Wasomi wa sheria always mnanichanganya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi wa sheria always mnanichanganya

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by bornagain, Aug 11, 2012.

 1. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mimi kuna kitu hata hakiingii akilini, unakuta eti mtuhumiwa anapelekwa Kisutu mahakamani kusomewa mashtaka, mara unaskia eti kesi yake imeahirishwa kwa kuwa ni ya mauaji eti mahakama ya Kisutu haina uwezo wa kusikiliza kesi za namna hiyo.Sasa swali langu ni kwamba, kama wanajua mahakama ya Kisutu haiwezi kusikiliza kesi ya namna hiyo kwa nini wanampeleka mtuhumiwa mahakamani?
   
 2. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Still am looking for clarification on this jamani ama nikiandika kiinglish ndo ntaeleweka mbona najua hapa ndo panapo msaada wa kila linaloshindikana uraiani.
   
 3. m

  msagalam Member

  #3
  Dec 14, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huo ni utaratibu ambao umewekwa kisheria, kwamba kesi zote za mauaji mahakama ambayo imepewa uwezo wa kusikiliza ni mahakama kuu sasa basi kabla ya hiyo kesi kufika huko mahakama kuu kwanza inaanzia mahakama ya chini kama ulivyosema awali kisutu kwa ajili ya uchunguzi wa awali wanaita "P.I" Preliminary Investigation.
  Hapo wanaangalia mazingira ya jumla kuhusiana na tukio lenyewe na uchunguzi ukikamilika ndio faili kamili linapelekwa mahakama kuu kwa ajili ya kesi kuanza kusikilizwa,
  Kwa hiyo mauaji yakitokea taarifa inapelekwa polisi jalada linafunguliwa then file linapelekwa mahakamani mfano kisutu then watuhumiwa wanapelekwa wanasomewa mashtaka yao lakini hawaruhusiwi kujibu then kesi unaahirishwa,uchunguzi unafanyika na ukishakamilika basi jalada linapelekwa mahakama kuu kwa ajili ya usikilizwaji.
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Swali zuri. Kama nitaweza kukupa jibu vizuri sijui, lakini nitajitahidi. Kwa kawaida kila mahakama ina mamlaka yake. Kwa Kiingereza, wanaita "jurisdiction".

  Mara nyingi mamlaka ya mahakama yanahusiana na sehemu au aina ya shauri lenyewe. Kwa mfano, kama kosa limefanyika wilayani Bagamoyo, basi mahakama ya wilaya ya Bagamoyo, na siyo ile ya Kibaha, ndiyo itakuwa na mamlaka ya kusikiliza hilo shauri.

  Mamlaka ya mahakama kulingana na shauri yanatofautiana kutoka mahakama moja kwenda nyingine na pia kama shauri ni la madai au jinai. Hapa nitaangalia zaidi mamkala kwenye makosa ya jinai kwa mujibu wa swali lako.

  Kwanza kabisa kuna mahakama ya mwanzo ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama ya Mahakimu ya Mwaka 1984. Mahakama ya Mwanzo ina uwezo wa kusikiliza kesi za jinai zote isipokuwa kwa makosa yahayohusiana na uhaini, mauaji, na yale ambayo kifungo chake kinazidi mwaka mmoja au faini ya shilingi 200,000/= (unless kama faini imeshabadilishwa).

  Iwapo hakimu wa Mahakama ya Mwanzo atasikiliza kesi na kutoa hukumu ya kifungo kinachozidi miezi kumi na mbili, basi anatakiwa alipeleke jalada la kesi hiyo kwa hakimu wa wilaya mfawidhi kwa ajili ya uthibitisho wa adhabu hiyo.

  Baada ya mahakama ya mwanzo, kuna mahakama za hakimu Mkazi au Wilaya ambazo nazo zimepewa majukumu mbalimbali. Mahakama za Wilaya ziko katika daraja moja na Mahakama ya Hakimu Mkazi. Uwezo wao katika mashauri ya jinai unalingana isipokuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ina uwezo mkubwa zaidi wa kusikiliza mashauri fulani ya madai kama vile chini ya Sheria ya Kodi za Majumba.

  Kuhusiana na makosa ya jinai, mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya zina mamlaka ya kusikiliza na kutolea maamuzi kesi zote za jinai isipokuwa makosa ya uhaini, mauaji na makosa ya uhujumu uchumi.

