BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Date::8/20/2008
Wasomi washauri Rais Kikwete kuwafukuza kazi washauri wake
Peter Edson na Happiness Matanji
Mwananchi
WASOMI na wanasiasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi washauri wake wa masuala ya siasa, uchumi na Kijamii ili kulinusuru Taifa.
Ushauri huo umetolewa siku moja baada ya utafiti wa hali ya kisiasa nchini uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet) kuonyesha kuwa Rais Kikwete ameshuka kiutendaji.
Wakizungumza na gazeti hili jana wasomi hao walisema baadhi ya washauri wa rais hawana dhamira kumsaidia na kumshauri vizuri ili kumrahisishia utendaji wake.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alisema washauri wa rais hawana nia ya kumsaidia kupambana na umaskini unaoliandama taifa badala yake wamekuwa wakishauri mambo yanayowanufaisha watu wachache.
"Hakuna kinachofanyika hadi sasa, badala yake maisha yanaendelea kuwa magumu kwa wananchi. Washauri wa Rais wanaendelea kuwa kimya jambo linaloonyesha dhahiri kuwa hawamshauri vizuri," alisema Kabwe.
Zitto aliikosoa ripoti hiyo ya Redet akisema kuwa si kweli kwamba rais Benjamin Mkapa alikuwa na matukio machache ya watu kudai uwajibikaji, bali hali hiyo ilijitokeza kutokana na uongozi wake kuwa wa kidikteta na mabavu.
Alisema Mkapa alitumia dola kuzima mambo mengi maovu ambayo wananchi walitaka kuyadai kama haki zao za msingi.
Kauli ya Kabwe iliungwa mkono na Mwenyekiti wa PPT Maendeleo, Peter Mzirai, aliyesema kuwa umefika wakati kwa Rais Kikwete kuwa na utawala wa mseto ili kupunguza migogoro ya kisiasa, kijamii na kiuchumi inayoendelea kutikisa nchi.
Alisema tatizo la Rais Kikwete ni kutokuwa na mikakati endelevu yenye nia ya kuonyesha mwanga wa mafanikio kwa wananchi wenye kipato cha chini na washauri wake wamechangia kupoteza dira na malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Serikali.
"Suala la Serikali ya mseto linahitaji kuzingatiwa kwani ndiyo suluhisho la matatizo ya kisiasa Afrika," alisema Mzirai
Alisema Serikali ya Rais Kikwete imekuwa ikiyumba kutokana na kukosa timu imara ya kumshauri kuhusu mazingira utendaji wake.
Alisema kuna haja kwa Rais Kikwete na serikali yake kukumbuka sera za Azimio la Arusha kwani ndiyo msingi unaoweza kubadilisha uelekeo mbaya wa upepo unaoendelea kuleta hali ngumu ya maisha kwa watanzania.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Siasa na Utawala, Dk Mohammed Bakari, alisema Rais Kikwete ni muoga katika kutoa maamuzi magumu kwa hofu ya kuchochea machafuko jambo ambalo limeendelea kuhalalisha kuwa anawalinda mafisadi.
Alisema Mkapa aliweza kusimamia mambo magumu na kuyatolea maamuzi kwa sehemu, lakini Rais Kikwete amekuwa akishindwa kutoa maamuzi yenye lengo la kuonyesha muelekeo wa maendeleo na kutatua kero zinazowakabili wananchi.
"Kama Rais Kikwete atataja orodha ya mafisadi atakuwa amerudisha imani kwa wananchi kwa asilimia 60 kwani wananchi wengi wanahitaji kumuona akitoa maamuzi magumu kwa masilahi ya taifa," alisema Dk Bakari.
Alisema pamoja na kupoteza umaarufu kwa wananchi, Rais Kikwete anatakiwa kutambua kuwa kuendelea kukaa kimya bila kutoa maamuzi kuhusu ufisadi unaoendelea nchini ni kuwanyima haki ya msingi wananchi ambao walimwamini na kumpa kura.
Naye Bashiru Ally ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es salaam (siasa) alisema kuna kila sababu kwa rais Kikwete kuhakikisha kuwa anatatua mambo makubwa ambayo ni chanzo cha migogoro.
Alitaja matatizo hayo kuwa ni yale yanayodhalilisha utu wa mtanzania na kuwafanya watu wachache waendelee kuwa bora katika jamii.
"Ipo haja kwa Rais kutangaza majina ya mafisadi kwa uwazi ili wananchi warudishe imani kwake kwani sasa amepoteza muelekeo," alisema Ally.