Wasomi wa kizazi kipya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi wa kizazi kipya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Omary Mwenda, May 31, 2011.

 1. O

  Omary Mwenda Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TANZANIA imebarikiwa kuwa na UTAJIRI WA WASOMI WENGI ambao huzalishwa kila kukicha, WASOMI HAWA WA KARNE YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA wamegeuza SIASA KM MTAJI na kusahau jukumu lao la msingi ktk TAIFA kwa kukubali kuwa WASHABIKI WA SIASA ZISIZOKUWA NA MASLAHI KWA MWANANCHI HOHE HAHE! WASOMI ambao wameegemea ktk hoja zenye KUBEZA kuliko KULETA MAPENDEKEZO YA MABORESHO KWA SERIKALI! Wasomi waliolelewa ktk MISINGI YA UOGA YA KULAZIMISHWA KUKUBALIANA NA FIKRA MFU! JE TUTAFIKA??!
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  tutafika tu
   
 3. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Umeandika mambo mengi but kwa mafumbo fafanua.

  1. SIASA ZISIZOKUWA NA MASLAHI KWA MWANANCHI HOHE HAHE! - Ni zipi?

  2. hoja zenye KUBEZA kuliko KULETA MAPENDEKEZO YA MABORESHO KWA SERIKALI! - Ni lini serikali ilitaka ushauri/hoja nzuri wakazikosa?

  3. MISINGI YA UOGA YA KULAZIMISHWA KUKUBALIANA NA FIKRA MFU! - Ni fikra gani hizo ambazo watu wamelazimishwa?
   
 4. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  tutafika tuuu,
  kila mtu anaangalia tumbo lake kwanza af baadae ndo utaifa unafuata.
   
 5. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sijakupa vizuri mheshimiwa. Je, unataka siasa waachiwe wasio wasomi au vipi? Au unajaribu kumaanisha nini? Labda tatizo kubwa ni ukosefu wa ajira baada ya kumaliza masomo.
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kinachoniudhi unawakuta wataalamu wanaacha siasa wanaenda kugombea ubunge. Wanapoteleza kabisa huko kwenye siasa na fani zao wanaziacha. Hakuna ubaya kwa wasomi kuwa wanasiasa, kama kama hata ma-experts wa fani nyeti nao wanakuwa wanasiasa ni mbaya kwa kweli.
   
 7. O

  Omary Mwenda Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilichomaanisha ni kwamba UTAJIRI WA WASOMI wanaokimbilia ktk SIASA UNATAKIWA kuwa na manufaa kwa wananchi na Taifa badala ya kukimbilia siasa km njia ya kujikwamua kimaisha! Pili FIKRA MFU ni fikra zisizoleta athari ya mabadiliko ktk jamii! Mwisho ni lazima ifikie MAHALI TURUDISHE UZALENDO NA TUWE NA UCHUNGU NA TAIFA!
   
 8. O

  Omary Mwenda Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cna maana siasa waachiwe wasio wasomi bt hao wasomi walete mabadiliko endelevu kwa wasio wasomi badala ya kuangalia matumbo yao!
   
 9. O

  Omary Mwenda Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SIASA ZISIZOKUWA NA MANUFAA KWA MWANANCHI- Tunashuhudia kila cku wananchi wakipandikizwa chuki dhidi ya serikali yao wenyewe walioiweka madarakani kwa kura zao wenyewe HAKIKA HIZI SI SIASA ZENYE MANUFAA KWA MWANANCHI HOHE HAHE!
   
 10. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufika tutafika, na nataka nikuhakikishie kuwa kwa sasa tuko halfway ya safari!
   
 11. G

  Galula Jr Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na wewe ni great thinker, i think you should join Nape, Makamba and Tambwe Hiza on facebook. Maana huu ni zaidi ya utumbo uliooza
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa kuwa wanaacha kazi za kitaalam kwenda kwenye siasa!

  Labda hatujuai maana halisi ya siasa!