  Mahakama Kuu hutekeleza majukumu yake ya utoaji wa haki Tanzania Bara kwa mujibu wa Sheria ambazo hutumika Tanzania Bara na zile ambazo hutumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwenye kesi za Mahakama Kuu husikiliza kesi za mauaji, uhaini na uhujumu uchumi.

  Hata hivyo, kesi nyingi za mauaji huanzia mahakama ya hakimu Mkazi/wilaya katika hatua za mwanzo. Katika hatua hii mshitakiwa haruhusiwi kujibu lolote mpaka shauri lake litakapofikishwa Mahakama kuu kwa ajili ya kusikilizwa. Mshtakiwa hatakiwi kujibu lolote kwa sababu kisheria mahakama ya hakimu Mkazi/wilaya haina mamlaka (jurisdiction) ya kusikiliza kesi za mauaji.

  Kwa hiyo, mahakama ya hakimu Mkazi/wilaya zinamsomea tuu mshtakiwa kosa analoshtakiwa nalo bila yeye kusema chochote. Nafikiri swali lako limejikita hapa. Kwamba kama mahakama ya hakimu Mkazi/wilaya hazima mamlaka, kwa nini basi shauri lisipelekwe moja kwa moja Mahakama Kuu ambayo ndiyo yenye hayo mamlaka?

  Kama nilivosema hapo juu, Mahakama ya Wilaya/Hakimu Mkazi zina uwezo wa kusikiliza karibu makosa yote ya jinai isipokuwa yale makubwa sana kama vile mauaji, uhaini, ujasusi na kadhalika. Kuhusiana na makosa hayo makubwa Mahakama ya Wilaya/Hakimu Mkazi zina uwezo wa kisheria wa kuendesha uchunguzi wa awali tu na kupeleka kumbumbuku za uchunguzi huo Mahakama Kuu kusikilizwa rasmi.

  Nadhani sababu ya kuwepo kwa sheria kama hii inatokana na sheria inayotaka mtuhumiwa badala ya kuwekwa rumande tuu mpaka uchunguzi ukamilike ni bora afikishwe mahakamani haraka iwezekavyo. Kama mtuhimiwa ameua na kukamatwa wilayani Tandahimba itabidi asafirishwe mpaka Mtwara mjini ilipo Mahakama Kuu ili asomewe shataka la mauaji wakati bado uchunguzi ukiendelea.

  Ni covenient zaidi kama akifikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Tandahimba, anasomewe shataka bila kujibu, mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na kesi kuanza kusililizwa na Mahakama Kuu ambayo inakuwa na vikao vya mara kwa mara kwenye wilaya, n.k. Nadhani hiyo ndio sababu, lakini I stand to be corrected.

  Mwisho kuna Mahakama ya Rufani ambacho ndicho chombo cha mwisho cha utoaji haki hapa Tanzania. Mahakama hii hushughulikia rufani zote za kesi za jinai na madai zinazotoka mahakama Kuu ya Tanzania, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Mahakimu iliyokasimiwa mamlaka fulani. Pia ina mamlaka ya kusikiliza maombi ya kupitiwa upya hukumu ya Mahakama Kuu na kurejea hukumu yake yenyewe.

  Maelezo zaidi unaweza kuyapata:

  1. Taratibu za Mwendo makosa ya jinai: http://www.humanrights.or.tz/wp-content/uploads/2010/10/TARATIBU-ZA-MWENENDO-WA-MAKOSA-YA-JINAI-8TH-JUNE-2010.pdf

  2. Mahakama Tanzania: Utaratibu wa Kutoa haki nchini Tanzania: http://chragg.go.tz/docs/p_info/1/Kiswahili%20versn-%20Judiciary%20of%20Tanzania%20FINAL.pdf
   
 5. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Thanks mkuu hahaha fanya mpango uchukue kile cheo cha yule Mkurya mwanasheria mkuu wa serikali
   
 6. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu uko vizuri sana ilitakiwa uwemo kwenye tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Warioba
   
 7. k

  katalina JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usikariri, si wanasheriaa tu wanaotakiwa kwenye tume ya warioba, hata taaluma zingine zinahitajika!
   
 8. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Haya basi Katalina uwemo wewe kwenye tume basi
   
Loading...