PreGE2025 Wasira: Amani ni lazima sasa kuna wanaosema haki, na sisi tunasema ndani ya amani kuna haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru na kuwapongeza viongozi wa Dini kwa ushauri kuhakikisha Nchi inaendelea kuwa na amani hususan kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na kubariki uchaguzi huo uendelee huku, kikisisitiza kuwa haidharau maoni yanayotolewa.

CCM imesisitiza kuwa haipuuzi ushauri mbalimbali unaotolewa kuelekea uchaguzi huo, lakini imesisitiza hautaahirishwa kwa kuwa mageuzi na mabadiliko ni jambo endelevu na haiwezi kuwa hoja ya kuahirisha uchaguzi.

Hayo yalielezwa leo Chamwino mkoani Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

"Uchaguzi utaendelea sio kwamba tunapuuza mawazo, tutaendelea kuzungumza mambo ambayo yanaendelea, na tunashukuru sana nchi imetulia. Viongozi wetu wa kiroho wametuongoza wametupa ushauri mzuri sana na mimi nashukuru sana kwa kututia moyo na kutuambia uchaguzi uendelee lakini kwa amani," alisema.

Wasira alisema CCM ni Chama kinachozungumza na kuhimiza amani ndio maana taifa limekuwa na utulivu kwa miaka 60, alisisitiza kwamba hilo linafanya Chama kijivunie kwa kuwa ni ushahidi kwamba kinaweza kusimamia amani.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Alisisitiza haki iko ndani ya amani na kwamba ukiondoa amani utavunja haki za watu wengi hususan wanyonge, "ukiondoa amani watakaoumia hasa ni wanawake, watoto na walemavu."

"Amani ni lazima sasa kuna wanaosema haki, na sisi tunasema ndani ya amani kuna haki, na haki hiyo inalindwa na amani kwa sababu ukiiondoa watu wengi wataathirika wala sio mtu mmoja ni wengi sana na ushahidi wake upo, sisi tumepokea wakimbizi maelfu kutokana na kuvunjia kwa amani kwa majirani zetu," alisisitiza
 
Huyu Babu anajua sana HOJA za Lissu, Uchaguzi sio wa HURU wala HAKI anajua sana lakini kwasababu kapewa Kibuyu cha Asali amejirusha UFAHAMU.

Bila HAKI hakuna AMANI.
 
..Haki huzaa amani. Ukichezea haki za watu utasababisha upotevu wa amani. Hicho ndicho kilichosababisha Gaddafi akafurumushwa.
 
View attachment 3313341

“Amani ni tunda la haki”, sio “Haki ni tunda la amani”!
 
Unatuwekea taarifa ya mtu asiyejuwa maana ya maneno anayoyatumia.
HAKI itakuwaje ndani ya AMANI; wakati HAKI ndiyo inayozalisha AMANI!
Mzee Wasira sasa anazungusha maneno tu kwa minajiri ya kuchanganya watu. Hana jipya.
 
Back
Top Bottom