Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 318
- 662
Bila shaka umeshasikia watu wanaojiita “Atheist” yani, wasioamini katika uwepo wa Mungu. Ifahamike kwamba Atheism sio dini. Ni neno tu linalotumika kumuelezea mtu asiyeamini katika uwepo wa Mungu.
Imani yao inasukumwa na tamanio la Mwanadamu la kutaka kujitawala mwenyewe. Ikumbukwe kuwa kiu ya Mwanadamu imelala katika vitu vikuu vitatu yani, FEDHA, MALI na MAMLAKA/MADARAKA. Katika hili la atheist, nitajikita zaidi kwenye Mamlaka.
Ni asili ya Mwanadamu kukataa kuwa chini ya mamlaka yoyote. Mathalani; asilimia kubwa ya watu hawapendi utawala wa kiserikali katika nchi zao kwasababu hawapendi kujiona wapo chini ya mamlaka fulani. Hata katika jamii za kawaida, mifumo ya kiutawala ni chukizo kwa wengi kwasababu Mwanadamu hapendi kuwa chini ya sheria.
Ndivyo ilivyo kwa Atheists. Hawataki nafsi zao ziwahukumu kwa yale wanayoyafanya sirini. Kwasababu ili nafsi ikuhukumu, lazima uwe na hofu ya Mungu. Atheists wanaamini wao ndo wana-control maisha yao na kuamua vile wanavyotaka yawe. Hawaamini kwamba ipo nguvu inayofanya mambo yote yawe kama yalivyo.