WASOMI" NA NDOTO ZA ABUNUASI

WASOMI" NA NDOTO ZA ABUNUASI

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,110
Reaction score
1,951
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na "vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa "kujilipua".
Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!
Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!
Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.
Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu!
Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vascoda Gama", baada ya shida kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani vyuo vimefungwa?
Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi#JIPANGE jombaaaaaaaaaa
FB_IMG_1559240357102.jpeg
 
Nimeona hii picha na uzi nimekumbuka kuna kadada kaliniletea pozi kisa kipo third year [emoji23][emoji23] kalifikiri mimi boya boya sasa kapo mtaani first year kakiniona kanatabasamu kweli yani ninakaambia welcome first year na bash litakuwa kwangu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
hahaaa kwamba welcome first year ya mtaa
 
Kuna rafiki yangu kila akirudi semester anavimba kujiona msomi ukicheki simu yake contact classmates wake Kawa save engineer kama wote.. Tutawasubiri wengi first year wakitaa akirudi kitaa kapigwa gap la kutosha
 
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na "vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa "kujilipua".
Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!
Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!
Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.
Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu!
Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vascoda Gama", baada ya shida kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani vyuo vimefungwa?
Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi#JIPANGE jombaaaaaaaaaaView attachment 1112538
Ni wivu tu.
 
Ila ninachoshangaa ni kwamba mtu ambaye hajasoma, akishindwa maisha wanamwambia ni kwasababu hakusoma.
Na ninachoshangaa kingine wale ambao hawakusoma na wanamaisha maziuri wanawaponda waliosoma, ila mda huohuo wanapeleka watoto wao chekechea ya million 2.
Lakin ninacho shangaa zaid ni kwamba wakati sisi tuliotoka chuo tukiisoma namba, waliofeli form four wanalia sana na kukata tamaa ya maisha.
 
M
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na "vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa "kujilipua".
Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!
Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!
Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.
Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu!
Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vascoda Gama", baada ya shida kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani vyuo vimefungwa?
Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi#JIPANGE jombaaaaaaaaaaView attachment 1112538
wenye kasumba mbaya hapa nadhani ni wewe na wengine wenye akili kama zako.

1.Hao wanaosoma vyuo unataka wafanye nini kwa wakati huu?

2.Age ya kuringa na kujidai huwa ni hiyo(kwa wale wenye hulka hiyo) haijalishi yupo chuo au mtaani.

3.Hii pengine ni stori ya maisha yako wewe ila haita-apply kwa wote.

Huwa nakereka sana mtu anajifanya kuwazodoa watoto wa wenzake kisa wapo chuo kwani we ulitaka wakiwa chuo wafanye nini hasa bila kwenda bash za pale Micasa,Maisha club?
Au ulitaka ukiwatongoza tu wakukubalie? wakikukatalia unasema wanajishaua kisa wapo 3rd year?
Kwani hukuwahi kumtongoza msichana ambaye hasomi chuo na akakukatalia?

Afterall,msoto baada ya chuo kwa watoto wa familia maskini ni suala la kawaida kabisa ambalo huwa mnalipa uzito kipuuzi sana.

Kwani kuna mtu gani maskini aliwahi kupata mafanikio bila kupitia kipindi cha msoto?
Au kwakuwa tu wao wanadegree?

Vijana wengi humaliza degree ya kwanza wakiwa na miaka 23-26 umri ambao bado mdogo sana kupambana na kufanya mambo makubwa,kwahiyo huwa sioni sababu ya mtu kushangaa kijana wa rika hili kula msoto wa maisha maana ndio kwaanza anaingia maisha ya kutafuta financial freedom.
 
kwasababu hakuna ajira haina maana watu wasisome, ELIMU ni bora na huwezi kumlinganisha mtu mwenye degree na aliyeishia darasa la saba... Leo utamuona aliyebahatika kuwa tajiri bila ya kusoma anamtafutia mwanae shule ya million 5 akasome halafu... ulimko chuo someni kwa bidii ni njia ya kutimiza ndoto zenu na tuliomaliza chuo tupambane kwa nguvu tutumie ELIMU tuliyoipata na tumuombe mungu tutatimiza ndoto zetu zinazoitwa za abunuasi
 
Sasa jaman, mtu bila kwenda shule ataijuaje dunia?
Ebu pata wasaa wa kuitizama hii video na kuiskiliza vzr upate kujifunza.
 
kwasababu hakuna ajira haina maana watu wasisome, ELIMU ni bora na huwezi kumlinganisha mtu mwenye degree na aliyeishia darasa la saba... Leo utamuona aliyebahatika kuwa tajiri bila ya kusoma anamtafutia mwanae shule ya million 5 akasome halafu... ulimko chuo someni kwa bidii ni njia ya kutimiza ndoto zenu na tuliomaliza chuo tupambane kwa nguvu tutumie ELIMU tuliyoipata na tumuombe mungu tutatimiza ndoto zetu zinazoitwa za abunuasi
Nani kakwambia kusoma ni kuwa Tajiri.. Nimeona umeandika.. Darasa la saba kabahatika kuwa Tajiri Bila kusoma.. Nna wasiwas na hata na usomi wako..
 
Back
Top Bottom