Wasifu (CV) ya Dr. John Pombe Magufuli

Wasaalam wakuu
Nimeawaza sana baada ya kuona taarifa za mkuu wikipedia zisizoeleweka kuhusu raisi wetu mpendwa.Wameonyesha amesoma advance mkwawa secondary je kuna ukweli?kama ni kweli mbona hakwenda kusoma degree ya ualimu akaenda kusoma diploma hapo mkwawa au alifeli hiyo advance.
Na miaka yake ya kumaliza kidato cha nne mbona haijatimia.
Kama wikipedia ni waongo naombeni source itayonipa taarifa za uhakika.

John Joseph Magufuli started his education at The Chato Primary School from 1967 to 1974 and went on to The Katoke Seminary in Biharamulo for his secondary education from 1975 to 1977 before relocating to Lake Secondary School in 1977 and completing in 1978. He joined Mkwawa High School for his A levels in 1979 and completed 1981. That same year he joined Mkwawa College of Education for a Diploma in Education Science, majoring in Chemistry, Mathematics and Education.[2]
 
Alifukuzwa seminari akaenda Lake Mwanza.
kufukuzwa seminari sio kitu cha ajabu sana kitu cha ajabu ni kupata division zero Ihungo sekondari kama nanilii
 
Wasaalam wakuu
Nimeawaza sana baada ya kuona taarifa za mkuu wikipedia zisizoeleweka kuhusu raisi wetu mpendwa.Wameonyesha amesoma advance mkwawa secondary je kuna ukweli?kama ni kweli mbona hakwenda kusoma degree ya ualimu akaenda kusoma diploma hapo mkwawa au alifeli hiyo advance.
Na miaka yake ya kumaliza kidato cha nne mbona haijatimia.
Kama wikipedia ni waongo naombeni source itayonipa taarifa za uhakika.

John Joseph Magufuli started his education at The Chato Primary School from 1967 to 1974 and went on to The Katoke Seminary in Biharamulo for his secondary education from 1975 to 1977 before relocating to Lake Secondary School in 1977 and completing in 1978. He joined Mkwawa High School for his A levels in 1979 and completed 1981. That same year he joined Mkwawa College of Education for a Diploma in Education Science, majoring in Chemistry, Mathematics and Education.[2]
Inaonekana wewe ni wa juzi na hujui shule kama Mkwawa High Schoo, Korogwe, Shicom, hizi shule ulikuwa unajiunga na kusoma miaka miwili ya Advaced then mwaka mmoja wa Diploma ya ualimu
 
Aliishia form three pale Katoke baada ya kibomoa dirisha na kutoroka. Alimalizia Lake sekondari.
 
Achana na smart people wa enzi hizo walioenda UDSM straigh from A level . Wengine walipiga mesele kwanza.
 
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, ambaye anatoka Chama cha Mapinduzi, kitaaluma ni mwalimu na mtalaamu wa kemia.

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Kagera, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi huko huko Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1975 na baadaye akajiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza mwaka 1977 hadi 1978.

Kiongozi huyo alijiunga na chuo cha ualimu cha Mkwawa kilichoko Iringa, Kusini mashariki mwa Tanzania kati ya mwaka 1979 na 1982 ambapo alitunukiwa Stahahada ya Ualimu.

Baada ya kufuzu, alifundisha masomo ya hisabati na kemia katika shule mbalimbali za sekondari kuanzia mwaka 1983.

Magufuli hakuishia hapo kielemu kwani aliamua kujiendeleza zaidi na kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 hadi 1988 ambapo alitunukiwa shahada ya ualimu katika masomo ya kemia na hisabati.

Baadaye, aliamua kukolea katika kemia na akarejea chuoni na kusoma hadi ngazi ya udaktari.

Siasa za Tanzania

Katika siasa, Magufuli mwanzoni hakujulikana sana hadi nyota yake ya kisiasa ilipoanza kung'aa pale alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995.

Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na baadaye akapanda ngazi hadi kuwa waziri kamili, nafasi aliyoishikilia hadi hivi sasa.

Kwa mujibu wa majirani wanaoishi karibu na nyumba yake jijini Dar es Salaam, yeye ni mtu anayeishi maisha ya kawaida.

