Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,492
- 4,770
WASHAIRI TUSILALE.
Sanaa ya ushairi ni sanaa ya kale sana na pia ni sanaa inayodumu kwa miaka mingi na pia ni sanaa inayoafanya marika yote bila ya kuleta athari kwa rika lingine na bado marika
yote yakafanya kazi kwa pamoja, ni sanaa yenye maadili na kuzingatia tamaduni za jamii.
Ni wakati sasa wa wasanii wa sanaa hii kuhamka na kufanya kazi ya ushairi kwa masilahi na kuelimisha jamii.
Mashairi ni mengi sana na kila siku yanaandikwa na swali la kujiuliza ni JE WASHAIRI WANAFAIDIKA VIPI KUPITIA KAZI ZAO ?
Unaweza kudhani labda ushairi wa zama hizi haupendwi lakini kiukweli sanaa hii inawapenzi wengi ila tatizo wasanii wenyewe hawajajitoa kupeleka kazi zao ktk jamii kama wafanyavyo wAnamuziki wa kizazi kipya.
Ni vyombo vichache sana vinavyotoa nafasi ya kuweka hadharani kazi za ushairi lakini vingi vimeipa kisogo sanaa hii na inakuwa ngumu kuiweka wazi kwa kuwa hata muhamko wa wasanii wenyewe kuwa mdogo.
Kwa kifupi, KUTUNGA TUMETUNGA SANA NA SASA NI WAKATI WAMABADILIKO,USHAIRI KWA FAIDA YA JAMII NA MSHAIRI.
Idd ninga
. .. . iddyallyninga@gmail.com

Last edited by a moderator: