Wasifu (CV) ya Dr. John Pombe Magufuli

Wasifu (CV) ya Dr. John Pombe Magufuli

Mkuu, naomba mwongozo; kuna wakati alitembelea mkoa wa Kagera na akaenda kwenye shule moja hivi akiwa na masista pamoja na mkewe na akaonesha hadi kitanda alicho kua analala na dirisha alilolibomoa na mkewe akamwambia alipe na akalipa pale pale, mbona siioni hiyo kwenye historia!? Well, niliipenda sauti na haiba ya mama Magufuli, she is so humble, anaongea kwa heshima, kwa vituo tena kwa utaratibu, long live mama Janeth Magufuli
Mkuu siku zote wanaume watata hupata wake waungwana sana and vise versa! Fanya ka utafiti kasiko rasmi utajiridhisha na hilo.
 
Ile

Ile alidanganya alivyoenda Kule. Si unajua mambo ya magumashi magumashi
Hamna bwana, yaani adanganye hadi kitanda na dirisha alilovunja!? Hiyo nakataa kabisa mkuu, mleta UZI kaisahau tu hiyo shule ya Katoke kuiweka humo
 
Ukiangalia CV ya Mkulu utagundua kuwa hakuwahi kufanya kazi uraiani kwa muda mrefu. Inaonekana ni kama amefanya kazi miaka 2 au 3 tu then akaukwaa Unaibu Waziri.

No wonder inaonekana kuwa na mapungufu kwenye social skills ..................!!
 
Nimekuuliza swali dogo tu unadhan Kilimo ni rahisi?
Kilimo kina ugumu gani kama sio uvivu tu wetu wa kupuuzia mambo...kilimo kimetukuza wengine mpaka tumesoma mpaka vyuo vikuu..tatizo lako liko wapi
 
Hahahahah kiboko ya mafisadi, hahaha...!!!!
Hapa sindano imekuingia nywiiiiii...ukitaka kujua hili muulize mzee mamvii..atakusimulia kilichomfanya awaambie wapinzani wenzake SHUT UP..!!! Hahahaha..
 
Hata urais pia inabidi vijana wagombee manake haihitaji experience
 
Kama ulikua humjui vizuri Rais John Magufuli ngoja nikufahamishe;-
- Jina lake halisi anaitwa John Pombe Joseph Magufuli,
- Amezaliwa tarehe 29/10/1959,
- Sehemu alizaliwa ni Chato Geita,
- Mke wake anaitwa Janeth,
- Anawatoto 3,
- Dini mkristo na dhehebu lake ni Mkatoliki,
- Kabila lake Msukuma,
- Mwaka 1967 alianza shule ya msingi iitwayo Chato primary iliopo mkoani Geita na kumaliza Mwaka 1974,
- Mwaka 1975 - 1978 alisoma shule ya sekondari iitwayo Lake Nyanza iliopo Mwanza,
- Mwaka 1979 hadi 1981 alisoma Mkwawa high school iliopo Iringa,
- Mwaka 1981 hadi 1982 alienda kusoma diploma ya ualimu katka chuo cha ualimu kiitwacho Mkwawa Education College na alikua anasoma Masomo mawili tu yaani Kemia na Hisabati,
- Mwaka 1982 alipo makiza tu kusoma aliajiliwa na kufundisha shule ya msingi Sengerema iliopo mkoani Mwanza na alikua anafundisha kemia na Hisabati Mpaka mwaka 1983,
- Mwaka 1983 - 1985 alienda kupata mafunzo ya JKT huko Dodoma katika Kambi ya Makutopola,
- Mwaka 1985 hadi 1988 alisomea degree ya kwanza ya elimu katka chuo kikuu cha dar es salaam na alikua anasoma masomo mawili tu yaani Kemia na Hisabati na kutunukiwa shahada ya kwanza,
- Mwaka 1989 hadi 1990 alikua mkemia mkuu wa chama cha ushirika cha Nyanza,
- Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea shahada ya pili yaani (Masters) ya kemia katika chuo kikuu dar es salaam na baadae akapata ufadhili na kwenda kumalizia Uingereza na kutunukiwa shahada ya pili yaani Masters ya kemia,
- Mwaka 1995 alijiingiza kwenye siasa na kugombea Ubunge katka jimbo Chato na kushinda,
- Alikua mbunge wa kawaida kwa miaka mitano yaani 1995 hadi 2000 ambapo baada ya hapo aliteuliwa na Mkapa kuingia kwenye baraza lake la mawaziri,
- Mwaka 2000 hadi 2005 aliteuliwa na mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi,
- Mwaka 2005 hadi 2008 aliteuliwa na kikwete kuwa waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi,
- Akiwa waziri wa ardhi mwaka 2006 alisoma shahada ya tatu ya kemia kwa njia ya masafa yaani distance learning na kumaliza Mwaka 2009 na kutunikiwa shahada ya tatu yaani Phd ya kemia,
-Mwaka 2008 hadi 2010 aliteuliwa kuwa waziri wa Mifugo na Uvuvi,
-Mwaka 2010 hadi 2015 aliteuliwakuwa waziri wa ujenzi,
-Mwaka 2015 alichukua fomu ya kugombea Urais na kufanikiwa kushinda kwa aslimia 58.46%.

