Washabiki jiulizeni, ni kwanini wanataka 100%?

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,288
2,000
Kama kawaida yetu Watanzania tuna utamaduni wa kushabikia tu kila kitu na kwenda na upepo. Lakini kuna wakati mwingine ni lazima tujiulize ili kunusuru taifa. Sio kila lifanyikalo ni kwa manufaa ya taifa kuna mengi sana ambayo viongozi wanafanya kwa manufaa yao kuonesha wenyewe ni miungu.

Kwenye hili la kutaka kushinda kwa namna yeyote 100% ya watu wote wanaochaguliwa bila kujali matakwa ya wananchi ina nia gani kwa taifa. Kwa sasa Tanzania bunge linapitisha chochote watakacho serikali, wana uongozi wote mpaka wilayani kwa 100%. Sasa jiulizeni ni yapi mapya ambayo wanatafuta?

Kwa mtazamo wa haraka haraka wanatafuta wakati ambako hata wabunge wa chama tawala kunyamazishwa. Kamati zote za bunge na CAG kunyamazishwa kabisa.

Vilevile kutafuta njia kunyamazisha hata mitandao iliyopo lakini kuwe na ubadilishaji wa sheria bila watu kujua.

Sasa kabla ya kushabikia kila kitu jiulize: Baada ya Magu kuondoka, tumeshaona muda ulivyo mfupi. Je, tukipata mtu mbinafsi itakuwaje? Mjue hii miradi mikubwa haijafika hata nusu na Magu ataondoka bila kumaliza? Treni hadi Dodoma bado; sasa itafika lini Kigoma?

Mradi wa umeme bwawa ndiyo wanasafisha njia itachukuwa miaka mingapi kuwa umeme?

Vilevile kuna uwezekano kabisa nia ya Magu ni kuwa na Bunge la kumuongezea muda madarakani kwa kisingizio cha miradi kutokukamilika na kutokuwaamini viongozi wengine.

Na kwasababu kutakuwa hakuna upinzani atasema sasa nani atazungumza kukitokea rushwa? Hivyo nia ni kuweka bunge lisiloaminika kwa wananchi na kubaki na serikali kuu pekee kama muhula mmoja tu.

Kwenye huo muhula mmoja nao wakumwamini awe mtu mmoja tu ambaye ni Rais. Sasa hivi wanatafuta mbinu za kuzuia mitandao kama hii ili Watanzania wasijue lolote.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,775

Mkuu Kamundu, kwanza nikurekebishe, hakuna yoyote aliyetaka ushindi wa asilimia 100%, na hata ule ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, sio CCM ndio waliotaka, bali ni wananchi ndio waliowachagua katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo hata uchaguzi Mkuu wa October, CCM haijichagui bali inakuja kwetu sisi wananchi ndio tunaichagua kwa hiari yetu katika uchaguzi huru na wa haki kwa ule ule mtindo wa unachukua..., unaweka...waaah! bila kujalisha how, na matokeo ya mwisho yanakuwa determined na the end justifies the means.
P
 
RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
1,847
2,000
Ndugu yangu haukumbuki kauli ya Nkamia?Bunge la miaka saba?unafikiri wanafanya kwa bahati mbaya haya???kwa maelekezo ya kagame!!!
 
lolypop

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,093

Kivipi kama mchezaji atakuwa yeye peke ake? Na kivipi uite ushindi wakati timu haikuwa na mpinzanu yoyote.
 
Mheshimiwa mkapa analo jibu sahihi hapa, huenda ni mpango uliopangwa muda mrefu ulikuwa unasubiri tu wakati mpango utimie.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,775
2,000
Kivipi kama mchezaji atakuwa yeye peke ake? Na kivipi uite ushindi wakati timu haikuwa na mpinzanu yoyote.
Kila mchezo unakuwa na rules of the game, kama sheria inasema, no show au ukitia mpira kwapani, timu iliyobaki inapewa point mbili za ushindi wa mezani.
P
 
lolypop

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,093
2,000
Kila mchezo unakuwa na rules of the game, kama sheria inasema, no show au ukitia mpira kwapani, timu iliyobaki inapewa point mbili za ushindi wa mezani.
P
Mchezaji mmoja akivunja hizo rules, mchezo unaendelea ili iweje. Kama ushindi ulikuwa mtamu mbona wameshindwa kuwarudishia mihuri wenyeviti wa vijiji?
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,775
2,000
Mchezaji mmoja akivunja hizo rules, mchezo unaendelea ili iweje. Kama ushindi ulikuwa mtamu mbona wameshindwa kuwarudishia mihuri wenyeviti wa vijiji?
Kipenga cha mwisho kikishapulizwa, ndio mwishowa mchezo mshindi anatwaa kombe, the winner takes it all, the loser standing small, sasa kama mshindi atasherehekea ua laa, haijalishi.
P
 
