Wasifu wa Siti Binti Saad

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,454
Siti binti Saad alizaliwa katika kijiji cha Fumba, Zanzibari mwaka 1880. Alipozaliwa alipewa jina la 'Mtumwa' hii ni kwa vile alizaliwa katika kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na mkabaila mmoja wa kiarabu.

Baba yake bwana Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na Mama yake alikuwa ni Mzigua toka Tanga, lakini wote wawili walizaliwa Zanzibari. Hali ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha zaidi katika shughuli za kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri pia.

75a4d3b2e35def1ca580f43c31c654a7.gif

Kama waswahili wasemavyo 'kuzaliwa masikini si kufa masikini' Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji. Kipaji hiki kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza. Siti alipoimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali wa maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo.

Alifananishwa kuwa na mapafu yenye nguvu kama ya simba kutokana na alivyoweza kupaza sauti yake mbali na bila kuachia pumzi.

Kutokana na wakati huo elimu kwa watoto wa kike haikutiliwa mkazo, Siti hakuwahi kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya Kurani.

Hivyo mnamo mwaka 1911 aliona ni bora ahamie mjini ili kubooresha maisha yake zaidi. Ujio wake wa mjini ulikuwa wa neema kwani alikutana na bwana mmoja wa kundi la muziki wa Taarabu la "Nadi Ikhwani Safaa" aliyeitwa Muhsin Ali. Katika kipindi hicho hilo ndilo lilikuwa kundi pekee la muziki wa taarabu lililoanzishwa na Sultani mpenda starehe na anasa bwana Seyyid Barghash Said. Kundi hili lilikuwa ni la wanaume peke yake, wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na vikundi vya muziki kwa vile ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni.

ASAIDIWA NA BWANA MUHSIN ALI
Bwana Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Siti na hivyo akajitolea kumfundisha kuimba kwa kufuata vyombo vya muziki na lugha ya kiarabu. Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenzie wa "Nadi Ikhwani Safaa" ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonyesho mbalimbali katika jamii. Walipata mialiko mingi hasa kutoka kwa Sultani na matajiri wengine wa Kiarabu, pia katika maharusi na sherehe zingine mbalimbali

13966039573b828cd628702581fcd97e.jpg
9f2e55e94495df83a65b353a3197c951.jpg
Inasemekana ulifika wakati ambapo sherehe ilishindwa kufana kama Siti binti Saadi hakuwepo kutumbuiza. Siti alikuwa ni moto wa kuotea mbali na jina lake lilivuma kwa haraka sana hadi nje ya mipaka ya nchi na bara la Afrika. Na punde Siti alianza kufananishwa na 'Umm Kulthum', mwimbaji mahiri wa kike aliyetamba wakati huo kutoka Misri.

Kama nilivyosema moto wa Siti ulikuwa si wa kuusogelea karibu, mwaka 1928 kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's voice yenye makazi yake Mumbai India ilisikia umaarufu wa Siti binti Saadi na hivyo ikamwalika yeye pamoja na kundi lake kwenda kurekodi kwa lugha ya Kiswahili ili kujaribu kama muziki wake utauzika. Kampuni ile haikuweza kuamini jinsi muziki ule ulivyouzika kwa kasi kubwa kwani wastani wa santuri 900 ziliweza kuuzika katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo, na hadi kufikia 1931 santuri 72,000 zilikuwa zimeuzwa. Kutokana na kusambaa kwa santuri hizi, umaarufu wa Siti ulizidi mara dufu watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikuwa wakija Zanzibari kuja kumwona. Mambo yalizidi kuwa mazuri kwa Siti hadi ikafikia hatua kampuni ya kurekodi ya Columbia kuamua kujenga studio ya kurekodi muziki palepale Zanzibar maalumu kwa ajili ya Siti binti Saadi.

AANZA KUONEWA WIVU
Hatua hiyo ya hadi kujengewa studio iliwaumiza wengi wenye wivu, hivyo wakaanza kumtungia nyimbo za kumkejeli ili kumshusha na hasa walitumia kigezo kwamba hana uzuri wa sura, nyimbo nyingi ziliimbwa lakini huu ndio uliovuma sana:

Siti binti Saadi kawa mtu lini,
Kaja mjini na kaniki chini,
Kama si sauti angekula nini?


Na yeye kwa kujua hila za wabaya wake, akaona isiwe taabu akajibu shambulio namna hii:-

Si hoja uzuri,
Na sura jamali,
Kuwa mtukufu,
Na jadi kebeli,
Hasara ya mtu,
Kukosa akili.


Kwa kujibu shambulio hilo kwa namna yake aliwafunga midomo wale wote waliokuwa wakimfuatafuata.

Siti pia alikuwa ni mwanamke wa kwanza mwanaharakati katika kipindi chake, alitetea wanawake na wanyonge kwa ujumla, kwani katika kipindi chake watu matajiri walikuwa wakiwaonea masikini na walipofikishwa mbele ya haki waliweza kutoa hongo na kuachiwa huru halafu wewe uliyeshitaki ndiye unayefungwa.

Utunzi wake wa wimbo wa Kijiti ulimpatia sifa kubwa kwani ulikuwa ukielezea kisa cha kweli kilichomkuta mwanamke mmoja mgeni kutoka bara,

Mwanamke huyu alipofika alikutana na Tajiri mmoja ambaye alijifanya amempenda, hivyo akamchukua na kulala naye halafu baadaye akamuua. Tajiri yule alishitakiwa na bahati nzuri walikuwepo mashahidi wawili walioshuhudia tukio lile, lakini kwa vile ni Tajiri alitoa pesa na kesi ikawageukia wale mashahidi na kufungwa.
Siti akatoa wimbo huu :-

Tazameni tazameni,
Eti alofanya Kijiti,
Kumchukua mgeni,
Kumcheza foliti,
Kenda naye maguguni,
Kamrejesha maiti.


Siti aliendelea kumwambia katika nyimbo zake kwamba asijethubutu kwenda Dar er Salaam kwa maana watu wenye hasira wanamsubiri na wameapa kwa ajili yake.

MWISHO WA UHAI WAKE
Siti aliendelea na shughuli yake ya muziki hadi uzeeni, muda mfupi kabla ya kifo chake alikutana na mwandishi maarufu na mwanamashairi Shaaban Robert ambaye alimhoji na kuweza kuandika wasifu wake katika kitabu alichokiita " Wasifu wa Siti binti Saadi."

ac5586acbab036079163d6a9f70698e7.jpg
Wasifu huu unaonekana kuwa ndio bora zaidi uliowahi kuandikwa katika fasihi ya Tanzania. Kitabu hiki kinatumika kufundishia shule za sekondari za Tanzania.

91436b4633642e757ed779b6547b1e82.jpg
Tarehe 8 Julai 1950 Siti binti Saadi alifariki dunia na kuacha pengo kubwa katika fani ya Taarabu. Ingawa pengo hilo haliwezi kuzibika lakini kuna watu wengi walioweza kuibuka na umaarufu wa kuimba taarabu kupitia kwake, mfano hai ni Bi Kidude.

Hata baada ya kifo chake jina lake bado linatumika sana kama kielelezo cha ushujaa wake, Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), kimetumia jina lake kulipa jina gazeti la chama chao "Sauti ya Siti". Hadi leo hii Siti hutumika kama kipimo cha kufundishia uimbaji wa Taarabu. Na anakumbukwa katika historia yake ya kuwa mwanamke wa kwanza Afrika mashariki kurekodi muziki katika santuri.

Ramadhan Kareem
 
Wow! Wasifu mzuri sana huu, kuna mambo ya kujifunza hasa kwa watu walivyofanikiwa zamani, na ukilinganisha na wakati huu.

Msolo
 
Ama Hakika Wasifu WA Siti Bint Saad kilichoandikwa na Komredi Shaaban Robart ni Wasifu bora kabisa kwa Siti.

Katika andiko lile limeelezea kwa kina Sana juu ya asili ya Siti, Harakat zake za maisha, ustawi wake katika muziki waTaarabu mpaka kifo chake.

Kwa upande wangu Wasifu ule ni Kati ya vitabu bora nilivyowahi kuvisoma na kunivutia, Hali inayopelekea kuusoma Mara kwa Mara, tena na tena.
Nukuu moja wapo katika Wasifu hule Ni
"Wazuri wana BAHATI zao, Wabaya wana VIPAWA vyao vilevile".

Shaaban Mwana WA Robart na Siti Bint WA Mzee Saad Hakika wameacha alama ambazo zitaishi karne nyingiii Sana bila ya kufutika kutokana na mambo ambayo wameyafanya katika nyakati zao.

Hakika kwa upande wangu ni Kati ya binadamu ambao huwa Natamani Sana ningelikuwa kwenye nyakati zao.

Mungu awapumzishe Kwa amani katika ufalme wake.

Nawasilisha.
 
Wakuu!

Kwa anaeijua vizuri historia ya siti binti saadi aishushe humu jamvini.

Nimesikia jina lake kwenye nyimbo moja ya bongo flava WHO AM I ? Nyimbo ya msanii RAPCHA ni muhimu sana tujue historia za watu wetu
 
Back
Top Bottom