Wakati watoto wa baadhi ya viongozi wakisoma shule za hali ya juu watoto wake wamesoma katika shule za kawaida.

Alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25, 2015, mpinzani wake mkuu akiwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa wa chama cha Chadema chini ya muungano wa Ukawa, na akaapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Novemba 5, 2015.

Elimu

2006 - 2009: PhD (Kemia ); Chuo Kikuu cha Dar es salaam

1991 - 1994: Msc. (Kemia); Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza

1985 - 1988: Shahada ya kwanza katika Ualimu (Kemia na Hisabati);Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

1981 - 1982: Diploma ya Ualimu masomo ya Sayansi; Chuo cha Ualimu cha Mkwawa Masomo makuu Kemia, Hisabati na Ualimu.

1979 - 1981: Kidato cha tano na sita, Shule ya Upili ya Mkwawa, Iringa

1977 - 1978: Elimu ya sekondari, Shule ya upili ya Lake, Mwanza

1975 - 1977: Katoke Seminary, Biharamulo, Kagera

1967 - 1974: Shule ya Msingi, Shule ya Msingi Chato - Kagera

Mafunzo ya kijeshi

Machi 1984 - Juni 1984: Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa - Dodoma

Januari 1984 - Machi 1984: Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni- Arusha

Julai 1983 - Desemba 1983: Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora - Dodoma.

Uchambuzi wa Marcus Mpangala

Mafanikio na changamoto ndani ya miaka mitano ya Rais Magufuli

Ngwe ya kwanza ya miaka mitano (2015-2020) ya rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli imefika tamati, lakini ameteuliwa tena na chama tawala CCM kuwania nafasi hiyo kipindi cha pili (2020-2025) huku kukiwa na taswira chanya na hasi katika uongozi wake kuelekea uchaguzi mkuu wa urais,ubunge na udiwani utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu ambapo atamenyana na wagombea wengine takribani 14.

Tangu mwezi Novemba mwaka 2015 serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani kumekuwa na mafanikio ambayo yanawapa kifua mbele ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu barabara,meli,viwanja vya ndege,ununuzi wa ndege,umeme,kufanya operesheni ya vyeti feki, kupambana rushwa, dawa za kulevya na utoaji wa elimu bure kwa kutaja machache.

Hata hivyo uongozi wake unalaumiwa kuporomoka uhuru wa habari,sekta binafsi, uhuru wa kutoa maoni,kuzuiwa mikutano ya hadhara ya kisiasa kitaifa,kuzorota hali ya usalama wa raia na uhusiano hafifu wa kidiplomasia.

Ni mafanikio gani aliyopata kwa miaka mitano?Uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano, Rais Magufuli ameonesha uthubutu na mabadiliko katika maeneo kadhaa ambayo duru za kisiasa zinabainisha kuwa huenda baadhi ya wapigakura wapya kati ya milioni 7 wakavutiwa mafanikio aliyopata kwa miaka mitano.

'Kuvunja mifupa migumu'; kiongozi huyo ameonesha uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo kutekeleza mipango iliyokuwa imeshindikana takribani miaka 40. Mojawapo ni kutekeleza mipango iliyopitishwa katika serikali ya awamu ya kwanza chini ya Julius Nyerere kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma.

Utekelezaji wa mpango wa mradi wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji ni miongoni mwa mafanikio yake

Halmashauri Kuu ya TANU (sasa CCM) ilipitisha mpango wa kuhamia Dodoma, lakini serikali hiyo hhaikuweza kutekeleza adi ilipoondoka madarakani mwaka 1984 haikukamilisha. Serikali ya awamu ya tatu ya Rais Mkapa ilihamisha wizara ya kilimo na ushirika jijini Dodoma lakini haikudumu huko, baadaye zilirejeshwa Dar es salaam.

Aidha, uamuzi wa kutekeleza mpango wa mradi wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji nao umetajwa kuwa ni mafanikio kwa serikali hiyo. Mradi huo umesuasua kwa miaka mingi, pamoja na kukumbana na changamoto wana mazingira lakini rais huyo ameshikilia msimamo wa serikali yake kujenga mradi wa umeme na ndiyo siri ya awamu ya tano.