omari londo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
1,805
2,000
Mkuu Kamundu, kwanza nikurekebishe, hakuna yoyote aliyetaka ushindi wa asilimia 100%, na hata ule ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, sio CCM ndio waliotaka, bali ni wananchi ndio waliowachagua katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo hata uchaguzi Mkuu wa October, CCM haijichagui bali inakuja kwetu sisi wananchi ndio tunaichagua kwa hiari yetu katika uchaguzi huru na wa haki kwa ule ule mtindo wa unachukua..., unaweka...waaah! bila kujalisha how, na matokeo ya mwisho yanakuwa determined na the end justifies the means.
P
Wewe jamaa sometimes ni zaidi ya kinyesi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhakiki

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
1,970
2,000
Mayalla ni wewe kweli au umedukuliwa? Ok ccm inapendwa sana kwa nini wanaiogopa tume huru ya uchaguzi badala yake wanang'ang'ania tume ya uchafuzi?
Mkuu Kamundu, kwanza nikurekebishe, hakuna yoyote aliyetaka ushindi wa asilimia 100%, na hata ule ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, sio CCM ndio waliotaka, bali ni wananchi ndio waliowachagua katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo hata uchaguzi Mkuu wa October, CCM haijichagui bali inakuja kwetu sisi wananchi ndio tunaichagua kwa hiari yetu katika uchaguzi huru na wa haki kwa ule ule mtindo wa unachukua..., unaweka...waaah! bila kujalisha how, na matokeo ya mwisho yanakuwa determined na the end justifies the means.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
9,819
2,000
Kama kawaida yetu Watanzania tuna utamaduni wa kushabikia tu kila kitu na kwenda na upepo. Lakini kuna wakati mwingine ni lazima tujiulize ili kunusuru taifa. Sio kila lifanyikalo ni kwa manufaa ya taifa kuna mengi sana ambayo viongozi wanafanya kwa manufaa yao kuonesha wenyewe ni miungu.

Kwenye hili la kutaka kushinda kwa namna yeyote 100% ya watu wote wanaochaguliwa bila kujali matakwa ya wananchi ina nia gani kwa taifa. Kwa sasa Tanzania bunge linapitisha chochote watakacho serikali, wana uongozi wote mpaka wilayani kwa 100%. Sasa jiulizeni ni yapi mapya ambayo wanatafuta?

Kwa mtazamo wa haraka haraka wanatafuta wakati ambako hata wabunge wa chama tawala kunyamazishwa. Kamati zote za bunge na CAG kunyamazishwa kabisa.

Vilevile kutafuta njia kunyamazisha hata mitandao iliyopo lakini kuwe na ubadilishaji wa sheria bila watu kujua.

Sasa kabla ya kushabikia kila kitu jiulize: Baada ya Magu kuondoka, tumeshaona muda ulivyo mfupi. Je, tukipata mtu mbinafsi itakuwaje? Mjue hii miradi mikubwa haijafika hata nusu na Magu ataondoka bila kumaliza? Treni hadi Dodoma bado; sasa itafika lini Kigoma?

Mradi wa umeme bwawa ndiyo wanasafisha njia itachukuwa miaka mingapi kuwa umeme?

Vilevile kuna uwezekano kabisa nia ya Magu ni kuwa na Bunge la kumuongezea muda madarakani kwa kisingizio cha miradi kutokukamilika na kutokuwaamini viongozi wengine.

Na kwasababu kutakuwa hakuna upinzani atasema sasa nani atazungumza kukitokea rushwa? Hivyo nia ni kuweka bunge lisiloaminika kwa wananchi na kubaki na serikali kuu pekee kama muhula mmoja tu.

Kwenye huo muhula mmoja nao wakumwamini awe mtu mmoja tu ambaye ni Rais. Sasa hivi wanatafuta mbinu za kuzuia mitandao kama hii ili Watanzania wasijue lolote.
Tokea nianze kusoma maandiko yako mbali mbali hapa JF, sijawahi kukusoma kama nilivyokusoma leo.

Najua unanikumbuka sana katika kupinga mengi ya yale ambayo wewe huyaweka humu, kwa sababu huwa sikubaliani nayo kabisa.

Leo imekuwa ni tofauti kabisa, na ajabu ni kwamba hata mimi nilikuwa na mawazo ya kuleta mada kama hii, na nadhani bado nitaileta kwa njia nyingine, kwa sababu ya umhimu wake.

Ngoja niachie hapa kwa sasa.

Naunga mkono kwa nguvu zote hoja alizoweka mleta mada.

