Wassira amruka Makamba, asema huenda alibebwa yeye

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,891
Waziri mwandamizi katika serikali ya awamu ya nne mhe Steven Wassira amemshangaa January Makamba kwa kauli yake kuwa serikali ya awamu ya nne ilikuwa ya kubebana akisema yeye binafsi hakuwahi kubebwa ila anadhani kwamba kama ilikuwa kubebana basi aliebebwa ni yeye January kwani hata kuingia tano bora ya urais hakukua na cha maana alichonacho zaidi ya kubebwa.

Mzee Wassira amelazimika kusema hayo kutokana na kauli ya Makamba aliyoitoa hivi karibuni kua serikali ya awamu ya nne ilikuwa ya kubebana na kuoneana haya na ndio maana nidhamu ya utumishi wa umma ilishuka kwani ilikosa usimamizi.

Chanzo: Magazeti
 
Makamba kachemka..... anadhani kwamba yeye ana uwezo zaidi ya vijana wote ambao hawakupata nafasi yake? Anadhani isingekuwa baba yake kuwa kada kindakindaki angekuwa pale? Thubutu..... hawa ndo watu wakisha toa nyayo waliko kanyaga basi wanafuta.....
 
waliokaribu na mke wa wasira wamshauri akae karibu na mumewe inaonekana mzee akili hazijakaa sawa, bado anamawenge ya kushindwa uchaguzi. Mzee chama ulichokiasisi ndio kimekumaliza mwenyewe.
 
Ila makamba hana shukrani kabisa kwani ktk watu waliobebwa na kikwete ni yeye na hakuwa na sifa hata kdg ila kwa kujipendekeza, kuchongea wenzake kwa mkuu, kupenda sifa ni hatareee weka mbali na watoto!
 
Kuna watu wengi hawajui sababu ya kubebwa kwa huyo anayedaiwa kubebwa lakini kuna kuna sababu ya kipuuzi sana, wakati wa miaka hio walivyokutana hao "wabebaji wa huyo m'bebwaji" walikua na ukaribu na ukaribu wao ulijengwa katika msingi mmoja tu (unaofahamika kwa sasa), huyo anadaiwa "kulipa fadhila" kwasababu ilikua ili adumu kwenye madaraka na apate madaraka makubwa Zaidi ilikua ni lazima aende kwa "mafundi" na "fundi" huyo alikua akipatikana maeneo ya SONI-Lushoto - Tanga. Aliemuunganisha na kumpeleka huko alikua ndio huyo ambaye ilibidi alipwe fadhila hio au asante hio. Je unataka kujua Zaidi? Achana na mambo ya giza, si mazuri.
 
Makamba alikuwa sahihi na Mzee Wassira yupo sahihi kwani yeye ametoa mfano wa mtu aliyebebwa mpaka akafikia tano bora kwenye kinyang'anyiro cha uraisi.
 
wote walibebwa wasijifanye sasaivi wanakana.tena wasila ndio alibebwa mpaka akawa anashikwa na usingizi mara kwa mara! makamba anatafuta kick,kujisafisha ili atengeneze namna yeyote uko mbele ya safari! hupati kitu apa!
 
Hawa watu chama chao kimeshawavuruga kifikra. Hawaelewi tena hata mabaya ambayo wanaweza kukubaliana wote kuyakemea. Yaani chama chao ni bora zaidi kuliko maisha ya watanzania!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom