Wasiwasi Wangu Kesi ya Mnyika

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,515
6,489
Kwa jinsi ninavyosoma kwenye vyombo vya habari (sijawahi hudhuria mahakamani), na kama kweli ndivyo ilivyo, nina wasiwasi ubunge wa Mnyika- Ubungo nao utatenguliwa. Sio kwa rushwa, matusi au kuiba kura ila kwa ushahidi uliotolewa mahakamani na aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi husika, na ushahidi ambao haujapingwa na upande wa Mnyika kuwa kuna kura kumi na nne elfu (14000) ambazo ni hewa na haijulikani ziliingiaje, japo ya kwamba Mnyika alimzidi mpinzani wake kwa kura 15000.
 
mahakama zenyewe ndo hizo tena!
siku zote sie tupo na mungu

Kwa kesi hii sio mahakama lawamani bali ni ushahidi wenyewe ulivyo hasa huo wa kura hewa. Mnyika ni mwanasiasa bora nisingipenda yamkute yaliyowakuta wengine. Yalikuwa ni makosa ya Returning Officer lakini kwa bahati mbaya inakuwa uchaguzi mzima.
 
tusubiri,tusikilize kama ilivyo sumbawanga town and arusha.Sometyms unknowngly CDM inakuwa popular.tym'll tell.
 
tusubiri,tusikilize kama ilivyo sumbawanga town and arusha.Sometyms unknowngly CDM inakuwa popular.tym'll tell.

Na mimi ndio maombi yangu CDM iendelee kupaa, ndio maana napatwa na hofu kila dalili ya kuyumba inapotokea.
 
Duh! Kweli magamba wabakaji kama ni hivi basi demokrasia inabakwa na magamba kibaya ni kwamba wakati demokrasia ina mimba karibia ya kujifungua bado magamba wanabaka hawaoni hata huruma kwa hiyo mimba ya mtoto demokrasia!!!!!????
 
Chapa Nalo Jr wasiwasi wako ni kuwa uchaguzi ukirudiwa CDM watashindwa? Kama alishinda kwa kura za halali na umaarufu umeongezeka hofu inatoka wapi?
 
Last edited by a moderator:
Chapa Nalo Jr wasiwasi wako ni kuwa uchaguzi ukirudiwa CDM watashindwa? Kama alishinda kwa kura za halali na umaarufu umeongezeka hofu inatoka wapi?

Hujui CCM wana kanuni mpya ya tangaza mgombea wa CCM hao wabishi tutakutana huku mbele mahakamani, mambo yanaenda mpaka karibia 2015, kule Arumeru vijana walisimama kidete na ingefanywa tofauti ingekuwa kiama, je na vijana wa DSM wana ujasiri wa Machalii wa huko kasikazini?

Zaidi ya yote marudio ya uchaguzi ni usumbufu na gharama kubwa, yote ikiwa ni makosa ya Returning Officer kuongeza kura hewa to polute the election results.
 
CCM inatangaza uchaguzi.
CCM inasimamia uchaguzi.
CCM inaendesha uchaguzi.
CCM inatangaza matokeo ya uchaguzi.
Halafu CCM inajiibia kura inampa CHADEMA.
CCM inafingua kesi dhidi ya CHADEMA
Yani najaribu kuielewa hii kitu kinaingia kinatoka kinaingia....
 
Hakuna haja ya kujadili kesi iliyopo mahakamani .tuiachie mahakama ifanye kazi yake.
 
Kwa jinsi ninavyosoma kwenye vyombo vya habari (sijawahi hudhuria mahakamani), na kama kweli ndivyo ilivyo, nina wasiwasi ubunge wa Mnyika- Ubungo nao utatenguliwa. Sio kwa rushwa, matusi au kuiba kura ila kwa ushahidi uliotolewa mahakamani na aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi husika, na ushahidi ambao haujapingwa na upande wa Mnyika kuwa kuna kura kumi na nne elfu (14000) ambazo ni hewa na haijulikani ziliingiaje, japo ya kwamba Mnyika alimzidi mpinzani wake kwa kura 15000.

Mkuu hata kama kura 14000 zikitolewa still zilizobaki zinamfanya Mnyika kuwa mshindi! Unless kuna hoja zaidi mimi sioni tatizo na hili! Halafu huyo msimamizi wa uchaguzi alimtangazaje Mnyika kuwa mshindi huku kuna kura zilizoongezeka huku baadaye anaenda kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya Mnyika?
 
wao wana mahakama, wana vyombo vya dola na hata maofisa wanaofanya madudu ili kufanikisha malengo ya mabosi wao lakini sisi tu MUNGU,hakuna mashaka wakitaka uchaguzi urudiwe hata kesho tena wamlete Nape apate haki ya chama chake
 
ccm ndo wezi kwa sababu wao ndio serikali inashughulikia mambo yote ya chaguzi nchini
 
si vizuri kusema ila nahisi magamba yamemkamata mnyika.... nahisi kabisa atapoteza hili jimbo maana ukiangalia kasoro za uchaguzi ni nyingi...... nachojiuliza magamba ndo wanaandaa uchaguzi, sijui inakuwaje wao waandaaji halafu lawama kwa watu wengine.... nadhani mambo mengine yanapikwa makusudi tu na hao hao
 
Back
Top Bottom