Miradi ya kiuchumi: Mosi, sera ya viwanda SIDP (Sustainable Industrial Development Policy) ya mwaka 1996 inabainisha kuwa Tanzania hadi mwaka 2015 ilitakiwa kuwa na viwanda vya kati.

Sera hiyo ilipitishwa na serikali ya awamu ya tatu ya serikali ya rais Benjamin Mkapa na waziri wa viwanda na biashara wa wakati huo alikuwa Dkt. Abdallah Kigoda. Hata hivyo sera ya viwanda imepigiwa upatu na serikali ya awamu ya tano tangu kuingia madarakani. Serikali imefanya jitihada kuvutia wawekezaji na kusisitiza ujenzi wa viwanda kwa wadau mbalimbali wa uzalisha,biashara na uchumi.

Pili, kuanzishwa vitambulisho vya machinga; Mwaka 2003 Profesa Hernando de Soto aliyekuwa mshauri wa serikali ya awamu ya tatu ya rais Benjamin Mkapa alipendekeza serikalini kuanzishwa mpango wa MKURABITA, ambapo aliainisha umuhimu wa kurasimisha biashara zisizo rasmi mfano Mama Lishe,saluni,wamachinga na wafanyabiashara wengine wenye mitaji ya chini milioni moja.


[https://ichef]
CHANZO CHA PICHA,IKULU TANZANIA

Serikali ya awamu ya tano imetumia mpango huo vizuri na kupata mafanikio kwa kusajili vijana wengi waliojihusisha na biashara ya umachinga. Uongozi wake umerasimisha shughuli za wamachinga na Mama Lishe, pamoja na wajasiriamali wadogo kwa kutengeneza vitambulisho vya kuwatambua. Kundi hili linatajwa na wataalamu wa uchumi na siasa kwamba limebeba matumaini ya CCM kupata kura za ushindi katika uchaguzi ujao.

Tatu, ununuzi wa ndege; Kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2015-2020 imeelezea suala la matengenezo ya viwanja na kufufua Shirika la Ndege (ATCL). Jumla ya ndege 11 zimenunuliwa na mamlaka za Tanzania. Hili ni eneo jingine linalotarajiwa kumwongezea wapigakura Rais Magufuli wakati wa kampeni. Matarajio ni ndege hizo kuongeza kiwango cha biashara ya utalii nchini humo pamoja na shughuli zingine za kiuchumi.

Sekta ya afya; mpango wa kuongeza vituo vya kutoa huduma za matibabu ya magonjwa kama vile saratani kwenye Hospitali za rufaa, pamoja na Kanda kama vile ya Ziwa ambayo kwa mujibu wa waziri wa Afya, jinsia na watoto, Ummy Mwalimu kwamba kanda hiyo ina watu wengi na inahitajika kuongezwa huduma za afya ambazo miaka ya nyuma ilikuwa changamoto kubwa.

Aidha, taarifa rasmi ya wizara ya Afya na Maendeleo ya Jinsia na Watoto nchini humo inaonesha kuwa jumla ya vituo vya afya 200 vimejengwa maeneo mbalimbali nchini chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano. Hatua hiyo inakusudia kusogeza huduma karibu huduma za afya kwa wananchi.

Mgogoro wa makinikia; serikali ya Tanzania iliingia kwenye mzozo na kampuni ya madini ya Acacia ambayo inamilikiwa na Barrick Gold kuhusiana na mchanga uliokuwa unasafirishwa kwenda kuchenjuliwa nje ya nchi ya nchi hiyo jambo ambalo halikubalika na mamlaka za nchini humo.

Majadiliano yaliyoongozwa na waziri wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi yaliwezesha kupatikana mwafaka ambapo pande zote zilionesha kuridhia makubaliano mapya ya kupata faida zaidi katika sekta ya madini. Uongozi wake unasifika kwa kulinda rasilimali za nchi.Zipi changamoto zilizoikabili serikali ya Magufuli?

Uhaba wa ajira; Kuondoa vyeti feki kumetengeneza wimbi kubwa la watu wasio na ajira. Papo hapo baadhi ya wenye vyeti stahiki na wahitimu wa vyuo vikuu kuanzia mwaka 2015 wamekuwa kwenye wakati ngumu kupata ajira serikalini pamoja na sekta binafsi kulazimika kupunguza wafanyakazi kutokana na hali mbaya ya uchumi na wataalamu wamebainisha imetokana na mzunguko wa fedha kuwa hafifu.

