassira kwamba yeye akiwa mbunge wa CCM ana wajibu wa kukikosoa chama chake na hakuwa mtu wa kwanza kukataa kuunga mkono bajeti hadi hapo marekebisho yatakapokuwa yamefanywa.

  "Mimi nina haki ya kuzungumza ndani ya Bunge na kusema kile ninachokiamini kama mbunge, wala hakuna mtu wa kuniwekea mipaka. Halafu kama ni uhusiano na wabunge wengine mbona wabunge wengi tu wa CCM wanashirikiana na upinzani?" alihoji Bulaya.

  Wakati hayo yakiendelea Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na mbunge mwingine wa Viti Maalum (CCM), Rosemary Kirigini walikuwa wakishuhudia.

  Nahodha alitumia dakika chache kumsihi Bulaya kutojibu mashambulizi ya Wassira.

  Msingi wa mvutano

  Msingi wa mvutano huo ni mchango wa Bulaya alipochangia hotuba ya bajeti ya Serikali na kuhoji sababu ya kutotengwa kwa fedha za kuwalipa fidia wananchi wa Bunda waliohama katika maeneo yao kupisha utekelezaji wa mradi wa maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).

  "Nitahitaji majibu sahihi katika hili, kwani wananchi wa Bunda wamenituma na bila majibu sina haja ya kuunga mkono hoja," alisema Bulaya.

  Mbali na suala hilo, mbunge huyo pia aliiponda bajeti ya Serikali kwamba haina jipya kutokana na kushindwa kuandaliwa kwa vipaumbele, ambavyo vitasaidia maendeleo ya Watanzania, badala yake bajeti hiyo, bado imetenga fedha nyingi kwa matumizi ya kawaida, imeendeleza misamaha ya kodi na kukuwa kwa deni la Taifa.

  Akichangia hotuba ya bajeti ya Serikali, Bulaya alisema bado hajaridhishwa na serikali kutenga fedha nyingi katika matumizi ya kawaida na kwenda kinyume na mpango wa serikali wa miaka mitano ambao ulieleza wazi fedha za maendeleo zitaongezeka walau kwa asilimia 35 kila mwaka.

  Mbunge huyo alisema ni lazima Serikali iwe na vipaumbele vichache ili iweze kutekeleza kwa fedha za ndani, kuliko kuwa na vipambele vingi ambavyo haviwezi kutekelezeka.

  Bulaya alisema pia inahitajika mchanganuo wa deni la Taifa kwani bado linaongezeka mwaka hadi mwaka na sasa limefikia trilioni 20.

  Alisema pia inashangaza wakati fedha za maendeleo zinapunguzwa matumizi mengineyo katika wizara yameongezeka hadi kufikia 583 fedha ambazo ni nyingi sana.

  "Haiwezekani zikatengwa Sh583 bilioni kwa ajili ya kula katika wizara, wakati miundombinu muhimu kama Reli ya Kati inahitaji zaidi ya Sh1.3 trilioni kuboreshwa na wizara nzima imepangiwa trilioni 3.8," alisema Bulaya na kuongeza:

  "Nina mhurumia sana Waziri wa Uchukuzi, Dk Mwakyembe (Harrison) kwani hawezi kutekeleza mipango yake kwa bajeti hii," alisema.

  Mgogoro wahamia bungeni

  Katika kile kinachoonekaka kwamba ni mvutano wa kisiasa baina ya Wassira na Bulaya, suala lao liliibuka kwa sura nyingine katika kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi.

  Bulaya aliuliza swali kuhusu wananchi 164 katika Wilaya ya Bunda waliosubiri kulipwa fidia kwa ajili ya kupisha utekelezaji wa mradi wa maeneo maalum ya uwekeza (EPZ).

  Katika majibu yake, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Gregory Teu alisema wananchi hao watalipwa fedha zao mwezi ujao.

  Akijibu swali la nyongeza la Bulaya, Teu alisema, "napenda kumpongeza Mbunge wa Bunda, Mheshimiwa Wassira kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia suala hili, kwa kweli amekuwa akifuatilia sana ili kuhakikisha kwamba wananchi hawa wanalipwa."

  Kauli yake hiyo ilizua miguno na minong'ono ya chinichini kwa baadhi ya wabunge, wakiashiria kile kinachoonekana ni vita baina ya Wassira na Bulaya.

  Kuhusu mchakato wa malipo hayo, Teu alisema malipo ya fidia yalilipwa kwa awamu mbili kupitia akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambapo mwaka 2009 jumla ya Sh1 bilioni zililipwa kama awamu ya kwanza kwa hundi kutoka EPZ.

  "Awamu ya pili ya malipo ya Sh100 milioni ililipwa mwaka 2010 kwa hundi namba
  6064316 kutoka EPZ, hadi sasa katika awamu hizo mbili, jumla ya watu 116 wameshalipwa,'' alisema Teu.

