Uchaguzi 2020 Washauri wa Lissu mitandaoni wana tatizo kubwa la kiufahamu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Tangu TUNDU LISSU achaguliwe na chama chake cha CHADEMA kuwania urais wa Jamhuri ya Tanganyika wamejitokeza waswahel washauri wanaomfuatilia kwa karibu mno na kujaribu kushauri kindezi kabisa ama kukosoa kila anachoongea Lissu

Kundi hili ndio lile lililokuwa likijiapiza kuwa Lissu kamwe hawezi kurudi nchini na akithubutu kufanya hivyo ni moja kwa moja selo...hizi tabiri na haya maapizi vyote vimedunda... Lissu is at large..health n sound...!!! Fully energetic...!!!

Zikafuatia shauri na tabiri kuwa hawezi kamwe kuchaguliwa na chama chake kupeperusha bendera ya CDM kwenye kinyanga'anyiro cha urais..fitina, uzushi na mazingaombwe vilikuwa vingi mno...hatimaye kachaguliwa sasa wamebadili gia angani wamegeuka washauri

Chadema sio cha porojo na maneno mingi...wanajua kwanini wamemchagua Lissu. Ambaye ni mwanasheria nguli ngumu sana kumshinda...mpanga na mpangua hoja makini anayejua kwa hakika anachofanya.

Tunatumia nguvu nyingi kumshauri na kumkosoa mtu ambaye kwasasa ni international figure akiwa kafanya press conference nyingi za kimataifa na kuhudhuria interviews nyingi ambazo amezifanya kwa mafanikio makubwa.

Ndugu yangu wewe kachala uko ghetto na bundle ya msaada uliyefeli hata interview ya who are you unajaribu kumshauri mtu aliyekuzidi kila kitu?

Kuna wakati ni sahihi watu kuandika mitazamo na mawazo yao lakini isifike ukampangia mtu cha kusema ama cha kufanya...kila mmoja ana hulka yake...na hulka hazifanani hata kama nyie ni pacha.

Kwa nyakati tulizonazo kwenye hizi siasa za Tanganyika...hatuhitaji tena mtu linient..ni lazima awepo mmoja mahiri ambaye ni hardcore hasa....waswahel wanaita chuma cha pua.

Lissu ni hardcore na ni fearless...tanuri alilopitia limemuongezea ujasiri wa ajabu..amekuja kwa nyakati sahihi na muda anaotakiwa hasa....kwa siasa hizi za Lissu jina la NYUMBU LITAKOMA.

mungu janja janja ...mungu wa kabari na bisibisi mungu wa tofali la kisogo...nyakati sio rafiki tena...sasa ni bandika bandua hoja kwa hoja.....msiwe busy kushauri mpaka mkasahau kuoga.
 
Lumumba buku7 wanahaha maana hawaamini wanachokiona...kwanza ile nyomi ya airport tena kipindi cha msiba na mkwara wa polisi ndio imewavuruga kabisa
 
Mkuu politics is a serious business siyo kama wengi tunavyo ichukulia na ndiyo maana kuna watu wa ajabu sana wenye elimu ndogo wanashinda wakiwaacha mbali wasomi.

Siasani ni sehemu ya kusikiliza sana ushauri toka kila upande na kuchuja kisha unachukua ushauri mzuri badala ya kushupaza shingo na kuwakejeli wanao kushauri, au kupokea kila unacho shauriwa.

Kwa mfano angalia hii hoja yako hapo chini kisha ipime kwa umakini, kwa maoni yangu (IMHO) hakuna watu wa kimataifa watakao kuja kumpigia kura Lissu. Hao watu wa kimataifa watakuja kumsaidia kumtetea pale tu itakapo onekana kashinda uchaguzi lakini anadhulumiwa waziwazi.
Hata wao wana aibu hawawezi kumsaidia kuingilia kati pale ambapo atakuwa ameanguka vibaya sana kwenye maboksi ya kura kihalali.

Tunatumia nguvu nyingi kumshauri na kumkosoa mtu ambaye kwasasa ni international figure akiwa kafanya press conference nyingi za kimataifa na kuhudhuria interviews nyingi ambazo amezifanya kwa mafanikio makubwa.

Anyway si lazima ushauri upokelewe na huwezi kuzuia watu wasishauri ukizingatia wewe kaulimbiu yako na hoja yako kuu ni demokrasia na uhuru wa maoni.
 
Back
Top Bottom