Wasomi tumechoshwa na dharau zenu

Uta Uta

JF-Expert Member
Feb 2, 2016
3,684
8,591
Habari za jioni wanajamvi,

Nadhani wengi wenu mko makini katika kufuatlia muandamo wa mwezi.

Wasomini tabaka ambao linaheshimika sana duniani, wengi tunaamini kwamba wasomi ni watu wenye busara na upeo mkubwa sana wa kupambanua mambo mbali kwa ujuzi wao.

Sisi tusiosoma tunawaheshimu sana wasomi tukiamini kwamba wao ndio wakombozi wetu katika kutatua changamomoto za kimaisha.

Wasomi nao hawako nyuma kwa majigambo na dharau, wanatutukana matusi ya kila aina mara vilaza, mbumbumbu,wapumbavu na kila aina ya majina ya kuudhi.

Sasa mi nimevumilia leo nimeona nipasue jipu nimechoshwa na hizi dharau, sisi hatukupenda kutokuwa wasomi ila mazingira tu ndio yalitukwaza kupata elimu.

Sasa swali langu kubwa ni "hivi ninyi wasomi na sisi tusiosoma mpumbavu ni nani? Bila ubishi wala nini wasomi ni wapumbavu wa kiwango cha juu kuliko sisi tusiosoma.

Wasomi mnapofanya reseach zenu ili mpate Masterz nk, mnakuja kutuhoji sisi tusiosoma na questionaire zenu, baadae mnapata Masterz zenu kwa kutuhoji sisi wapumbavu.

Sisi ndio tunaowapa hizo Masterz halafu mnatutukana, kama sisi wapumbavu kwa nini hizo questionaire zenu msiwapelekee Maprofesa ambao ni wasomi wenzenu.

Masterz unayoipapta kwa kuwahoji wapumbavu inakuwaje, ya kijanja? Mimi mpumbavu mmoja, ila wewe unachukua zaidi ya mawazo ya wapumbavu 100 unapata masterz yako.

Sasa mimi mpumbavu mmoja na wewe uliechukua masterz kwa mawazo ya wapumbavu zaidi ya 100, nani mpumbavu zaidi.

Mimi inaniuma sana wasomi mnapotudharau sisi tusiosoma wakati elimu zenu zinatutugemea sisi, naomba kuwasilisha huku nikiwa na uchungu sana.
 
ajAAR7Q_700b.jpg
 
wengi tunaamini kwamba wasomi ni watu wenye busara na upeo mkubwa sana wa kupambanua

Hapo napingana na wewe hususan kwenye busara.

Busara na usomi havina uhusiano kabisa.

Kuna watu wamesoma na mashahada wanayo kemkem lakini busara tu za kawaida hawana.

Wakifungua midomo yao kusema kuhusu jambo fulani unaweza usiamini kama kweli ni wasomi au la.

Vivyo hivyo, kuna watu hata darasa la saba hawakumaliza lakini wana busara ajabu!

Mtu anaweza pia kuwa ni msomi na akawa na busara na vilevile mtu anaweza akawa si msomi na akakosa busara.

Suala la busara kwa maoni yangu, linaendana zaidi na tajiriba ya mtu na uwezo wake wa kuelewa na kung'amua mambo kuliko mafunzo aliyoyapata darasani.
 
Mzee baba hata baada ya wewe kuhojiwa na kutoa mawazo yako hua yanachujwa na kuangaliwa kama yana ubora.

Mfano unamhoji msichana anayejiuza akakwambia anajiuza kwa kua maisha magumu, lakini kafanya kazi kwa miaka 4 na anaweza kupata 10000 kwa siku kama pesa ya chini.
Hivyo huyu sababu yake ya kujiuza ni ya uongo kwakua angeweza kupata mtaji na kujiajiri tangu muda tu.
 
Sasakwa nini msiende kuwahoji maprofesa mnakuja kutuhoji sisi, hata kama umechuja chanzo chake si mpumbavu
 
Sasakwa nini msiende kuwahoji maprofesa mnakuja kutuhoji sisi, hata kama umechuja chanzo chake si mpumbavu
Kwa sababu ili ufanye utafiti utakua una Kichwa cha utafiti wako.
Kabla ya kufanya utafiti utaandaa pendekezo la jinsi gani utakusanya data, utakusanya kwa nani na kwa mtindo gani.
Na hapo utakua unatumia nadharia gani katika kufanikisha huo utafiti.

Kichwa ulichokiamua ndiyo kitaamua nani ahojiwe, mfano nikiwa na Kichwa kinachouliza "Kuvuta bangi ni chanzo cha uchizi Kiluvya?"
Maana yake hapo atahojiwa mvuta bangi, Daktari, utaangalia na vitabu kama vipo vilivyowahi kuonyesha hiko kitu, na wengine.

Halafu nani kakukasirisha hadi unajiita mpumbavu muda wote tu?
 
hivi hakuna profesa anaekula msuba/kijiti?
 
Pole sana mkuu, fanya jitihada na wewe uwe msomi Elimu haina mwisho, na kumbuka dharau ni tabia ya mtu binafsi..hamna darasa linalofundisha kudharau watu ambao hawajasoma
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom