Wasioishiwa pumzi ya kuupinga ufisadi tunakutana hapa!

Yaani una shangaa kabisa kwamba mtu anasema kwamba hata kama ni mwizi tuna mtaka huyohuyo!! Yaani unajua kabisa ni fisi ila unataka umpe banda la nyama kweli!

ACT pekee ndio ina hoja muimu wengine wote wana tukanana tu

Tunampenda hivyo hivyo
 
Attachments

  • 1444819427572.jpg
    1444819427572.jpg
    70.5 KB · Views: 96
Lowasa sio fisadi

Kauli ya Mwalimu Nyerere Kuhusu Lowassa: NEC Dodoma 1995
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu." - Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995

mimi nataraji kuwa kama mwalimu angekuwepo leo hii kuna watu wangechezea bakora ile mbaya.
 
Mkuu umeongea point kubwa. Hivi excuse ya kumweka Lowassa ni nini? Kuimarisha chama?
How wakati sasa hivi Chadema kama institution imekufa hata nyimbo za kampeni ni kuhusu mahaba ya Lowassa?
Pili wana promote hii kitu kinaitwa Ukawa. Haipo na haijasajiliwa.
Leo Mbatia anampigia debe mgombea wa Chadema na hata katika matangazo yao ni dhahiri lazima wapigie kura Chadema. Yaani vyama vya CUF na NCCR mwaka huu hawapo ktk urais lakini hata majimboni. Wasichotambua Chadema ni kuwa hii inawapa tu life line ya muda lakini ni guaranteed death. CUF bara imeshakufa. Lowassa ni mharibifu, kila anakoenda anaharibu vitu na watu.
Agenda ya kupiga vita ufisadi na uadilifu ndiyo ilikuwa njia pekee ya kujihakikishia uendelevu kama chama!

Huyo huyo mwaribifu anatufaaaaaaaa
 
Dah! Kwanini nimechela kuiona thread hii!!

Posha!!!! Inanihusu hii, Mimi kwa sasa sina kadi ya chama chochote (tangu niichane chane kadi ya CDM) lkn nawaunga mkono ACT.

Na ungana na wale wote wanaopinga ufisadi nchini, ktk hili sintabadilika mpaka naingia kaburini.
 
Nashauri Mh Freeman Mbowe achukue fursa hii kukanusha tuhuma zilizozagaa kila kona ya nchi kuwa alipokea tsh 12 billioni kama gharama ya "kiingilio/registration fee" ya Lowassa chadema. Akishindwa kukanusha tuhuma hizo mbele ya jamii hii, nadhani tutakuwa tumetenda haki kama tukiifanyia amendment list of shame na kumuongeza Mh Freeman Mbowe

Wawezaje kukanusha ukweli usiojificha????
 
Wawezaje kukanusha ukweli usiojificha????

Hilo tope walilojipaka kina lissu,Mbowe,Msigwa na Mnyika litawatafuna kama jamaa anayegombea kupitia UKAWA leo hii.wao wanadhani litapita tu na sisi tutaeachekelea
 
Mabadiliko ya KWELI yataanzia Bungeni na siyo IKULU. Kama kuna mtu anadhani Lowassa ataleta mabadiliko basi ni au hajui nini maana ya Bunge au anajua (kama mimi) ila tu tunataka kumtumia Lowassa kuongeza nguvu ya kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani.
Dr Slaa alisaidia sana mwaka 2010 kwa kugombea Urais. Umaarufu wake wakati ule ulikuwa chachu ya Chadema kuvuta Wabunge wengi. Lowassa na ugonjwa wake, na ufisadi wake, kaweza kuwaunganisha UKAWA dakika za mwisho. Lipumba alikuwa atoe pigo la mwisho la UKAWA ila kuja kwa Lowassa, kulisaidia sana.
Lowassa unaweza ukamchukua kwa mabaya yake yote ila dakika za mwisho, amini usiamini ndiye kasaidia upinzani usisambaratike. Delila angelifanya vitu vyake dakika ya mwisho , tungelia na kusaga meno.

Maadamu Lowassa simpendi, sasa kwa nini namshangilia? Jibu ni rahisi: Asaidie kuwaunga UKAWA kupata wapinzani wengi. Mungu Ibariki Tanzania.

Sasa tujikite kuongeza wabunge wa upinzani tuachane na hii failed project ya 2015! Naamini tupo pamoja katika malengo ila approach ndo tumetofautiana!
 
Mabadiliko ya KWELI yataanzia Bungeni na siyo IKULU. Kama kuna mtu anadhani Lowassa ataleta mabadiliko basi ni au hajui nini maana ya Bunge au anajua (kama mimi) ila tu tunataka kumtumia Lowassa kuongeza nguvu ya kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani.
Dr Slaa alisaidia sana mwaka 2010 kwa kugombea Urais. Umaarufu wake wakati ule ulikuwa chachu ya Chadema kuvuta Wabunge wengi. Lowassa na ugonjwa wake, na ufisadi wake, kaweza kuwaunganisha UKAWA dakika za mwisho. Lipumba alikuwa atoe pigo la mwisho la UKAWA ila kuja kwa Lowassa, kulisaidia sana.
Lowassa unaweza ukamchukua kwa mabaya yake yote ila dakika za mwisho, amini usiamini ndiye kasaidia upinzani usisambaratike. Delila angelifanya vitu vyake dakika ya mwisho , tungelia na kusaga meno.

Maadamu Lowassa simpendi, sasa kwa nini namshangilia? Jibu ni rahisi: Asaidie kuwaunga UKAWA kupata wapinzani wengi. Mungu Ibariki Tanzania.
Chadema iliongezaje viti vya serikali za mitaa?

Tusitafute justification za ufisadi uliofanyika Ukawa...watu wamechukua mpunga wakaja na matokeo ya utafiti feki kuwa Slaa kachuja ha ha ha...

Ungeniambia mabadiliko ya kweli yanaanzia kwenye mitaa na udiwani labda ungekuwa na mantiki.

CCM/TANU haikupewa nchi wakiwa kama genge bali kama taasisi inayojitambua.
 
meningitis kelele peke yake hazitoshi bali hizo ni kampeni nje ya uwanja wa siasa za kuwachafua watu. kama kweli hii ni thread ya wapinga ufisadi na wachukia ufisadi basi na iwe darasa mahsusi kwa wote kwanza wafahamu nini maana halisi ya ufisadi na unabebwa vipi kwenye katiba na sheria za nchi. wajifunze nini hatua za kuchukua kuwezesha kuukomesha na nini mpiga kelele anacho kama ushahidi usio na shaka utakaotuwezesha kuwafungulia mashtaka mafisadi na serikali ishinde kesi. kwa kuanza kuchezesha mpira mimi nitazungumzia ufisadi uliofanyika wakati wa zoezi ove la uuzwaji nyumba za serikali ambapo ndani yake viongozi waligawa nyumba hizo kwa ndugu na vimada.huu ndio ufisadi wa mwanzo kujadiliwa ili sasa yale magazeti ya rai na mtanzania yaliyoanika ushahidi wa dhahiri dhidi ya vitendo hivyo yatusaidie kama sehemu ya ushahidi wa kuwafikisha wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine katika ufisadi huu. baada ya hapo tujadili fisadi nyinginezo kama richmond, epa, escrow; meli ya samaki, twiga waliotoroshwa pamoja na vijisenti vya waziri mmoja
Hii ni thread maalum ya wale wote wanaoukataa ufisadi katika mavazi yake yote.

Ni thread ya mashujaa wa kweli wanaopambana dhidi ya ufisadi hata pale unapojipa majina mapya!

Ni thread ya mashujaa na kwa ajili ya mashujaa wote waliosimama,wanaosimama na watakaoendelea kusimama dhidi ya mafisadi!

Ni thread ya waliopiga kelele na kuendelea kupiga kelele na watakaoendelea kupiga kelele dhidi ya mafisadi na ufisadi nchini Tanzania.

Ni thread kwa ajili ya waliowahi kuibuka,wanaoibuka na wayakaoibuka kuupinga ufisadi!

Ni thread ya kuunda umoja dhidi ya ufisadi uwe unatoka kwa CCM,CHADEMA,CUF au chama chochote au mwanasiasa yoyote anayesimama ipande wa ufisadi kwa nia yoyote ile.

Ni thread inayotambulisha maadui wakuu wa ufisadi Tanzania ili ikibidi historia iwahukumu katika hilo.

Ni katika thread hii ndio itatupasa kukumbushia aina ya ufisadi na mafisadi.

Ni katika thread hii tutatakiwa kuwataja na kuweka kumbukumbu na hukumu za kijamii dhidi ya mafisadi...yaani ukitajwa hapa ndio utakuwa umehukumiwa

Ni katika thread hii mtuhumiwa wa ufisadi ataweza kujitetea au kujisafisha.

Ni katika thread hii ushahidi wa ufisadi uyawekwa baada ya uthibitisho ukiwa na baraka za TCRA..

Hii iwe thread maalum ya mahakama ya kijamii ya mafisadi kwani sio serikali au vyama vya kisiasa vinavyoweza kuhukumu kwa haki na kutoa majibu ya nani hasa ni fisadi bali ni sisi pekee kama wana jamii forums ndio wenye mamlaka ya haki na huru na ya kimantiki ya kuhukumu mafisadi.

Thread hii iwe mwiba na eneo hatari kwa kiongozi kitajwa kwenye ufisadi.

Thread hii itumike kama laana ya kiongozi au yoyote yule awaye mtanzania kuhusishwa na ufisadi.

Orodha ya kweli na haki ya aibu (list of shame) iwekwe hapa.

Mods wawe na mandate ya kumfuta yule ambaye atasingiziwa ili tu aingizwe kwenye list yetu mpya ya ufisadi.

Thread hii isibebe Chama au mtu flani bali ibebe maslahi mapana ya nchi..!

Watu muhimu wenye michango yenye kura ya veto kwenye thread hii wawe kina ...

MzeeMwanakijiji Susuviri @Dr W.P Slaa Invisible na wengine ambao robot la JF litaona inafaa...

Let JF get back to its roots...!

Ni thread ya vizazi vyote vitakavyojiunga JF isiyoathiriwa na mihemko!

Thread hii iwe na gia moja tu isiwe na gia za angani au majini au ardhini..!!
 
Chadema iliongezaje viti vya serikali za mitaa?

Tusitafute justification za ufisadi uliofanyika Ukawa...watu wamechukua mpunga wakaja na matokeo ya utafiti feki kuwa Slaa kachuja ha ha ha...

Ungeniambia mabadiliko ya kweli yanaanzia kwenye mitaa na udiwani labda ungekuwa na mantiki.

CCM/TANU haikupewa nchi wakiwa kama genge bali kama taasisi inayojitambua.

ESCROW ndio ilisaidia CHADEMA kupata viti vingi kwenye serikali za mitaa baada ya hapo Watanzania tukasahau ndio maana hadi muda huu watu wanazungumzia ufisadi wa UZWAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI NA RICHMOND TU.
 
kabla hamjakanusha ukweli mnaodai usiojificha kwanza muwatake wale wote waliopata mgao wa escrow kutoka kwa harbinder singh pale standard chartered waanze kukanusha tuhuma zilizozagaa awali kabisa kila kona ya nchi mpaka nje ya nchi. mkishindwa kuwataka wafanye hivyo na wakishindwa kutoa maelezo sadifu basi tutakuwa tumetenda haki kama tukiwaongeza kwenye list ya wazushi na warongo
Wawezaje kukanusha ukweli usiojificha????
 
jingalao huu ujinga mlioufanya wa kumlisha marehemu baba wa taifa maneno ambayo kamwe hakuyatamka na hayapo kabisa katika kumbukumbu zake zote utawatokea puani pale TCRA watakapowataka mupeleke uthibitisho

mimi nataraji kuwa kama mwalimu angekuwepo leo hii kuna watu wangechezea bakora ile mbaya.
 
meningitis kelele peke yake hazitoshi bali hizo ni kampeni nje ya uwanja wa siasa za kuwachafua watu. kama kweli hii ni thread ya wapinga ufisadi na wachukia ufisadi basi na iwe darasa mahsusi kwa wote kwanza wafahamu nini maana halisi ya ufisadi na unabebwa vipi kwenye katiba na sheria za nchi. wajifunze nini hatua za kuchukua kuwezesha kuukomesha na nini mpiga kelele anacho kama ushahidi usio na shaka utakaotuwezesha kuwafungulia mashtaka mafisadi na serikali ishinde kesi. kwa kuanza kuchezesha mpira mimi nitazungumzia ufisadi uliofanyika wakati wa zoezi ove la uuzwaji nyumba za serikali ambapo ndani yake viongozi waligawa nyumba hizo kwa ndugu na vimada.huu ndio ufisadi wa mwanzo kujadiliwa ili sasa yale magazeti ya rai na mtanzania yaliyoanika ushahidi wa dhahiri dhidi ya vitendo hivyo yatusaidie kama sehemu ya ushahidi wa kuwafikisha wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine katika ufisadi huu. baada ya hapo tujadili fisadi nyinginezo kama richmond, epa, escrow; meli ya samaki, twiga waliotoroshwa pamoja na vijisenti vya waziri mmoja

Mkuu nimeupenda ushauri wako kuhusu kuwa na common understanding ya nani hasa ni fisadi au ufisadi ni kitu gani.
Hilo litaboreshwa kadri siku zinavyoenda.