Huyo ndio John Magufuli rais wa Tanzania kwa sasa.
Neno moja kwake....View attachment 780016
Huko koote alikuwaa antumia lugha ipi kujifunza kuongea najamii mpaka akafikia kukwama kujibu swali akasaidiwa na Mu7
Tu rimuvu fridomu ov woti
 
attachment.php

attachment.php


Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 1991 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.

Mwaka 1985 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1981 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.
Mwaka 1975 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.

Mafunzo
Machi 1984 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.

Januari 1984 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.

Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).

Mwaka 2005 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)

Mwaka 2000 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.

Mwaka 1982 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).

Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.

Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.
Hivi nikweli alikuja bongo akiwa ametokea nchi jirani?
Au huyu dogo anatuzingua
 
attachment.php

Mwaka 1991 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.
Kama huyu mtu alisoma Masters Uingereza na bado hawezi kuongea sentensi moja ya Kiingereza basi huyu akili yake imejaa matope siyo Ubongo....

Na hivi alisoma kweli chuo hicho au alitunukiwa cheti cha chuo hicho? Maana kwa mfano pale IFM kuna watu wanatoka na degree za Dublin Institute of Technology(DIT) cha Ireland, kama hujajua ukiona vyeti vyao unaweza kudhani kweli waliondoka TZ wakaenda kusoma huko, shida watakushangaza hawawezi kuongea sentensi hata moja ya English
 
Kama huyu mtu alisoma Masters Uingereza na bado hawezi kuongea sentensi moja ya Kiingereza basi huyu akili yake imejaa matope siyo Ubongo....

Na hivi alisoma kweli chuo hicho au alitunukiwa cheti cha chuo hicho? Maana kwa mfano pale IFM kuna watu wanatoka na degree za Dublin Institute of Technology(DIT) cha Ireland, kama hujajua ukiona vyeti vyao unaweza kudhani kweli waliondoka TZ wakaenda kusoma huko, shida watakushangaza hawawezi kuongea sentensi hata moja ya English
Anaongea ila anachanganya na kihutu
 
Ukiangalia CV ya Mkulu utagundua kuwa hakuwahi kufanya kazi uraiani kwa muda mrefu. Inaonekana ni kama amefanya kazi miaka 2 au 3 tu then akaukwaa Unaibu Waziri.

No wonder inaonekana kuwa na mapungufu kwenye social skills ..................!!
Graph ya ukuaji wake inaonesha is like alikuaga shushushu so ni kama alikua anatumwa kwenye special missions, akimaliza tu anahamishwa; that is my mtazamo regarding his growth carrier, I stand to be corrected!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom