Wasiotumia EFDs marufuku kufanya biashara na serikali

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
KUANZIA Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema hayo jana bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma jana. Aidha, Dk Mpango aliwapongeza wafanyabiashara walioitikia matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka kila mfanyabiashara isipokuwa wale ambao wametangazwa rasmi na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia mashine za EFD kutoa risiti kila anapouza bidhaa au huduma.

Alisema ili kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuhakikisha kwamba zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Umma na kanuni zake, alitangaza kuwa malipo yote lazima yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice) zilizotolewa na mashine za EFD.

“Kwa sababu hiyo kuanzia tarehe 1 Julai 2016, ni marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.
 
Ni wazo zuri, lakini wameziboresha hizo risiti? mana material yanayotumika yanafutika baada ya muda, itakua wakaguzi wakienda wanakutana na risiti zisizo na maandishi. Kabla ya huo mfumo kuanza kazi wahakikishe wameboresha ubora wa risiti zitokanazo na efd machine.
 
Licha ya EFD receipts kufutika, pia hazioneshi orodha ya bidhaa kwa kina. Specifications hazioneshwi ni risiti hizo. Mfano ukinunua computer itaishia tu kuandika computer, bila kuainisha kama ni computer ya DELL, 4 ports, 4GB, Processing speed pentium 4, warranty etc,etc these are necessary to determine value for money.
 
Back
Top Bottom