Naamini tukiwa na uelewa wa pamoja tutakuwa na uwezo wa kutofautisha fisadi anayekataliwa na magwiji wa ufisadi nakukubaliwa na waliojiita wapinga ufisadi versus yule anayekubaliwa na magwiji wa ufisadi na kupingwa na wanaojiita wapinga ufisadi.

Mkuu jisikie huru kushusha nondo zote ili kila anayetajwa humu iwe halali yake kweli.Jitahidi kama mimi ninavyojaribu hapa kutokuwa biased.

''be as wise as the serpent you encounter''
 
kabla hamjakanusha ukweli mnaodai usiojificha kwanza muwatake wale wote waliopata mgao wa escrow kutoka kwa harbinder singh pale standard chartered waanze kukanusha tuhuma zilizozagaa awali kabisa kila kona ya nchi mpaka nje ya nchi. mkishindwa kuwataka wafanye hivyo na wakishindwa kutoa maelezo sadifu basi tutakuwa tumetenda haki kama tukiwaongeza kwenye list ya wazushi na warongo

Naona mkuu unakuja kwenye njia sahihi.
Kwenye uchaguzi huu hatukutakiwa kupotezwa kwenye ajenda ya msingi ya kuwakataa kwa sababu ni mafisadi.

Nilitegemea Chadema na pengine Ccm iteue wagombea wake kwa kuzingatia uadilifu hasa hasa eneo la ufisadi.

Nilitegemea mwaka huu wa uchaguzi kuwa ni hukumu kuu ya wote wanaotuhumiwa kuwa mafisadi.

Sasa kuna mtu ghafla ghafla katutoa kwenye ajenda hiyo na kuifanya kutojadilika au kuifanya ya kawaida sana.

Sijayasikia haya mawe ya escrow,nyumba,epa,richmond yakivuma mara baada ya julai 28.

Madhara ya jambo hili sio madogo,sasa hivi hakuna anayemkumbuka 'tumbili' ambaye amefunguliwa kesi.

Mafisadi wamepata nguvu baada ya kuwa mapilot wa ndege iliyokuwa ituvushe dhidi ya ufisadi.

Ndio maana nakuja na hoja hii ya kutokuishiwa pumzi kamwe kwani kwa kufanya hivyo ni kukaribisha mikandamizo zaidi kutoka kwa mafisadi.

Na siku moja wajukuu watakuwa wanapiga viboko makaburi yetu.
 
Mleta mada hata wewe kwenye eneo lako la kazi utakua unafanya ufisadi indirectly
 
Ndiyo maana nilikuambia kuwa CCM walishammaliza Dr Slaa kwani sifa pekee aliyokuwa anajulikana nayo ni UFISADI.

Waliruhusu makusudi Ufisadi usemwe wazi na mzigo wote akabebeshwa Lowassa wakati siyo kweli.

Ukiniambia Escrow Lowassa alilamba ngapi? Ntailipia kadi yangu ya CCM. Ukiniambia fedha zilizopotea Wizara ya Magufuli Lowassa alikula ngapi? Tatizo lenu ni kutufanya hatuna akili kwa kutulisha upuuzi wenu kuwa Fisadi ni Lowassa peke yake. Nchi ni giza, miaka 10 ya Kikwete bado anaiacha nchi giza. Lawama apewe Lowassa aliyeondoka miaka 8 iliyopita.

Slaa alishapoteza umaarufu wake kwa namna moja au nyingine. Asingeliweza kushindana na CCM hata kidogo. Na ili kuonyesha hilo, serikali za Mitaa, Chadema walifanya vibaya sana. Hata wewe umelijua hilo na umeliandika hapa kwenye BOLD. Sasa ili kutibu hilo tatizo, LOWASSA kaja na kibao kimegeuka. Mnahemewa Kisogoni kwa mara ya kwanza.

Hata kwa Mbinde, safari hii lazima Lowassa awachukue.

https://www.youtube.com/watch?v=mnAlHuGWOFg

Back
Top Bottom