Date::8/20/2008
Wasomi washauri Rais Kikwete kuwafukuza kazi washauri wake
Peter Edson na Happiness Matanji
Mwananchi
WASOMI na wanasiasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi washauri wake wa masuala ya siasa, uchumi na Kijamii ili kulinusuru taifa.
Hao ni baadhi ya wasomi, sio wote, maana hata mimi kwa elimu niliyonayo ni msomi,Lakini siwezi kutoa wala kuzungumza utumbo kama huu wa REDET na hao wengine.
Kwanza hatujaelezwa ni wapi na lini washauri wa Rais wameshindwa kumshauri rais, research haijaelezwa with evident kuwa washauri fulani kuwa wameshindwa ushauri, naamini HII NI NAMNA NYINGINE YA KUMUINUA KIKWETE HUKU TUKIPUMBAZWA.
REDET this is fool, and we never expected wasomi kama nyie ambao mlishafanya makosa ya kumuweka kikwete mzungumze tena utumbo kama huu.
Kikwete ameshindwa kazi hii iko wazi , lolote atakalofanya kipindi hiki ni kugain popularity ni kuwapumbaza wananchi wengi.
Redet walimtwisha mzigo Kikwete, Redet hawakufanya wala kuact kama wasomi waliofunguka macho, walifanyika kundi moja na waandishi wa habari kumuinua kikwete.
Najua kuwa REDET ni wasomi mmoja wao akiwa Mkandala,msomi wa Marekani, USOMI NI NINI BASI kama akili za Mkandala ziko sawa na Rweyemamu nani msomi?
Wasomi ni taa ni foreseer, wasomi ni macho na darubini ya kuona mbali, jamii ya watanzania wengi hawajasoma , kazi ya wasomi ni kuwaamsha waliolala.LAZIMA WAJUE NA WASEME QUALITY YA RAIS INATAKIWA IWE VIPI, NINI AMBACHO KIKWETE ALIFANYA SIKU ZA NYUMA AMBACHO KILIPELEKEA WASEME ANAFAA KUWA RAIS, KAMA WALIFANYA UTAFITI NA WAKAGUNDUA ATASHINDA WHAT WAS THEIR RECOMMENDATIONS NA CONCLUSIONS.Tusidanganyane research lazima iwe na Conclusion na recommendation, kusema kuwa awafukuze washauri wake huku rezerach haionyeshi ni wapi wameshindwa kazi ni upuuzi na matusi yasiyovumilika, mnasahili kutukanwa matusi makubwa yote muyajuayo.
NATAMANI moja ya Recommendation au conclusion mwaka 2005 ingesomeka hivi
''Kutokana na utafiti tulioufanya tunaona Kikwete anaelekea kushinda uchaguzi ujao, lakini pamoja na wananchi wengi kuamini na kuona hivi, bado tunashawishika kusema kuwa Kikwete hatafaa kuingoza Tanzania, based on his previous performances'' Kama REDET wanatoa tu matokeo ya tafiti wanatofauti gani na BBC, majira, n.k ambao waliendesha tafiti zao na kuonyesha Kikwete atashinda?? they have to show difference.
Lazima ifike wakati wasomi wawe wasomi,kwa sasa naona wapumbavu au wajinga fulani wanaojiita maprofesa, huku hatuoni faida yao TANZANIA labda mtu anisaidie kuwa profesa nani Tanzania ambaye tunatumia utafiti wake? hamna?? ndio hao mwandishi wa habari anasema wasomi.wasomi hawa wanadharaulika '' kuwa wasomi wa kiafrika hawana mchango wowote kwa maendeleo ya binadamu duniani'' sitaki kuamini hivi , lakini haya si tunaona!!
WASOMI WENGI WAMESOMA abroad niliamini kuwa WANAJUA QUALITY YA RAIS, NA VIGEZO , mostly IS BASED ON WHAT THEY DID PREVIOUS, KWELI WASOMI WETU HAWA HAWAJUI HILI?? Hii haihitaji kusoma ulaya wala PhD. ili ujue ili.
Eti wanasema atangaze majina ya mafisadi! akishatangaza basi!, wanataka kikwete awe mdaku! siyo mchukua hatua.Kuna lipi kafanya Kikwete asilaumiwe? aliyesema inatakiwa serikali ya mseto two thumbs up! wengine wameongea uozo ambao mpaka wake zenu wanawashangaa!!, Zito kaka be careful usiiingie kwenye lugha za kipropaganda, eti awafukuze kazi washauri, wewe mwenyewe ni mshauri wa Kikwete!
Maoni mengi ya hao wasomi bado yanaonyesha '' grace period kwa Kikwete'' kuwa bado anaweza kazi, miezi, miaka, siku vinaenda huku hali za watanzania zikiwa duni leo afadhali ya jana!
Unajua kuwa profesa ni rahisi sana bongo, swala ni utafanya nini na usomi wako.maoni mengi waliyotoa ni ya kiuoga, kikwete anafaa aachie ngazi, wasomi wasiposema hivi nani aseme?? wamekalia matumbo yao,magari na maisha mazuri they dont have problem.
Nimeona mbwa wengi ulaya wanakula, wanakunywa. wanapelekwa hospitali,wanapanda na kusafiri kwenye magari mazuri sana ya kufahari, lakini hawa ni mbwa, they are remotely uncomparable far away from human value! hawana na hawataweza kuwa na thamani ya sawa na mwanadamu.
Inapotokea msomi, mwanasiasa anawaza kula, kulala, kusafiri na kuvaa vizuri, na kutoa statement kama hizo,then thats is final of his thought, hana tofauti na mbwa, tena mbwa huyu mbaya kwa maana anaweza kuongea na kurubuni watu.na mwandishi wa habari akaripoti kama hivi! eti '' wasomi washauri kikwete kuwafukuza kazi washauri wake.
washauri wa Rais ni wananchi , tumemweleza tunataka achukue hatua kuhusu EPA, RICHMOND, IPTL, rada, ndege yake, Kiwira, maliasili, madini n.k hataki mnataka ''washauri wake'' waseme nini tena?? au sisi unshauri wetu haukubaliki? kwa sababu siyo special?
Habari ndiyo hiyo!!!
waberoya
I have come to the conclusion that politics are too serious a matter to be left to the politicians''. Charles De Gaulle (1890 - 1970)