Wassira: Atibua mitandao Urais 2015

Wassira: Atibua mitandao Urais 2015

Uchaguzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
914
Reaction score
171
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu),Stephen Wassira,anadaiwa kutibua mitandao ya makada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) waliojipanga kuusaka Urais wa mwaka 2015 kupitia chama hicho,Tazama Tanzania limeelezwa.


Habari za uhakika zilizopatikana kutoka mikoa inayounda Kanda ya Ziwa,zimetaja mwanasiasa huyo mkongwe nchini kwamba kwa sehemu kubwa amekuwa kikwazo kwa baadhi ya mitandao kujijenga katika ukanda huo.


Kanda ya Ziwa inatajwa kuwa moja ya kanda muhimu katika mbio za urais,ambayo imekuwa ikifanikisha ushindi wa si tu kwa wagombea urais,bali wote wanaosaka nafasi za juu za uongozi ndani ya CCM, na hasa ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa.


Kwa mujibu wa Habari hizo,Wassira ametajwa kuwa kikwazo kikuu kwa baadhi ya Makada wa CCM wenye nia ya kugombea urais mwaka 2015,baada ya wasimamizi wa mitandao hiyo kutakiwa kuweka msimamo wao wazi kwanza kama nao wako tayari kumuunga mkono mwanasiasa huyo endapo na yeye ataamua kujitosa katika kinyang'anyiro hicho cha urais.


Wassira anatajwa kukubalika kwa kiasi kikubwa katika ukanda huo wa Kanda ya Ziwa, na kwahiyo wengi wa wanamitandao ya urais 2015 wamekuwa wakipigana vikumbo kumtaka awaunge mkono katika mbio zao hizo, ili kupitia kwake waweze pia kuungwa mkono na wajumbe wa vikao vya uteuzi kutoka kanda hiyo.


Hata hivyo, gazeti hili limeambiwa kwamba matokeo ya vikumbo hivyo vya wanamitandao hiyo ya urais katika kanda hiyo ya Ziwa,yamekuwa si ya kuridhisha baada ya kubainika kuwa hata Wassira mwenyewe anayo nia ya kugombea urais mwaka 2015 ingawa yeye binafsi hajaweka wazi nia yake hiyo.

Kutokana na hali hiyo,imeelezwa kwamba makada wote wa CCM wanaokwenda kutafuta uungwaji mkono katika kanda hiyo,wamekuwa wakipewa sharti linalowataka na wao wakubali kufanya kazi ya ziada kuwashawishi wajumbe kutoka katika kanda zao wamuunge mkono Wassira endapo naye ataamua kuweka jina.

Bofya hapa upate uhondo kamili
 

Attachments

Hope he can make it, let him try, but remind you this game is very tough and needs tough people, is he tough to this game? Is Mr.Wassira tough enough to face the chase? Lets wait.
 
Wasira ni hatari sana kwa siasa za ndani ya CCM na katika Majukwaa, anaweza akawapita wagombea wenzake wamesimama, kwa sasa ndani ya CCM ushindani ni Lowassa na Wassira. Lakini sielewi nani zaidi.
 
Jamani huu urais tuwe tunatazamako na sura!!! Huyu bwana akiupata huo urais na kisha akaenda kuhutubia UN atasababisha taharuki kwa wazungu!!

This is a total abuse.Tusijione wazuri sana mpaka tufikie hatua ya kumtukana mwenzetu.
 
wassira anautaka uraisi...na wapambe wake ni akina nyambari na kila siku vikao usiku nyumbani kwa wassira hilo liko wazi na ndiye lowassa ana muangalia sana lowasa hata wakati wa kikao cha bunge kuisha kulifanyika mkutano mkubwa kwa wana mara pale dodoma na watu wengine wanao muunga wassira mkono na katika hicho kikao lowassa alikuwa anapewa taarifa kuhusu maendeleo yake na udhuliaji wake kwa wageni kwa siku hyo.
 
mimi naona kuwa babu wanzita anatapa tapa kama mfa maji, kwani hana mbavu za kuzyia mabadiliko , pia akumbuke kuwa uzee unamyemelea na vijana wa xaxa sio wal ewa kipindi kile "TYL"
 
We really are in store for new surprises, each new day!
Wasira, my hairs!

Nakuambia huyu Tyson anaweza asihesabike kwasababu kampeni zake hafanyi kwa Magazeti, watu makini wanamsapoti sana, siku akiibuka utashika hizo nywele maradufu.
Quote my word brother.
 
Kanda ya ziwa lipi unakosema wasira ana nguvu?
MWANZA-Magu,Ilemela,Nyamagana,Ukerewe,Misungwi,Sengerema na Kwimba.

MARA-Musoma Mjini,Butiama,Tarime,Rorya,Serengeti na Bunda.

SIMIYU-Bariadi,Itilima,Busega,Maswa na Meatu

SHINYANGA-Shinyanga Mjini,Shinyanga Vijijini,Kishapu na Kahama.

GEITA-Geita,Bukombe,Chato

KAGERA-Bukoba,Bihalamuro,Ngara n

Nadhani hapo umeanza kupata picha.
 
Nyambali atampa uwaziri mkuu ni habari ya chumbani niliyoipata
 
Jamani huu urais tuwe tunatazamako na sura!!! Huyu bwana akiupata huo urais na kisha akaenda kuhutubia UN atasababisha taharuki kwa wazungu!!

Kweli nimeamini Nyani haoni kundule, hivi urais ni sura au Performance?
Mbona kuna Mahandsome serikalini na bado mnasema Nchi imewashinda na Serikali ni Dhaifu.
"Tunataaka mtu atakaye sema sitaki Rushwa hata sura yake inaonyesha"-JK Nyerere.
Wasira ni Mwanafunzi wa Mwalimu Nyerere he may predictably bring Moral changes to this damaged country.
 
Nyambali atampa uwaziri mkuu ni habari ya chumbani niliyoipata

Hapo atakosea, na sidhani hiyo itakuwa hivyo.
Nadhani unajaribu kutania, Nyambari gani? yule wa Tarime-Rorya?
 
Nchi imepata hasara sana hii,sasa mtu kama wasira anauwazia urais kwa weledi upi alionao??
huu Urais sasa umekosa hadhi, nilipokuwa primary nilifikiri Rais ni mtu mwenye akili kuwazidi wote; kafanya mtihani kawazidi wote then kapewa URAIS.

Kumbe hata zuzu anaweza kutangaza kugombea cha msingi tu awe na wafuasi wa kutosha hata kama kawanunua kwa pesa zake.
 
Back
Top Bottom