  Naibu Waziri alisema fedha zilizobaki, Sh 1,042,852,910, tayari zimetengwa na hazina na inatarajiwa kulipwa Julai 2012 kwa wahusika 164 waliobakia, ili kukamilisha idadi ya watu 280 waliostahili kulipwa.

  Alisema mwaka 2007, wizara kupitia Mamlaka ya EPZ na kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ilitenga eneo la hekta 2,316 katika kijiji cha Tairo Bunda ikijumuisha vitongoji vitatu kwa ajili ya uwekezaji wa EPZ.

  Teu alibainisha kuwa katika mpango huo, jumla ya Sh3.4 bilioni zilihitajika ili kulipa wananchi wanaomiliki maeneo hayo, lakini kutokana na gharama kuwa kubwa EPZ kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara walikubaliana kupunguza na kubakiza kitongoji kimoja cha Kirumi.

  Hata hivyo, Naibu Waziri alisema kuwa malipo yatayotolewa katika kipidni cha sasa, yatakuwa katika bei ya soko la sasa, na kwamba serikali imekwisha wa kuangalia namna ya kufidia deni hilo.


  Habari hii imeandaliwa na Neville Meena, Mussa Juma na Habeli Chidawali
   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  hivi wasirra hawezi kutatua chochote bila kugombana??
   
 3. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wasira anataka kuwa mbunge hadi mauti!! waachie watoto - hawa wana full vigour!!
   
 4. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,362
  Likes Received: 6,701
  Trophy Points: 280
  kazi tunayo watanzania!
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Huyu si yule aliyepachikwa jina la Tyson kwa kumtwanga tu makonde? Sishangai.
  Hawa wananchi katika suala la malipo ya fidia huwa wanaibiwa tu. Nimefanya hesabu ya chap chap, shilingi bilioni 1.1 ukizigawa sawa sawa kwa hao watu 116 wanaodaiwa kulipwa, kila mmoja angepata kiasi cha milioni 9, je ni kweli wamelipwa zote?

  Ukitaka kuona madudu na mizengwe inayofanyika, inakuwaje watu 116 walipwe milioni na watu 164 waliobakia walipwe milioni 6 kila mmoja?
   
 6. Van persie

  Van persie JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 917
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 60
  Haya sasa, nchemba yuko wpi?. Mbunge toka ccm asema bajet ni mbovu, mzee wa first class anasemaje?. Au anasubir waseme chadema ndio puvu limtoke?.Au huyo mzee wa igunga hakuwepo wkt sister shupavu anachangia?. Sister wakikuzubaisha hao magamba njoo cdm, ungane na mdee.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Kwani Tyson bado anafikiri atarudi bungeni tena?nitashangaa sana sana sana muda wake wa kupumzika umefika 2015 wazee wote wote wapuzike la sivyo wataaibika anzia Makinda,Wassira,Komba,na wengine wanaojua wamekaa bila mafanikio
   
 8. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  BEAUTY AND THE BEAST! Peabo Bryson na Celine.
   
 9. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  kama hao watoto wana hiyo "full vigour" basi wamng'oe ubunge kwa kutumia hiyo "full vigour" badala ya kuomba Wassira "awaachie watoto." Si unasema wana "full vigour"? hahahaha...
   
 10. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Wassira 2015 harudi mjengoni aanze kuaga
   
 11. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  namkubali sana bulaya,ni mkweli na muwazi!chachu kama hizi ni muhimu sana !keep it up!
   
 12. M

  Masabaja Senior Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yote magamba hakuna la kuchukua jimbo la Bunda 2015
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Bunda hawataki kumsikia huyu Mheshimiwa wa Gombe!
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wassira amezeeeka vibaya sana hajui aendako wala kazi yake
   
 15. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimempenda Bulaya!!
   
 16. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 890
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80
  Nataka kuzimia kwa kucheka!!! Hakuna anaeweza kutuwekea picha zao ili tupate Taswira linganishi halisi?
   
 17. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nae huyu bulaya, kama ni mpiganaji si aje CDM tu, aache kuonekana ana sura mbili, kweli ni vibaya kwa mtu yeyote kuwa na sura mbili. Wassira is right at least on logical grounds, wabovu wako CCM, wazuri wako CDM. Bulaya acha kuwa na sura mbili itaku-cost mpaka hutakuwepo kushuhudia cost hiyo, take my words.
   
 18. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ubabe hautamsaidia
   
 19. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Soon, stay tuned. Kwani unachokiona kinamfanya atoke povu na kutaka kuwakunja ni nini, anajua kinachofuata.

  Mwaka 2015, Ester Bulaya atakuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Bunda kupitia CDM. Mwisho wa Wassira na Hasira zake na mapovu
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Bulaya na Mdee kulikoni?

  Inasadikika kuwa Bulaya ameolewa na Chadema.
   
Loading...