WASOMI" NA NDOTO ZA ABUNUASI

WASOMI" NA NDOTO ZA ABUNUASI

kwasababu hakuna ajira haina maana watu wasisome, ELIMU ni bora na huwezi kumlinganisha mtu mwenye degree na aliyeishia darasa la saba... Leo utamuona aliyebahatika kuwa tajiri bila ya kusoma anamtafutia mwanae shule ya million 5 akasome halafu... ulimko chuo someni kwa bidii ni njia ya kutimiza ndoto zenu na tuliomaliza chuo tupambane kwa nguvu tutumie ELIMU tuliyoipata na tumuombe mungu tutatimiza ndoto zetu zinazoitwa za abunuasi
Patience, persistence and perspiration make an unbeatable combination for success.. Acha kukariri maisha uajiriwe uwe Tajiri.. Hicho kitu never..
 
Nani kakwambia kusoma ni kuwa Tajiri.. Nimeona umeandika.. Darasa la saba kabahatika kuwa Tajiri Bila kusoma.. Nna wasiwas na hata na usomi wako..

ndio narudia tena la saba kabahatika kuwa tajir either kwa kurithishwa au vingune.. na huwez kumdhalau mtu ambayo kasoma kisa tuu eti hana ela
 
ndio narudia tena la saba kabahatika kuwa tajir either kwa kurithishwa au vingune.. na huwez kumdhalau mtu ambayo kasoma kisa tuu eti hana ela
Umuhimu wa elimu una tegemea na ujinga ulionao...
 
Patience, persistence and perspiration make an unbeatable combination for success.. Acha kukariri maisha uajiriwe uwe Tajiri.. Hicho kitu never..
patience and persistence bila ya knowledge ??? sijasema uajiriwe ili uwe tajir ila naamin ukiwa na knowledge ya kutosha unaweza Fanya gud kuliko asiye na knowledge
 
ndio narudia tena la saba kabahatika kuwa tajir either kwa kurithishwa au vingune.. na huwez kumdhalau mtu ambayo kasoma kisa tuu eti hana ela
Elimu yako haijakusaidia ipasavyo kama bado una akili hiyo kwaiyo mtu amefight na life katoboa eti kabahatisha kisa hakufika chuo kikuu.... We ulikuwa unakariri shuleni
 
Umuhimu wa elimu una tegemea na ujinga ulionao...
kwani ujinga ni nn? ujinga ni ukosefu wa maarifa na naamin aliyeenda shule ana maarifa zaidi ya ambayo hajaenda shule
 
patience and persistence bila ya knowledge ??? sijasema uajiriwe ili uwe tajir ila naamin ukiwa na knowledge ya kutosha unaweza Fanya gud kuliko asiye na knowledge
Knowledge sasa siyo lazima uipate chuo kikuu Kuna ambao wamezaliwa Vijijini kwao ni wa kulima tayari mtu huyu anapata elimu kuhusu Kilimo Tena kwa vitendo na yule aliye fika jkt amejifunza kilimo kwa vitendo huyu tayari amejifunza siyo lazima afike chuo na elimu ya theory haisaidii chochote mtaani zaidi ya kusubiri ajira.. Kwaiyo suala la elimu tambua haipatkani chuo peke ake..
 
kwani ujinga ni nn? ujinga ni ukosefu wa maarifa na naamin aliyeenda shule ana maarifa zaidi ya ambayo hajaenda shule
The real measure of intelligence is action. Sasa ww na degree yako umesoma maelezo ysko mwenzio kapita veta au kajifunza kivitendo zaidi unasema ww una akili kushinda yy ikiwa ww uwezi apply knowledge yako mtaani..
 
The real measure of intelligence is action. Sasa ww na degree yako umesoma maelezo ysko mwenzio kapita veta au kajifunza kivitendo zaidi unasema ww una akili kushinda yy ikiwa ww uwezi apply knowledge yako mtaani..
ahsante... nadhan tumeanza kuelewana... me shida tangu ilikua uaknowldge elimu... kwa vile umetaja veta au kujifunza kwa vitendo means huyo mtu ana kwoledge kitu ambacho ndo nilichokua nasema na wala sio degree ya udsm
 
Aliye ishia form four na akatambua fursa zilipo na akazifanyia kazi na akatoboa maisha akaajiri watu huyu ni intelligence kuliko yule aliye Soma theory alafu akaja mtaani pia akashindwa kubadilika amekaza kichwa yy ni msomi ko anataka kufanya shughuli ya alicho Soma ikiwa akiwezi kuwa applicable zaidi ya kuajiriwa mwisho wa siku anakaa tu kwao.. Huyu awezi kuwa na akili kumzidi wa form four.. maisha yamebadilika na ss tunatakiwa kubadilika..
 
Ngumbalu mkipata visenti kidogo mnaongea shombo sana. Mfano ni yule mwenzenu wa ist
 
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na "vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa "kujilipua".
Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!
Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!
Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.
Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu!
Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vascoda Gama", baada ya shida kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani vyuo vimefungwa?
Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi#JIPANGE jombaaaaaaaaaaView attachment 1112538
Nimecheka mpaka machozi!,huu ni ukweli lakini unauma!
 
The real measure of intelligence is action. Sasa ww na degree yako umesoma maelezo ysko mwenzio kapita veta au kajifunza kivitendo zaidi unasema ww una akili kushinda yy ikiwa ww uwezi apply knowledge yako mtaani..
Daah mbona kama una bifu na wenye degree hivi? Kwani wamepunguza nini kwenye maisha yako ?
 
Rule moja ya watu wasiofanikiwa maishan ni watu wanaokuza mambo.
 
Back
Top Bottom