Washili Chadema Imeshawashtukia

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa wabunge jimbo la Arumeru Mashariki baada ya kutokea kifo cha muheshimiwa Sumari, lilijitokeza dosari moja kutoka kwa wanaojiita wazee wakimila wanaojulikana kama Washili kua hawatakubaliana na musheshimiwa Godbless Lema kufanya kampeni kwa mgombea wa Chadema kwakua alitoa maneno ya kashfa kwenye mazishi ya muheshimiwa Sumari ambayo kwao Washili hao wameona kitendo hicho kimewazalilisha.

Basi habari zinazoendelea hapa maeneo ya Usa River na vitongoji vilivyojirani na jimbo hili la Arumeru Mashariki ni kua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepata habari kua vizee hivyo vinavyojiita Washili ni usanii fulani kukwamisha juhudi za chama cha chadema kukosa nguvu kumbe vizee hivi vinatumia kinga hii ya kikwako kwakujiita wazee wa jadi huku wakipeleka nguvu kwa watoto wao wanaogombea kinyanganyiro hiki cha ubunge Arumeru Mashariki.

Mtakumbuka pia vizee hivi ndivyo vilivyotoa kauli na kuweka matangazo mji mzima wa Arusha kua watavunja chungu kwa wale woote waliohusika na sakata lile lililopelekea kwa kijana wao ambae ni mfanyabiashara maarufu aliyetumikia kifungo cha miaka mitano jela kwakile walichosema alihusika na mauaji yakutumia silaha na kupora madini ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia. Washili hawa walitaka waliohusika wajitokeze ili waombe msamaha ama sivyo watavunja chungu, lakini tukio hili likaishia hewani.

Chadema imeshashtukia njama hizi zinazoendelea kupitia kwa vizee hivi vinavyojiita Washili ili kukwamisha juhudi za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo lakini shime Chadema tusonge mbele! ALUTA CONTINUE!
 
jibu tuhuma za kwa nini lema alifanya uhuni na kusababisha fujo msibani

Natumaini kwenye msiba ule viongozi wote wakitaifa walikuwepo akiwapo raisi wako pamoja na mkuu wa polisi Arusha kulinda usalama, kama alifanya fujo usalama wa taifa ulikua wapi? Usidandie Treni kwa mbele!
 
Nina mashaka na aloandika hii thread, imekaa kichonganishi chonganishi....lugha alotumia 'vizee' haina staha. Kwahiyo basi hata mimi CHADEMA kindakindaki nakana kuthubutu km huyu ni mwenzetu! CCM wana mitego, sisi tuna mbinu!
 
Lugha niliyotumia ni lugha Adhimu kabisa ya kiswahili mkuu na imeeleweka!
 
jibu tuhuma za kwa nini lema alifanya uhuni na kusababisha fujo msibani

Mkuu Inakuuma,

Unajua kwamba Lema ni aina ya kiongozi mwenye mvuto has kwa vijana.Siku ya mazishi ya Mheshimiwa Sumari Vijana walishindwa kuzuia hisia zao na kwenda kumzonga.Hili kimsingi sio kosa lake,si rahisi yeye angewafukuza kwamba nendeni kule.Laiti kama hao washili wangethibitisha maneno ambayo LEMA aliyasema ya kuwakashifu hapo sawa tungejadili hii issue.Wameishia kusema kwamba lema aliwaudhi kwa kukusanya kundi la vijana.

Laiti ungejua jinsi LEMA anavyopendwa Arusha ungeelewa ninachosema.Lema anapendwa,Ana ushawishi mkubwa ndio maana hawa wazee wanaitwa washili ambao mwenyekiti wao ni Hezron Sumari wa ukoo wa Sioi Sumari lazima wamwogope kwamba atabadilisha akili za watu wengi.Kina Hezron na washili wenzake wanapigania mtoto wao Sioi apite.
 
Huwezi lkukwepa mchezo mchafu katika nchi ambayo viongozi wake wanapenda kuendelea kuwa madarakani come what may!!!
 
jibu tuhuma za kwa nini lema alifanya uhuni na kusababisha fujo msibani

Kwa baadhi yetu mtafuta haki na mwenye msimamo ni muhuni mbele ya dhulumati na mchumia tumbo kama wewe. Basi afadhali uitwe muhuni kuliko kuwa dhulumati na lege lege kama serikali ya CCM chini ya MJK
 
Lugha niliyotumia ni lugha Adhimu kabisa ya kiswahili mkuu na imeeleweka!

mkuu unaweza kutupotezea wanachama, 'adhimu' ya lugha iko wapi hapo. CDM hatutukani ovyo wala kutoa kashfa. Mfano ungeandika 'wazee waumbuka'...hebu twende jukwaa la elimu nikufunde staha ya lugha!
 
Na inakuaje Washili haohao wakubali viongozi wengine wa Chadema watawakubali waende kumkampenia mshiriki wa Chadema lakini si Lema hapa ndipo napopata shida kujua ni nini kinawasumbua kuhusiana na muheshimiwa Lema.
 
Mkuu Inakuuma,

Unajua kwamba Lema ni aina ya kiongozi mwenye mvuto has kwa vijana.Siku ya mazishi ya Mheshimiwa Sumari Vijana walishindwa kuzuia hisia zao na kwenda kumzonga.Hili kimsingi sio kosa lake,si rahisi yeye angewafukuza kwamba nendeni kule.Laiti kama hao washili wangethibitisha maneno ambayo LEMA aliyasema ya kuwakashifu hapo sawa tungejadili hii issue.Wameishia kusema kwamba lema aliwaudhi kwa kukusanya kundi la vijana.

Laiti ungejua jinsi LEMA anavyopendwa Arusha ungeelewa ninachosema.Lema anapendwa,Ana ushawishi mkubwa ndio maana hawa wazee wanaitwa washili ambao mwenyekiti wao ni Hezron Sumari wa ukoo wa Sioi Sumari lazima wamwogope kwamba atabadilisha akili za watu wengi.Kina Hezron na washili wenzake wanapigania mtoto wao Sioi apite.

na watu wa arumeru mash. wakimpigia kura huyu kijana watakuwa na upungufu wa akili!
haiwezekani kuongozwa na familia moja kama hakuna wengine wenye uwezo!!
 
Hiyo ni kama inaonekana kulipana fadhila! Kisa nimeoa kwao au kaolewa kwetu huo ni kama utawala wa kidikteta.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom