illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Kipindi changu cha ujana sikukitumia vizuri hivyo ngoja niutumie uzee huu kwani tunaishi mara moja tu....nikitoka kutafuta ridhiki huwa napita pita kwenye vimiziki kidogo kuangalia mambo yanayotokea usiku duniani basi mara nyingi huwa najisahau kwamba "tamko" lilipita kuwa kukaa sehemu za starehe mwisho saa tano isipokuwa kwenye club za usiku basi nimeshajikuta kwenye mikono ya washika doria mara kwa mara ambapo huwa natoa ushirikiano wa kutosha ila nilichogundua ni kwamba hawa washika doria huwa hawako macho makavu, huhitaji alcoblow kujua kama mtu yuko bwax utamgundua mdomo mzito kutamka maneno kutembea anayumba pengine hata kuanguka (ni hatari kwani huwa wana silaha)matusi makelele ......siku moja tegeta sehemu fulani wanachoma nyama ya bata walipaki kisha wakaja wakaanza kuagiza huku zile za kuulia watu wameziweka mezani tuliondoka mmoja mmoja na bar ikafungwa bila wao kujua tukawaacha peke yao kwani tulijua kitakachofuata hapo ni kuwasaidia doria basi mi ngoja niishie hapo.