Wosia wa tajiri Bilionea Bill Gates

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Leo nilikuwa nafatilia moja ya kituo cha television huko marekani tajiri nambari moja duniani Bilionea Bill Gates aliulizwa na mwandishi mmoja wa habari kuwa anajisikiaje kuwa tajiri mkubwa zaidi duniani. Akajibu kuwa hadhani kama yeye ni tajiri namba moja. Akaulizwa anadhani kuna mtu anamzidi? Akajibu "Nadhani yupo mmoja" Akaulizwa ni nani?

Akasema "Nilipokuwa shuleni sikuwa na fedha. Kuna wakati nilienda kwenye "vijiwe" vya kuuza magazeti ili nisome tu japo vichwa vya habari. Kijana mmoja mweusi (black American) ambaye alikua ombaomba eneo lile aliniona Alijua nilihitaji gazeti lakini sikuwa na uwezo wa kununua. Akatoa kiasi cha pesa katika zile alizokuwa akiombaomba akaninunulia gazeti. Nilijaribu kukataa kwa sababu nilijua anaweza kulala njaa kwa sababu yangu, lakini alinisihi nichukue...

...Siku nyingine tena nilienda kijiwe kile na sikuwa na fedha. Sikutaka mtu yule anione. Hivyo nikapitia vichwa vya habari kimyakimya, na wakati naondoka nikaletewa gazeti, nimelipiwa na yule ombaomba. Akanitizama, akafurahi. Nikamtazama. Nikalia. Nikaondoka"

Mwandishi akamuuliza sasa huyo awezaye kuwa tajiri kuliko wewe wakati umesema ni ombaomba? Bill Gates akasema "mtu yule alitoa hata kile kidogo alichokuwa nacho ili kunisaidia. Hakujali kuwa anaweza kulala njaa, kukosa malazi, kukosa mavazi, hakujali kupoteza akiba yake yote ndogo aliyokuwa nayo ili kunisaidia. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi."

Mwandishi akamuuliza, kwanini usimtafute umlipe? Bill akajibu. Nimeshamtafuta, nimemnunulia nyumba, na kumpa dola milioni moja (kama bilioni mbili za kibongo), lakini sijaweza kulipa hata robo ya alichonipa. Mwandishi akamuuliza kwanini? Bill akajibu "kwa sababu mimi nimetoa sehemu ndogo katika kikubwa nilichonacho, lakini yeye alitoa sehemu yote katika kidogo alichokuwa nacho. Nadhani mtu yule ni tajiri kuliko mimi"

Umejifunza nini?me nimejifunza wema wa mtu haulipwi.
 
Angalia akili za wabongo wakichangia mada fikirishi kama hii.....#11,12,13...
Tibaijuka na Ngereja endeleeni kutugawia hicho kidogo maana akili zetu ndio kama hizi za mfano wa wachangiaji hapa!
 
Bado siamini kama kweli biligate kanena matamshi hayo, wabongo nawajua vizuri katika kutengeneza tukio
Bado siamini hadi kwenye trusted source
Wewe unaangalia ukweli wa matamshi au ujumbe uliomo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom