Wasichana waliozaa wakiwa mashuleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasichana waliozaa wakiwa mashuleni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mfamaji, Jul 28, 2009.

 1. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Katika gazeti la leo la Uhuru, maoni ya editor , wanazungumzia eti kwamba wasichana waliozaa wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo kwa sababu hawawezi kufanya vyote, yaani kulea watoto wenzao na kitabu.

  Wakuu huku ni kufikiri kwa njia gani? Na hili ndio gazeti la seriakali ya Tanzania.
  Huyu jamaa anajua lolote kuhusu constitutional right za Mtz? kwamba elimu ni haki ya msingi regardless? F****c///k.

  Nashindwa cha kusema ila angekuwa karibu nami ningemtemea za usoni. Potelea mbali .Nyie wenzangu vipi.Mwaliojane hilo?
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mazee kwa sababu wengine hatujasoma hilo gazeti ungefanya la maana kutujuza points za yeye kusema hayo aliyoyasema, ili tujue mantiki ya tunachokijadili.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa mtoa mada PUNGUZA MAKALI YA LUGHA, kwani kwa bin'Adam tunasema wasichana wanaopata ujauzito mashuleni.

  Huku ni kuwanyima haki hawa watoto wanaopata ujauzito shuleni.Nashauri serikali ya Tanzania kuliangalia hili ili kuwapa nafasi hao waliofanya makosa ya kupata ujauzito kwani pamoka kuwa ni haki yao kupata elimu lakini pia nataraji hawatafanya makosa tena
   
 4. m

  mchakato Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  sio gazet la serikali, ni la chama cha mafisadi (CCM)
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Poa mkuu. Samahani kwa hilo . Jazba shauri ya upuuzi wa baadhi ya wenzetu wa Kibongo.
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Vyo vyote vile . Serikali ni ya CCM na gazeti ni la CCM , na mafisadi na wa CCM . Can't separate em?
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Naomba usinitemee mate kwa haya nitakayosema (joke!).

  Binafsi siwezi kumlaumu sana. Kwa ujumla kama taifa bado hatujawa na njia bora inayokubalika ya kushughulikia matatizo ya ujauzito kwa watoto ambao bado wapo shuleni.

  Kumbuka bado tuna mkanganyiko mkubwa tu juu ya mtoto ni nani kisheria. Sheria mbalimbali zinatoa tafsiri tofauti na baadhi zinakinzana juu ya umri hasa wa mtoto. Angalia kama sheria ya ubakaji (mtoto ni chini ya miaka 18, lakini sheria ya ndoa binti wa miaka 15 anaweza kufunga ndoa.

  Kusema kwamba mtoto akipata ujauzito aendelee na shule pengine ni vema na haki. Lakini wengine wanaangalia pia athari zake kimaadili kwa taifa. Kama mwanafunzi akipata ujauzito anaweza kuendelea na shule, tunaweka utaratibu gani wa kuwafanya watoto wengine waepuke kupata ujauzito?

  Leo hii mtoto wangu wa kike nikiona mwenendo wake si mzuri, nitamwambia moja kati ya athari za kuzini ni kupata ujauzito asioutarajia na kwa hakika utamuaribia maisha kwani atashindwa kuendelea na masomo. Sasa kama akipata ujauzito bado anaweza kuendelea (na anaona 50% ya wenzie wana ujauzito na wanapiga kitabu kama kawaida!) na shule binti huyu nikimwambia asizini bado atanisikiliza?

  Pamoja na kusema hayo nadhani ni lazima kuwe na utaratibu ambao utawadiscourage watoto/wanafunzi kuzini lakini wakati huo huo kuwepo na namna mbadala ya kuwapatia elimu watoto wanaopata ujauzito.
   
 8. W

  WONDERWOMAN Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  swadakta SMU
  Ni lazima tutafute utaratibu wa kuzui mimba za utotoni (Mashuleni),watoto waone kuwa kuzini ni jambo baya na lenye madhara mengi na wao wenyewe waelewe mazingira gani ni hatarishi na kwa kushirikiana na walezi na walimu waepuke/waepushwe na mazingira hayo.
  Na pia inapobidi bint arudi shuleni baada ya kujifungua (kwa maana juhudi za hapo juu zimefeli) nionavyo mimi ni bora watengewe darasa lao na humo wawe wanapewa nasaha na kupata elimu kama wenzao ili wajirekebishe na wasiwaambukize wenzao tabia hatarishi kama wanazo .
  Hatari ya kutowasomesha hawa ni kuzidisha tatizo la ujinga na umasikini na watoto wa mitaani pia.
  IT IS COMMON EXPERIENCE THAT PEOPLE PERISH BY THE VERY MEANS BY WHICH THEY SEEK TO DESTROY OTHERS
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kwa mantiki hiyo, ambayo bado iko too low. Kila mtu anafikiria hivyo na ndio line of thinking ya Editor wa Uhuru.

  Sasa fikiria katika mkoa mmoja wa Kagera watoto 600 wa kike wameshindwa kuendelea na masomo sababu ya ujauzito .Hii ni sample tu . Sasa angalia kitaifa uone ni wangapi wanaoathirika kwa tatizo hili. Sijui ni njia zipi tunazoweza kutumia kuzuia ngono kwa watoto.Je mmojawapo ni hiyo ya kutowaendeleza tena baada ya kujifungua?

  Naona hata HVI pamoja na kueleweka kwa kiasi kikubwa bado haijaweza kuwa dis insentive . Someone has to think deeper. Kwa maana nyingine tatizo litaendelea na sisi tutaendelea kuwa conservatives na kunyanyapaa badala ya kusaidia pale palipokwisha haribika. Vipi sheria zinasemaje kuhusu wanaume waliowapa mimba wanafunzi. Je zinaweza kuwareinfocred zaidi badala ya kuwaadhibu hao watoto kihivyo?

  Someoe has also to consider environments which facilitate this issues. Hujawa na mtoto akaenda kusoma Uganda au Kenya akaja na mimba .May be ungefirikia vinginevyo na for sure usingepanda awe house girl au bar maide in future. Ni wewe , sembuse kijijini ?

  Mind you .I am niether happy nor am I supporting this habit. Ni kama ule msemo --Je mtoto akijinyea mkono utamkata? Tubadilike.
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu hapo ndipo kwenye tatizo kubwa. Kwa sababu waharibifu wa watoto hawa hawachukuliwi hatua za kueleweka ndio maana watu hawaogopi kufanya ngono na watoto. Na mbaya zaidi, wakati mwingine hata walimu wanahusika.

  Ukijaribu kufuatilia kati ya hao 600 waliopewa ujauzito unaweza kuta hakuna hata muhusika (mwanaume) ambaye amefungwa kwa ubakaji kama sheria zinavyotaka.

  Kwa sehemu kubwa hata jamii yenyewe inachangia kwa kiasi kikubwa kuwaficha/kuwalinda waharibifu. Hivyo pengine hili ni tatizo la kijamii na pia kisheria.

  Ni lazima tujenge jamii ambayo inatambua kwamba ni 'mwiko' kufanya ngono katika umri mdogo na pia ni mwiko kufanya ngono na mtoto. Nilisoma kile kisa cha Babu Seya, kilinisikitisha sana, lakini kilinifungua macho pia kuhusu malezi ya watoto wetu hasa wa kike.
   
Loading...