Wassira ashitakiwe

Chakunyuma

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
810
152
Polisi juzi walinukuliwa na gazeti la Mwananchi kukiri kwamba hawakuwa na taarifa kuhusu kufanyika kwa mkutano ambao ulipelekea kukamatwa kwa wafuasi wa CHADEMA, tunajua ni kosa kufanya mkutano bila kujulisha polisi sasa kwa kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wanakamatwa kwa kosa hilihili alilolifanya wasila kwann hakukamatwa? Fujo zile zisingetokea kama polisi wangekuwepo.
 
Viongozi wa kiafrika walio wengi hata wakijifanya wasomi siasa za ushindani kwao ni uhasama. Wamekuwa wahanga wa mabadiliko kwani hawataki kubadilika.
 
Ni vizuri wana JF tukatambua kuwa kuna vita ya akina Daudi na Goriath. Akina Goriath wanatumia nguvu zao wakisaidiwa na mfumo wao dharimu!! Akina Daudi wanatumia nguvu wanayopewa na wananchi! Tunahitaji kujiamini na kujitoa mhanga ktk kuuelekeza umma ukweli yakinifu ambao hawa dharimu wanauficha kwa masilahi yao! Mwisho wa siku kitaeleweka tu, wanaIgunga pigieni kura chama chenye demokrasia ya kwli inayolenga kumsaidia mwananchi sio madharimu hawa! Mliahidiwa maisha bora kwa Mtanzania, yko wapi? Kuweni makini na aina hii chafu ya utawala!
 
tatizo la magamba wanajiona wako juu ya sheria na hao polisi hawaangalii sheria wanasubiri remote ndo wafanye,nchi za africa hazitaendelea kama hatutofwata sheria,tz mpaka mjumbe wa nyumba kumi anaweza kukutisha na kukuweka mahabusu bila kosa kila kiongozi ni mbabe kwa wanyonge.
 
Tatizo lililopo si kwa mzee wa kusinzia bali ni hao polisi wanafanya kazi kwa kutekeleza matakwa ya ccm. Hawatumii taaluma yao hata kidogo vinginevyo wasingekuwa wanashindwa kuwachukulia hatua wahalifu wanaojificha kwenye mwavuli wa ccm.

Hii yote ni kwasababu askari polisi wengi ni failures madarasani ndio maana hawajiamini.
 
Polisi walikuwa wa taarifa sana, wanakanusha ili kukwepa lawama kuwa hawakufanya chochote, hawajui kuwa kukanusha kwao kunazalisha kosa jingine la kufanya mkutano bila kuarifu polisi. Hii inaonesha kuwa wamepewa muongozo wa kukanusha na ccm, maana wao ndio huwa wana ruka mk.. wanakanyaga ma..i
 
Kwahiyo kukomesha hili tatizo IGP akiteuliwa na rais inabidi aizinishwe na bunge ili asimuogope rais pekee bali pia awaogope watanzania kupitia bunge. Hili lifanyike hata kwa wakurungezi wa mashirika ya umma waizinishwe na bunge na wale wote wanaoshika positions kubwa kama mhifadhi mkuu wa park zetu, principal secretaries na nk bila hivyo hawa watu wataendelea kuogopa na kuwa double standard kila siku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom