Wasomi tumechoshwa na dharau zenu

Wasomi tumechoshwa na dharau zenu

Habari za jioni wanajamvi,

Nadhani wengi wenu mko makini katika kufuatlia muandamo wa mwezi.

Wasomini tabaka ambao linaheshimika sana duniani, wengi tunaamini kwamba wasomi ni watu wenye busara na upeo mkubwa sana wa kupambanua mambo mbali kwa ujuzi wao.

Sisi tusiosoma tunawaheshimu sana wasomi tukiamini kwamba wao ndio wakombozi wetu katika kutatua changamomoto za kimaisha.

Wasomi nao hawako nyuma kwa majigambo na dharau, wanatutukana matusi ya kila aina mara vilaza, mbumbumbu,wapumbavu na kila aina ya majina ya kuudhi.

Sasa mi nimevumilia leo nimeona nipasue jipu nimechoshwa na hizi dharau, sisi hatukupenda kutokuwa wasomi ila mazingira tu ndio yalitukwaza kupata elimu.

Sasa swali langu kubwa ni "hivi ninyi wasomi na sisi tusiosoma mpumbavu ni nani? Bila ubishi wala nini wasomi ni wapumbavu wa kiwango cha juu kuliko sisi tusiosoma.

Wasomi mnapofanya reseach zenu ili mpate Masterz nk, mnakuja kutuhoji sisi tusiosoma na questionaire zenu, baadae mnapata Masterz zenu kwa kutuhoji sisi wapumbavu.

Sisi ndio tunaowapa hizo Masterz halafu mnatutukana, kama sisi wapumbavu kwa nini hizo questionaire zenu msiwapelekee Maprofesa ambao ni wasomi wenzenu.

Masterz unayoipapta kwa kuwahoji wapumbavu inakuwaje, ya kijanja? Mimi mpumbavu mmoja, ila wewe unachukua zaidi ya mawazo ya wapumbavu 100 unapata masterz yako.

Sasa mimi mpumbavu mmoja na wewe uliechukua masterz kwa mawazo ya wapumbavu zaidi ya 100, nani mpumbavu zaidi.

Mimi inaniuma sana wasomi mnapotudharau sisi tusiosoma wakati elimu zenu zinatutugemea sisi, naomba kuwasilisha huku nikiwa na uchungu sana.
mfano mzuri Sizonje. Ana phd lakini angalia na sikiza anayaongea. Hana busara kabisa zero brain. Grow up Sizonje
 
kwanini watu wengi wanaamini ukiwa msomi basi wewe umekamilika kwenye nyanja zote za maisha?
kuna mambo mengine mtu anayafanya ni tabia ya asili, ayawezi kubadilika kwa elimu hata aende kusomea mwezini!
sasa hizi tabia zinapooneka kwa watu wakawaida inaonekana ni jambo la kawaida lakini tabia hizo hizo akifanya mtu msomi ataonekana kama ana mapungufu flani
tunasahau kwamba hata kama wewe ni msomi kiasi gani lakin mwisho wa siku unabaki kuwa binadamu wa kawaida tu, hii mentallity ya watu kudhani kuwa usomi ndio kujua kila ndio inaleta mawazo mabaya kwa baadhi ya watu. watu wabadilike kwa hilo..
 
Mi nafuatilia mijadala mbali mbali hapa JF na hapa jukwaaani ndio panaongoza kwa dharau mtu akichangia jambo basi matusi na kejeli kibao kisa elimu, huko vijijini sasa ndio balaa msomi akishapiga bapa zake stupid zitakuwa kibao siku hiyo. Kwa hiyo nawakumbusha tu sisi ndiotunaowapa huo usomi sio hao walimu wenu au wasomi wenzenu. Hivi tukigoma sisi kujibu/kujaza hayo madude yenu mtakuwa wasomi tena.Na mawazo yetu sisi mnaotupuuza ndioyanayowapa usomi sasa mawazo ya unaowapuuza na wewe uliyewanyia kazi nani mpuuzi. Kwa mfano umemuuliza chizi " kuvua nguo hadharani ni raha akajibu ndio" halafu wewe ukaenda kuvua nguo hadharani, wewe utakuwa kundi gani? N a wengi wenu mnasomeshwa na sisi tusiosoma, ila hilo mnasahau. Kwa hiyo mkae mfikirie kwa umakini mchango wetu sisi tabaka tusiosoma. Nilitumia lugha kali kidogo sio jazba hapana ila kukelwa tu hizo dharau na hasa jukwaa la siasa
 
kusoma sio kuelimika unaweza ukawa si msomi lkn umeelimika
Tena sisitunamchango mkubwa wa wasomi kuanzia kuwauzia ubuyu na ice cream, mihogo mpaka chips ambazo zinawapaka nguvu na uwezo wa kusoma, ila baadae mnaleta dharau acheni bana
 
Back
Top Bottom