  Ni kazi gani ambayo haiathiriwi na siasa mbovu? utafanya kazi gani katika system ya nchni yenye siasa chakavu! Siasa bado inaathiri kila dakika moja ya Mtanzania inayopita kila siku, sababu kubwa inayoweza kupereka wasomi kufanya siasa ni mbili:
  1. Katika nchni kama Tanzania tupo katika mpito hadi tutakapo tengeneza mfumo wa siasa imara wenye maslahi kwa umma ndipo mtu anaweza kuchagua ama kubaki katika siasa au kufanya kazi za kitaalam maana tutakuwa na mfumo imara unaojali wataalam na ambao unawajibika kwa umma; hivyo kwasasa kila mtu anahitajika kuingia katika siasa kwa ajili ya kukomboa nchni yake kutoka katika mikono ya wachache wenye maslahi binafsi ambao wapo zaidi kwa ajili ya kudhoofisha nchni na si kuendeleza nchni. Utakuta wataalam hawa wapo katika vyama vya upinzani mstari wa mbele kudai haki na mabadiliko.
  2. Sababu ya pili ni wataalam ambao wanajiunga na chama ambacho kinanyonya watu kwa maslahi yakushirikiana na wanyonyaji kwasababu haridhiki na kipato kidogo anachopata kwa kazi yake ya utaalam maana uchumi ukisha bomolewa na hawa Mafisadi kazi za utaalam zinakosa maslahi bora! mara nyingi watalaam kama hawa wamekuwa wakishirikiana na vyama vinavyonyonya toka zamani kwa kuwapa ushauri wa kitaalam namna ya kuiba na kupindisha mambo, mfani mzuri ni chenge akiwa mwanasheria ndipo alipopata nafasi ya kushirikiana na wanasiasa kutengeneza mikataba mibovu na hivyo akawa hana budi kujiunga nao moja kwa moja katika siasa.
   
 13. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mabadiliko ya ukweli yanapatikani mjengoni so wasomi wanatakiwa kwenda kurekebisha,kutunga,kuondoa sheria mfu,wanatakiwa kuonesha mikataba mibovu inayoangamiza nchi iwe kiza cos of 10%,na uzalendo wa kweli ni huo cos wanakwenda kulinda rasilima ya nchi hii kwa manufaa ya watanzania wote,au ww ni wale wenye mawazo siasa ni za wazee?
   
 14. moblaze

  moblaze JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kimjini mjini hapa...
   
 15. R

  Ray Isly Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah kiukweli kutoka uongoz wa dini mpaka urais,kutoka mfanya biashara mpaka mwenyekit wa chama,kutoka ukuu wa Idara(profesor) mpaka mpiga debe wa siasa! wasomi kweli utendaji na ujenz wa Taifa kupitia taaluma kweli haulipi 2jimwageni. CCM,CDM,TLP nk.watu wote wameacha taaluma zao ambazo zingekua msada katika ujenz wa taifa. Matokeo yake walotarajia hayawi wanataka watu watiane mikononi,uchochez,kugombanisha wadau na viongoz wao!co ishu Wakubwa.
   
 16. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180


  well said Omera.
   
 17. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mie nalia tu hebu niambieni kwa takwimu za Sub saharan Africa daktari mmoja anahudumia wananchi 25,000 na hii ni pamoja na Tanzania, sasa huko mjengoni umeona idadi ya Madaktari walivyoongezeka??? Mkuu ni katika kufata maslahi kwani hata hao waliopo sijaona lolote watakalofanya la maendeleo, hivi Daktari mwenye akili timamu anaweza kusupport wazo la kununua piki piki bajaji kubebea wajawazito kutapunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na kuchelewa kufika hospitali?? Wakapiga makofi nyie madaktari wabunge nawasubiri sana kuwasikia kipindi hiki cha bunge la bajeti mtatetea vipi wananchi wapate huduma za Afya zilizo bora. Mungu atusaidie, wote wezi tu..............serikali ya chama cha magamba.....kufika tutafika lakini sio leo wala kesho
   
 18. O

  Omary Mwenda Member

  #18
  Jun 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @Galura nadhani HASIRA NI DALILI YA UVIVU WA KUFIKIRI N ACTUALLY UR NOT A GREAT THINKER N SORRY 4 DIS! HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA SIO KWA PUMBA ULIZOZIPOST! Huo ni mtazamo na nafikiri ma great thinker wametoa pia hoja zao nimeziona! HUO NI USHAURI TU UCWE MVIVU WA KUZITUMIKISHA FIKRA ZAKO N NISAMEHE KWA HILI! LETE HOJA..!
   
 19. O

  Omary Mwenda Member

  #19
  Jun 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @Arafat umeweka mchanganuo mzuri na nimekuelewa vizuri kabisa kaka!
   
 20. O

  Omary Mwenda Member

  #20
  Jun 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @Measkoron dat z a logic..!
   
Loading...