Wasiwasi : Jakaya kugombea urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasiwasi : Jakaya kugombea urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Nov 11, 2011.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 12,928
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Jamani, tuzizubaishwe na ukweli kwamba Jakaya ameshindwa GROSSLY kuiongoza serikali yetu,
  na kwamba hakubaliki kabisa hapa nchini kiasi cha kugaragazwa vibaya sana na DR kwenye
  uchaguzi wa mwaka jana tukategemea kwamba na yeye analielewa hilo na hivyo anajiandaa
  kukabidhi madaraka kwa mtu mwingine hapo 2015.

  Mawazo yangu yamenipeleka kwenye nchi mbalimbali Africa ambako marais waliopo madarakani
  walifikia kufanya maamuzi ya kulazimisha mabadiliko ya katiba za nchi zao ili zitengeneze mazingira ya
  wao kugombea hata baada ya kikomo kilichoainishwa kwenye katiba hizo kufikia. Huko nimeangalia
  ni sababu zipi hasa (tofauti na urafi wa madaraka) zilizowasukuma Marais hao kufikia maamuzi ya
  namna hiyo, nilichobaini ni kwamba, wengi wao walikuwa kwenye mikanganyiko kama aliyonayo
  Ndugu Jakaya.

  Baadhi yao ni
  Yoweli Kaguta Museveni (Uganda)
  Robert Mugabe (Zimbabwe)
  Blaise Compaore (Burkina Faso)
  Idris Beby (Chad)
  Omar Bongo (Gabon)
  Lansana Conte (Guinea)
  Gnassingbe Eyadema (Togo)

  Viongozi wote hawa katika nyakati ambazo walikuwa wakibadili katiba zao,
  walikuwa katikati ya changamoto ya kutokubaliwa na wananchi wao, na kulikuwa
  na kila dalili kwamba watakapoachia madaraka wataishia mikononi mwa vyombo
  vya sheria, ama wao wenye na familia zao, au maswahiba zao. Kitu ambacho
  watanzania tumeishaanza kukijadili dhidi ya Ben Mkapa na Jakaya.

  Wote hawa walishinda katika chaguzi hizo kwa hila za kutosha,na kwa msaada wa
  wa vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama.

  Kinachonipa wasiwasi kwa Jakaya ni king'ang'azi kinacholazimiswa kwamba yeye
  ndio awe na mamlaka ya kuchagua tume itakayosimamia mchakato wa uandikaji
  katiba mpya, na pia ndio awe na mamlaka ya kuteua members wa bunge la katiba.
  Kwa nini anang'ang'ania madaraka mazito namna hii, anataka kufanya nini Jakaya.

  Kitu kingine, ni mahaba ya matumizi ya nguvu za kijeshi kwa harakati za kidemocrasia
  yanayoendelea kushamiri hivi karibuni. matendo haya nayachukulia kama mazoezi
  ya kutumia nguvu za dora katika project kubwa zaidi huko tunakoelekea.

  Hata Ujeshi wa Jakaya, unanitia mashaka kama utatuacha watanzania salama, kwanza
  ukizingatia kwamba amekuwa a very big failure, nahofia anaweza kusukumwa na
  roho ya kutaka kuonyesha kwamba anaweza kufanya kitu, na hivyo kuishia kutuweka
  matatani.

  Mwisho, Kimya kingi kina Mshindo Mkubwa. Jakaya kawa Kimya sana, haeleweki
  anafikiria nini kichwani Mwake, Ukizingatia ameishapoteza Marafiki wote, kabaki na
  vigeugeu, wasiwasi wangu unaongezeka kwamba ataamua kujiokoa Mwenyewe

  Naomba tuufuatalie mchakato wa Uandikaji katiba Mpwa kwa Umakini.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bora JK agomee 2015 kuliko mnafiki SITTA
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 9,586
  Likes Received: 2,916
  Trophy Points: 280
  Inasemekana mama Salma ndiye mgombea wa CCM 2015 kwa kigezo kuwa wanataka mgombea mwanamke.
   
 4. B

  Bundajo JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nitajiua na kisha nitatembea uchi nchi nzima kama hilo litatokea.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  WEe kibaka tu. Huna jipya
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,484
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  Ni ndoto, alichokipata mwaka jana unadhani anaweza tena kugombea?
   
 7. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mpango huo ungewezekana kama angeanza huo mkakati alipopewa madaraka na Mkapa, sio sasa..! Tumia akili rahisi sana ya kulinganisha uelewa wa wananchi na uthabiti wa serikali iliyoko madarakani, kwa kifupi sasa hivi Umma una nguvu kubwa mbali sana kushinda serikali iliyopo kwenye madaraka. Kwa sasa akijaribu ataishia njiani na ita-backfire vibaya kuliko nchi zote kulikowahi kufanyika mambo haya kwenye bara la Afrika, nchi za uarabuni pia zimeleta mwamko mkubwa na huu ni wasiwasi mkubwa sana kwa serikali zetu kwa wakati huu. Kwanza nawashangaa sana Polisi kwa sasa hivi wanavyojaribu kuwaonyesha watanzania nguvu ya dola maana naona wanawazoeza watanzania vitu vya milipuko, kwa watanzania hili litakuwa jambo la kawaida muda si mrefu na utawaona hawakimbii tena polisi kwa lolote. Hata ukipitia thread nyingi hapa jamvini zinaongelea sana na kutumia sana mifano ya Libya na kwingineko, mapambano yanaendelea.
   
 8. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 12,928
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Sawa, Uoga unaweza kumusaidia asiingize kwenye udhalimu huu, lakini unadhani anaweza akawa ameamua
  kuondoka Ikulu na kuachana nayo kabisa kabisa.

  Moi alitaka kumuchia Uhuru Kenyatta.
  Ghadafi alitaka kumuacha Kijana wake
  Hussein Mubaraka alitaka kumuacha Kijana wake
  Jamaa wa Equitorial Guinea anampango wa kumuachia kijana wake
  Mkapa alitaka kumuachia Sumaye
  Joseph Kabila aliachiwa kiaina
  Jamaa wa Malawi anataka kumuachia mdogo wake.

  Kinachonitatiza nashindwa kuona Jakaya anampango wa kumuachia nani?
  ndo maana napata wasiwasi atalilia kuendelea
   
 9. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135

  Akitangaza tu Kugombea nakunywa SUMU tena ya PANYA
   
 10. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,405
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Utatembeaje uchi nchi nzima wakati utakua umeshakufa?
   
 11. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,539
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hana hamu na uchaguzi.kutoka mshindo hadi ushindi mwembamba unafikiri aturudi kwa watz tena.
   
 12. 2

  21DEC2012 Senior Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MUNGU tuepushe na hili balaa.
   
Loading...