Wasomi maofisini wamejaa ushamba?

Bonesmen

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
929
991
Hivi kutreat equal Watu wote ni tatizo? kwanini maofisini mnataka mpaka mumjue huyu ni nani ndo mumpe customer care nzuri? Huu ni ushamba ndugu zangu siamini mtu alie elimika vyema akajenga dharau kwa wengine pasipokuwajua..Wengine tunapenda kuwa simple si lazima nikutajie wadhifa wangu ndio unihudumia poa..Jenga heshima na yoyote.
 
Pole sana, kuna wengine wanaumiza kichwa ukimuelekeza kuelewa mpaka keshokutwa, hapo utafanyaje?
 
hata humu wapo ngoja waje, niliwahi kuingia airtel hapo duh! ni shida aisee, hasa wadada wakipata nafasi wanajisahau sana
 
Labda kazi zao pia zinawafanya wawajue kwanza wateja wao wanafanya kazi gani?, kwa mfano madaktari anaweza kukuuliza kazi yako ili aweze kujua chanzo cha tatizo lako na jinsi ya kulitatua
 
Labda kazi zao pia zinawafanya wawajue kwanza wateja wao wanafanya kazi gani?, kwa mfano madaktari anaweza kukuuliza kazi yako ili aweze kujua chanzo cha tatizo lako na jinsi ya kulitatua
Hapana mkuu si dokta alieuliza ni taasisi tu ambayo utambulisho wangu hauna faida kwao na najisikia furaha kujitambulisha kama mwananchi wa kawaida mpaka nione hali tete Ndo nawaanzia taabu kweli kweli
 
Pole sana, kuna wengine wanaumiza kichwa ukimuelekeza kuelewa mpaka keshokutwa, hapo utafanyaje?
Uzuri huwa natembea na ID za kazi ivo naelewa akizidisha kuniweka pending ntampa tu utambulisho na kumletea tabu mpaka aniombe msamaha
 
Uzuri huwa natembea na ID za kazi ivo naelewa akizidisha kuniweka pending ntampa tu utambulisho na kumletea tabu mpaka aniombe msamaha
Sasa chukulia wewe ni mhudumu unafanya kazi za customer care, wanakuja wateja wakorofi sana, wengine wazito kuelewa, wengine hata elimu ya ustaarabu hakuna, mwingine anakuchafulia mood yako ya kufanya kazi, wakati mwingine unazongwa sana na kazi wateja wanakuona unawadharau wakati mwenyewe unajitune vizuri ili uweze kuwasaidia, kwa mtu aliyewahi kufanya kazi za customer care hatashangaa kuona watu wanavyolalamika customer care ya TZ ni mbovu, hii kazi yahitaji moyo sana.
Kwa mgeni wa kazi hii atafanya kazi vizuri sana mwanzoni baaadaaaaye ataanza kuchoka na wakati mwingine mood zinaanza kubadilika leo anafanya kazi vizuri sana kesho analipua, keshokutwa wateja wanamharibia siku, wanaofanya kazi hizi wana uvumilivu kwa kweli.
Customer care zinapishana, kuna zingine unatumia kichwa zingine hautumii kichwa, kwa hiyo lazima ujue hapa kwanini wakati mwingine huduma zinakuwa mbovu!
 
Uzuri huwa natembea na ID za kazi ivo naelewa akizidisha kuniweka pending ntampa tu utambulisho na kumletea tabu mpaka aniombe msamaha
Sasa wewe una tofauti gani na hao?!! Nyinyi ndio wale 'unanijua mimi'. ID yako ni yako na mwajiri wako huko customer care nzuri anastahili kila mteja bila kujali wewe ni nani.
 
Umekaa nae dk 10 anakupa shit tu...akija jua wadhaifa wako ndo na shkamoo anaanza kukupa..eti shkamoo bro karibu sana jamani..tena umkute ni demu anachachawa mbaya...Na wewe ndo wakati wako wakumpa shit.
 
Uzuri huwa natembea na ID za kazi ivo naelewa akizidisha kuniweka pending ntampa tu utambulisho na kumletea tabu mpaka aniombe msamaha
Wewe pamoja na huyo anayekuletea dharau tatizo lenu ni moja, unalingishia ID yako kunyenyekewa!! Kwa nini usiwe mtu wa kawaida ukahudumiwa na kuondoka..
 
Sasa wewe una tofauti gani na hao?!! Nyinyi ndio wale 'unanijua mimi'. ID yako ni yako na mwajiri wako huko customer care nzuri anastahili kila mteja bila kujali wewe ni nani.
Kama umenisoma apo juu huwa sitoi ID kama hakuna usumbufu mana naelewa haina umuhimu wa kuwa public au wengine kuijua but majukumu ni mengi basi panapobidi sina budi kufanya ivo nipate huduma haraka na kuendelea kulitumikia taifa kwa wakati
 
Wewe pamoja na huyo anayekuletea dharau tatizo lenu ni moja, unalingishia ID yako kunyenyekewa!! Kwa nini usiwe mtu wa kawaida ukahudumiwa na kuondoka..
Rejea hapo juu nimesema sipendi na wala sina ulimbukeni wakujulikana ID yangu but usumbufu unapokuwa too much inabidi tu sasa
 
tatizo hawakupata vyeti vyao kwa njia inayostahili, wameajiriwa kwa mlango wa nyuma ila sasa hivi wanaipata saa zote wanaishi kwa hofu ya kutumbuliwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom