GE2025 Wasira: Wewe unanung'unika tu maandamano utakula maandamano?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
654
Reaction score
1,598
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kunung'unika na kufikisha ujumbe wa changamoto mbalimbali kwa njia ya maandamano kumepitwa na wakati

1759135833149.jpeg

Amesema Watanzania wanataka maendeleo ukiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo itarahisisha shughuli za kiuchumi na ajira kwa wananchi.
Wasira amesema hayo Septemba 28, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kutoka majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, mjini Moshi.

"Wewe unanung'unika tu maandamano utakula maandamano, tunataka reli ya kisasa kwa sababu katika dunia inayoendelea tofauti ya nchi zetu na nchi zilizoendelea ni miundombinu, ukifika tu unaiona barabara pana, kuna reli inakwenda 'speed' kwa hiyo barabara inakwenda speed.

"Hakuna biashara ya kisasa ya kutunza vitu kwa matenga umebeba kichwani, hiyo ni biashara ya zamani, biashara ya kisasa ni ile inayokwenda 'very fast' and speed (inayolwenda haraka).

Kwa mujibu wa Wasira, Ilqni ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 inaelekeza reli kuunganisha Pugu (Dar es Salaam), Tanga na Arusha kupitia Mkoa wa Kilimanjaro.

"Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inataka reli iunganishe Pugu, Tanga na Arusha kupitia Kilimanjaro, na sisi Musoma kule hata isipokuja miaka mitano hii inayokuja mpaka Arusha tunaisubiri na ili tuipate tutahakikisha CCM inaendelea kushinda.

"Ilni inasema sasa Musoma tujenge bandari kama hatua ya kwanza ya kupokea reli na reli ikifika itakuwa inatokea Arusha inatuunganisha na Tanga na sisi tutafanya biashara kati ya Musoma na Port bell ya Uganda," amesema.

Amebainisha kuwa, kwa namna hiyo vijana watapata kazi kwenye reli na kwamba ni muhimu kutafuta majibu ya matatizo mapya mara kwa mara.

Amesisitiza kuwa, zipo njia sahihi na bora zaidi kufikisha ujumbe mahali husika hususan kwa njia ya amani.
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kunung'unika na kufikisha ujumbe wa changamoto mbalimbali kwa njia ya maandamano kumepitwa na wakati.

Amesema Watanzania wanataka maendeleo ukiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo itarahisisha shughuli za kiuchumi na ajira kwa wananchi.
View attachment 3480493
Wasira amesema hayo leo Septemba 28, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kutoka majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, mjini Moshi.

"Wewe unanung'unika tu maandamano utakula maandamano, tunataka reli ya kisasa kwa sababu katika dunia inayoendelea tofauti ya nchi zetu na nchi zilizoendelea ni miundombinu, ukifika tu unaiona barabara pana, kuna reli inakwenda 'speed' kwa hiyo barabara inakwenda speed.

"Hakuna biashara ya kisasa ya kutunza vitu kwa matenga umebeba kichwani, hiyo ni biashara ya zamani, biashara ya kisasa ni ile inayokwenda 'very fast' and speed (inayolwenda haraka).

Kwa mujibu wa Wasira, Ilqni ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 inaelekeza reli kuunganisha Pugu (Dar es Salaam), Tanga na Arusha kupitia Mkoa wa Kilimanjaro.

"Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inataka reli iunganishe Pugu, Tanga na Arusha kupitia Kilimanjaro, na sisi Musoma kule hata isipokuja miaka mitano hii inayokuja mpaka Arusha tunaisubiri na ili tuipate tutahakikisha CCM inaendelea kushinda.

"Ilni inasema sasa Musoma tujenge bandari kama hatua ya kwanza ya kupokea reli na reli ikifika itakuwa inatokea Arusha inatuunganisha na Tanga na sisi tutafanya biashara kati ya Musoma na Port bell ya Uganda," amesema.

Amebainisha kuwa, kwa namna hiyo vijana watapata kazi kwenye reli na kwamba ni muhimu kutafuta majibu ya matatizo mapya mara kwa mara.

Amesisitiza kuwa, zipo njia sahihi na bora zaidi kufikisha ujumbe mahali husika hususan kwa njia ya amani.
Huyu mzee Bwana wenda anatamani kwa sasa angekua na miaka 18
 
Wazee walioharibu kupata katiba mpya ni KIKWETE NA WASIRA
 
Hakuna mmiliki wa kadi ya kijani hata mmoja anaweza kuelewa maana ya maandamano, ngoja tuone siku husika ikifika.
 
Kwani unanilisha ? After all unachukua kodi zangu hence usinipangie jinsi ya kulalamika...

Nyerere kaondoka, yeye yupo, mwinyi, yeye yupo, mkapa, yeye yupo by Makongoro Nyerere
 
Huyu mzee ameungana na mange kimambi kiaina ktk kuhamasisha maandamano. Maana kila aendapo ajenda yake ni maandamano.

Mungu aendeelee kumpa hekima hii
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kunung'unika na kufikisha ujumbe wa changamoto mbalimbali kwa njia ya maandamano kumepitwa na wakati

Amesema Watanzania wanataka maendeleo ukiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo itarahisisha shughuli za kiuchumi na ajira kwa wananchi.
Wasira amesema hayo Septemba 28, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kutoka majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, mjini Moshi.

"Wewe unanung'unika tu maandamano utakula maandamano, tunataka reli ya kisasa kwa sababu katika dunia inayoendelea tofauti ya nchi zetu na nchi zilizoendelea ni miundombinu, ukifika tu unaiona barabara pana, kuna reli inakwenda 'speed' kwa hiyo barabara inakwenda speed.

"Hakuna biashara ya kisasa ya kutunza vitu kwa matenga umebeba kichwani, hiyo ni biashara ya zamani, biashara ya kisasa ni ile inayokwenda 'very fast' and speed (inayolwenda haraka).

Kwa mujibu wa Wasira, Ilqni ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 inaelekeza reli kuunganisha Pugu (Dar es Salaam), Tanga na Arusha kupitia Mkoa wa Kilimanjaro.

"Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inataka reli iunganishe Pugu, Tanga na Arusha kupitia Kilimanjaro, na sisi Musoma kule hata isipokuja miaka mitano hii inayokuja mpaka Arusha tunaisubiri na ili tuipate tutahakikisha CCM inaendelea kushinda.

"Ilni inasema sasa Musoma tujenge bandari kama hatua ya kwanza ya kupokea reli na reli ikifika itakuwa inatokea Arusha inatuunganisha na Tanga na sisi tutafanya biashara kati ya Musoma na Port bell ya Uganda," amesema.

Amebainisha kuwa, kwa namna hiyo vijana watapata kazi kwenye reli na kwamba ni muhimu kutafuta majibu ya matatizo mapya mara kwa mara.

Amesisitiza kuwa, zipo njia sahihi na bora zaidi kufikisha ujumbe mahali husika hususan kwa njia ya amani.

Kwani tunakula kura...?
 
Back
Top Bottom