Katika pitapita zangu nimekuja kuona hawa wa Ibisinia hawanaga ile kitu kufunga ndoa au mahusiano na watu wasio wabisinia (wahabeshi) hata huko kunako mataifa ya nje vinginevyo kwa sababu hana jinsi anatafuta njia ya kupita. haina maana kukusitishia penzi lako kwao, ila tu kwa utamaduni na mapokeo ya kikwao kama walivyosema wengi hapo juu wanajali zaidi asili na damu yao kwa walio wengi. Kwa urafiki wa kawaida tu ni watu wazuri sana na wanajisikia wa kutoka Afrika Mashariki, lakini hapa kwenye mahusiano si vipaya ukachukua tahadhari kama unakusudia awe mwenzi wa maisha isije ikawa anatafuta nafasi tu ya kusetirika.