Vyanzo vya habari mbalimbali kwenye mamlaka za Tanzania zimemwambia mwandishi wa makala haya kuwa matumaini pekee ya kuzalisha ajira yamebaki kwa viwanda ambavyo ni sehemu ya sera kuu ya serikali ya awamu ya tano. Lakini bado matarajio hayajakidhi ikizingatiwa.

Usalama wa raia: Matukio yenye kuashiria uhaba wa usalama wa raia na viongozi yameibua wasiwasi miongoni mwa raia wa nchi hiyo, kushambuliwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na matukio mengine yaliyotekelezwa na watu wanaoitwa wasiojulikana ambapo hadi leo hakuna ripoti rasmi zilizowekwa mbele ya Umma.

Vilevile kutoweka baadhi ya watanzania katika mazingira yenye utata,kutekwa, kuibuka kwa dhana ya watu wasiojulikana kutenda maovu na mengine yanayofanana nayo yamekuwa changamoto kwa kipindi cha miaka mitano, hali ambayo inaibua wasiwasi miongoni mwa raia kuhusu usalama na mali zao.
Demokrasia; vyama vya upinzani vimekutana na wakati mgumu katika kipindi cha miaka mitano ambapo mikutano ya hadhara ya kitaifa ya kisiasa ilipigwa marufuku. Licha ya wanasiasa ambao ni wabunge kuruhusiwa kufanya mikutano katika majimbo yao ya uchaguzi, bado walikumbana na wakati mgumu kupata vibali kutoka Jeshi la Polisi ama wakipata kunyimwa fursa ya kufanya mikutano hiyo.

Aidha, baadhi ya wanasiasa kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kulipa faini hususani kutoka chama kikuu cha upinzani Chadema, wakiwemo Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko, pamoja na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Wakati wanasiasa wa chama tawala CCM wakiwa huru kufanya mikutano, kwa upande wa wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa. Hivyo basi, suala la demokrasia ni eneo ambalo limekuwa changamoto mno.

Hali kadhalika taasisi kadhaa za kiraia zimefungwa ama kunyimwa usajili mpya kutokana na sheria iliyopitishwa ya kudhibiti na kukagua mapato na matumizi yake au kwa sababu zingine kutokana na uamuzi wa mamlaka ya nchi hiyo.

Hivi karibuni mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Ole Ngurumwa alitangaza kufungwa shughuli za taasisi hiyo baada ya akaunti zake za benki kusimamishwa na mamlaka za Tanzania, huku Inspekta Jenerali Polisi, Simon Sirro akibainisha kuwa wanachunguza kiasi cha shilingi bilioni sita za taasisi hiyo ambacho hakijafahamika kitatumika kwa madhumuni gani. Hali hiyo inachangia sintofahamu na kuzifanya shughuli za asasi za kiraia kuwa katika wakati mgumu.

Uhusiano wa kidiplomasia; mwanzoni mwa mwaka huu wa 2020 serikali ya Marekani ilitoa orodha ya baadhi ya viongozi ambao hawaruhusiwi kuingia nchini humo, ambapo miongoni mwao alikuwepo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Kitendo cha kuwekewa vikwazo pamoja na mamlaka za Tanzania kulaumiwa kuvunja sheria za haki za binadamu ni ishara ya uhusiano mbaya baina ya mataifa hayo.

Aidha, matamshi hasi na shutuma yanayotolewa mara kwa mara kwenye majukwaa ya siasa dhidi ya mataifa ya magharibi ambayo ni wafadhili wakubwa wa miradi ya maendeleo pamoja na bajeti za serikali zinatajwa kujenga taswira hasi ya serikali hiyo hivyo kukabiliwa na changamoto kubwa ya kurejesha mahusiano mazuri ya kidiplomasia.

BBC swahili

_114243496_9fd37c71-bb5f-4d97-9407-c4dedbdf2e7f.jpg
_114243499_5db80cef-438d-4976-9cb5-ba879112478e.jpg
_114243501_8c2d12a1-9a9a-4d76-bd5a-92d2d2743389.jpg
_114243803_2f4e7091-ede4-48bd-90f5-ff81a3a49b79.jpg
 
Back
Top Bottom