Wasomi waelezea tafsiri ya wapinzania kukimbilia CCM

FikraPevu

Verified Member
Jan 2, 2010
303
250
Kutokana na kasi ya wanachama wa vyama vya upinzani kuhama vyama vyao na kukimbilia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuunga mkono juhudi za rais John Magufuli za kupambana na ufisadi, wachambuzi wa siasa wameitafsiri hali hiyo kuwa ni kutafuta maslahi ya kisiasa.

Hamahama ya wanachama ilishika kasi baada ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kujiuzuru nafasi yake ya ubunge kutoka CCM kwenda Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kuondoka kwake kulifungua milango kwa viongozi wa vyama vingine vya upinzania kuwa na ujasiri wa kujiuzuru nafasi zao za uongozi na kukimbilia katika chama tawala.

Siku chache zilizofuata wanachama kutoka vyama vya upinzani walianza kuingia CCM ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita Mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Said Mtulya alitangaza kujivua uanachama na kuomba ridhaa ya kuingia CCM kwa hoja zinazofanana na wanachama wanaoingia katika chama hicho tawala.

Wachambuzi wa Siasa za Afrika Mashariki wamejitokeza na kusema kasi hiyo inatafsiri nyingi ikiwemo ya ubinafsi na kutafuta maslahi ya kujinufaisha kisiasa ambayo yanatokana na kukosekana kwa utashi wa kisiasa na mfumo wa kisheria unaosimamia haki za vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa uhuru na uwazi.

Akizungumzia suala hilo, aliyewahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Mwesiga Baregu amesema ubinafsi wa wanasiasa ambao hauzingatii maslahi mapana ya wananchi ndio sababu inayowafanya wabadilike kila mara na kukimbilia katika vyama vingine ili kutafuta ahueni ya maisha.

Zaidi, soma hapa => Kasi ya wapinzania kuhamia CCM yawaibua wasomi nchini | FikraPevu
 
poa tu

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
1,174
2,000
Huo ndio ukweli. Ila CCM wanajua watatumia faida ya upumbavu wa Watanzania wengi kuwadanganya kuwa mwenyekiti wao 'anapendwa' sana.
 
kamikaze tz

JF-Expert Member
Apr 29, 2017
233
250
Huo ni ukweli bila shaka yoyote, mwanasiasa yoyote anahitaji kuongoza na kuheshimiwa, sasa kwa mtindo wa uongozi huu wa kuwabana wapinzani kwa kila hali, ni vigumu sana kwa mtu mwenye kutaka kuwa kiongozi mwenye uhakika na heshima akabaki upinzani, ninauhakika kama vyama vya upinzani hawatajaribu kudai katiba mpya au uhuru wa mikutano ya kisiasa mahakamani, basi wasishangae 2020 tukawa na uchaguzi wa chama kimoja tu. Kwa sababu hata watakaoteuliwa kugombea watajitoa sababu wanajua hawatashinda.
 
Vumilika

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
928
1,000
Kutokana na kasi ya wanachama wa vyama vya upinzani kuhama vyama vyao na kukimbilia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuunga mkono juhudi za rais John Magufuli za kupambana na ufisadi, wachambuzi wa siasa wameitafsiri hali hiyo kuwa ni kutafuta maslahi ya kisiasa.

Hamahama ya wanachama ilishika kasi baada ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kujiuzuru nafasi yake ya ubunge kutoka CCM kwenda Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kuondoka kwake kulifungua milango kwa viongozi wa vyama vingine vya upinzania kuwa na ujasiri wa kujiuzuru nafasi zao za uongozi na kukimbilia katika chama tawala.

Siku chache zilizofuata wanachama kutoka vyama vya upinzani walianza kuingia CCM ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita Mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Said Mtulya alitangaza kujivua uanachama na kuomba ridhaa ya kuingia CCM kwa hoja zinazofanana na wanachama wanaoingia katika chama hicho tawala.

Wachambuzi wa Siasa za Afrika Mashariki wamejitokeza na kusema kasi hiyo inatafsiri nyingi ikiwemo ya ubinafsi na kutafuta maslahi ya kujinufaisha kisiasa ambayo yanatokana na kukosekana kwa utashi wa kisiasa na mfumo wa kisheria unaosimamia haki za vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa uhuru na uwazi.

Akizungumzia suala hilo, aliyewahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Mwesiga Baregu amesema ubinafsi wa wanasiasa ambao hauzingatii maslahi mapana ya wananchi ndio sababu inayowafanya wabadilike kila mara na kukimbilia katika vyama vingine ili kutafuta ahueni ya maisha.

Zaidi, soma hapa => Kasi ya wapinzania kuhamia CCM yawaibua wasomi nchini | FikraPevu
Wabunge wa upinzani wanahama kwa kasi kutokana na wanapokewa huko wahamiako na kupewa "shavu" kama ilivyo onekana kwa baadhi ya wahamiaji wapya wa kisiasa na wengine waliyopewa "shavu" ilhali wakiwa katika vyama vyao vya siasa. Hali hii ina faida na hasara zake, kwani kuna watu ndani ya chama tawala ambao hawapati "uteuzi" wakati hao wahamiaji wanateuliwa katika nafasi tofauti, hali hii inaweza kuleta sintofahamu kwa wafia chama ambao hawapewi mtazamo wa pili kwa kujitolea kwao katika kukijenga chama.
Ni kweli kabisa hii hamahama ni sababu za maslahi binafsi kwa wahamiaji si kwa maslahi ya umma.
Kumuunga mkono raisi si kuhama chama tu, hata kama huna chama unaweza kumuunga mkono raisi, kuna watu walimuunga mkono raisi ilhali wapo kwenye vyama vyao vya upinzani, hao wanamuunga mkono mwenyekiti wa chama tawala na si raisi.
 
xenaxena

JF-Expert Member
May 20, 2014
2,237
1,500
Wanasiasa wanaohama vyama vyao aidha wanabanwa na kunyimwa fursa ili warudi ccm kwa kuwa ccm inawafahamu tabia zao na mitazamo yao.Pili,CCM inaona kuwa njia ya kupambana na upinzani nikuwaahidi na kuwapa vyeo niwaulize swali chadema inawafuasi zaidi ya milioni nane na wengi wao takribani laki nne nivijana wasomi sana nao wote watakapoachiwa nafasi na wahamaji nao mtawapa shavu?

Tatu,ccm iawatisha wasiojielewa ikiwa inamajimbo ya uchaguzi karibu Dodoma nzima kuanzia mwenyekiti wa mtaa,kijiji,kitongoji ,diwani na mbunge ni ccm lakini bado wananchi wake hawana maji safina saama,hakuna miundombinu,na hakuna umeme wa kutosha na huduma bora zakutosha,badowagogo wanaoichagua ccm wanahaha na matatizo leo iwadanganye kuwa ukirudi ccm tutapeleka maendeleo kwa kasi kiasi gani?

wanachaema msihadaike
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom