wakuu, nyie ambao mnawasikiliza mtuambie kile wanachozungumza, sisi wengine tuko mbali na hilo ni jambo la muhimu, sio thread inaanzishwa halafu mnaponda tu, wengine hatujui hata nini kinaendelea,
Hata kama ni utumbo hebu mtujulishe nini kinazungumzwa huko..
Kaka wewe umenena jamani JF tusiwe tunaponda tuuuuu ila tuelimishe so, Mjadala ulikua kama ifuatavyo:-
-Wasira kasema na leo kweli nimemshagaa sana akua wasira kama ninayemjua katulia na kaongea jambo la msinngi kuwa mswada wa kupata katiba mpya utachapishwa kwa lugha ya kiswahili na pia umma utaelimishwa na kutoa maoni kupitia wabunge wao, vyombo vya habari NK na wabunge watapewa copy ili waende majimboni mwao kuelimisha.
-watu wasiwe na uoga wowote kuwa huu si mchakato wa kujadili katiba laa, huu ni mchakato wa kujadili kwenda kupata katiba mpya.
-mjadala kuhusu muungano kasema utajadiliwa ruksa ila kwa maudhui yake hapo sina utaalamu wanasheria naomba mtusaidie.
-Kasema maudhui ya kupata ktiba mpya ni sawa ila kwa maoni yake kuwa bado yapo mengine ya msingi yatachukuliwa kwenye hii ya sasa mfano; DINI kuna kifungu katika katiba ya sasa kimejitosheleza kuhusu serikali na madhehebu ya kidini sikifahamu vizuri.
Warema;
-ajikanyaga sana kuwa mswada aukua na kasoro yoyote
-jukumu la kuchagua tume huru tusahau kabisa ni jukumu la rais wa tz na znz kutokana na katiba ya sasa inavyosemwa so, nyie wanasheria naomba kabla ya kwenda kwenye mswada halisi embu tengueni hicho kipengele kinachomruhusu rais kuwa na mamlaka ya kuchagua tume ili hayo mamlaka yarudishwe kwa wananchi kwanza kuliko kulaamu tuuu then mwisho wake wanatupiga bao.
-wako kwenye mjadala hata kesho anaenda znz kujadili na mwanasheria wao ili wapate kauli mbiu kuhusu muungano.
-kamati or tume aitahusisha wanasiasa ila itateuliwa na rais kutoka watu mbalimbali kama kina shevji, bomani, etc so, hapa hata kama wanasiasa hawachaguliwi ila watakaochaguliwa nahisi ni mrengwa wa rais or kada wa chama ila kama wananchi watashirikiswa+wanaharakati kwenda kuchagua tume basi itakua huru tuwe makini hapa wajanja hawa.
Maswali:
znz-kunawakati walishawakilisha maoni yao kwenye tume ya mswada wa katiba ya znz moni 14 lakini hata moja alikuchukuliwa kwenye tume?
Jibu la warema: si lazima maoni yote yakubalike inawezekani yako au yangu yakakubalika lakini si yote yakubalike so, nawasiwasi hata haya maoni yetu si yote yatakubalika ila yakwao ndio yakayokubalika tuwe makini hapa wana JF.
Rais anakuaje na madaraka ya kutuchagulia tume? na ukizingatia yeye ni chama tawala na hatakao wachagua aidha watakua na mrengo wake?
Jibu kwa wasira- Ingawa katiba inasema ivyo na baadhi ya mifano aliyotoa pia alisema na hilo kama mnaliona halifai basi ni jambo la kulijadili.
So wana JF hapa zaidi ukiangalia majibu na katiba ya sasa naomba, naomba nyie kina tundu lissu akikisheni kabla ya kujadili huu mswada tengueni kile kifungu kinachomruhusu raisi kuteua tume au kuwa na madaraka ya kuchagulia katiba hiki ni muhuimu sana kabla ya yote
Nawakilisha