MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,114
- 3,769
Bunge la Congress la Marekani limepitisha msaada wa Dollar Bilioni 40 Sawa na Tsh Trillion 97 kwa ajili ya msaada wa kijeshi Kwa Ukraine. Msaada huu unakuja ikiwa Ni Ombi la Rais wa Marekani Joe Biden kulitaka Bunge Hilo kuidhinisha kiasi Cha $ 33B kwa ajili ya msaada wa kijeshi ya kiutu Chini Ukraine wiki iliyopita.
Akiongea na Kiongozi wa walio wengi kwenye Bunge la Congress la Marekani, Nancy Pelosy Jana Usiku, Rais wa Ukraine alilitaka Bunge la Congress kupitisha msaada huo ili Wanajeshi wa Ukraine waanze kuyakomboa maeneo yaliyotekwa na Urusi ikiwemo kuwafurusha Wanajeshi wa Urusi Mariopul ambao wamewazunguka wapiganaji wa Ukraine kwenye Kiwanda Cha Chuma.
Akiongea na Vyombo vya habari hi Leo,Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lyod Austin,amesema kuwa Msaada huo utajumlisha Silaha za masafa Marefu zenye Uwezo wa Kushambulia Kilometa 200.
Wataalamu wa Mambo wanasema, Kuna uwezekano wa Marekani kupeleka Arterarry Aina ya HIMIRS ambazo zinauwezo wa Kupiga Crimea. Daraja la Crimea Ni nyendo mhimu kwa Russia kwani linaunganisha Crimea na Urusi. Endapo Marekani itapeleka hata Mfumo mmoja wa HIMIRS,Basi Daraja la Crimea litakuwa mashakani.
Ikumbukwe kuwa, Kwa zaidi ya miezi 2 Sasa, Wanajeshi zaidi ya 500 wa Ukraine walikuwa Nchini Poland na Romania wakipatiwa Mafunzo ya jinsi ya Kutumia Silaha za Marekani.
Katika Ripoti ya Leo,Jeshi la Ukraine limevikomboa vijiji 7 katika mji uliotekwa na Urusi wa Kherson tangu mwezi Machi. Pia Jeshi la Ukraine limedai kuwarudisha nyuma Wanajeshi wa Urusi kwenye mji wa Kharkiv.
The package would give Ukraine more military and economic aid, with $5bn to go towards the global food shortage. US House approves $40bn aid package for Ukraine