Ni wakati mwafaka sana waTanzania wasipumbae. Kumpa Rais Magufuli ushindi wa asili mia 90 kutailetea manufaa gani Tanzania?

Kwa nini anataka ushindi wa namna hiyo, ni kipi alichoshindwa kukifanya wakati huu kinachosubiri akifanye akiwa na ushindi huo wa asilimia kubwa?

Si tumeona juhudi zinazofanywa kuwanunua wabunge toka upinzani, ni kipi kilicholeta manufaa kwa kufanya hivyo?

Jiulizeni waTanzania, kuna manufaa yapi kwenu kwa Magufuli kushinda kwa asili kubwa hivyo?

Wakati mkijiuliza, fikirini, mtapoteza au mtafaidika kwa kuwaweka wapinzani wengi bungeni? Hili ni swali mtakalotakiwa kulijibu kwa kura zenu, na kukataa njia zote za kuwanyima haki yenu ya kuwachagua viongozi mnaowataka nyinyi wenyewe, bila ya kumsubiri Magufuli awawekee viongozi ambao hamkuwachagua.

Mnazo akili za kutosha kujua mazuri na mabaya kwa nchi yenu. Msiache mtu mmoja ndie awe mwamuzi wa kila kitu.
 
IPECACUANHA

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
3,152
2,000
Kama kawaida yetu Watanzania tuna utamaduni wa kushabikia tu kila kitu na kwenda na upepo. Lakini kuna wakati mwingine ni lazima tujiulize ili kunusuru taifa. Sio kila lifanyikalo ni kwa manufaa ya taifa kuna mengi sana ambayo viongozi wanafanya kwa manufaa yao kuonesha wenyewe ni miungu.

Kwenye hili la kutaka kushinda kwa namna yeyote 100% ya watu wote wanaochaguliwa bila kujali matakwa ya wananchi ina nia gani kwa taifa. Kwa sasa Tanzania bunge linapitisha chochote watakacho serikali, wana uongozi wote mpaka wilayani kwa 100%. Sasa jiulizeni ni yapi mapya ambayo wanatafuta?

Kwa mtazamo wa haraka haraka wanatafuta wakati ambako hata wabunge wa chama tawala kunyamazishwa. Kamati zote za bunge na CAG kunyamazishwa kabisa.

Vilevile kutafuta njia kunyamazisha hata mitandao iliyopo lakini kuwe na ubadilishaji wa sheria bila watu kujua.

Sasa kabla ya kushabikia kila kitu jiulize: Baada ya Magu kuondoka, tumeshaona muda ulivyo mfupi. Je, tukipata mtu mbinafsi itakuwaje? Mjue hii miradi mikubwa haijafika hata nusu na Magu ataondoka bila kumaliza? Treni hadi Dodoma bado; sasa itafika lini Kigoma?

Mradi wa umeme bwawa ndiyo wanasafisha njia itachukuwa miaka mingapi kuwa umeme?

Vilevile kuna uwezekano kabisa nia ya Magu ni kuwa na Bunge la kumuongezea muda madarakani kwa kisingizio cha miradi kutokukamilika na kutokuwaamini viongozi wengine.

Na kwasababu kutakuwa hakuna upinzani atasema sasa nani atazungumza kukitokea rushwa? Hivyo nia ni kuweka bunge lisiloaminika kwa wananchi na kubaki na serikali kuu pekee kama muhula mmoja tu.

Kwenye huo muhula mmoja nao wakumwamini awe mtu mmoja tu ambaye ni Rais. Sasa hivi wanatafuta mbinu za kuzuia mitandao kama hii ili Watanzania wasijue lolote.
Ukishazoea vya kunyonga kuchinja kwa ibada ni kupoteza muda.
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,288
2,000
Mkuu Kamundu, kwanza nikurekebishe, hakuna yoyote aliyetaka ushindi wa asilimia 100%, na hata ule ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, sio CCM ndio waliotaka, bali ni wananchi ndio waliowachagua katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo hata uchaguzi Mkuu wa October, CCM haijichagui bali inakuja kwetu sisi wananchi ndio tunaichagua kwa hiari yetu katika uchaguzi huru na wa haki kwa ule ule mtindo wa unachukua..., unaweka...waaah! bila kujalisha how, na matokeo ya mwisho yanakuwa determined na the end justifies the means.
P

P,
Juzi tu nimesikia makamu mwenyekiti wa CCM akiongea na wafanyakazi wa serikali na kuagiza wahakikishe wanashinda kwa 100% maana nia ni kufuta upinzani Tanzania. Pili uchaguzi wa serikali za mitaa haukuwa halali nasikitishwa wakati mwingine kwa ushushwaji wa kufikiri Watanzania wengi hawana upeo hadi balozi na jumuia za haki za binadamu zimeona hili. Tatu unavyosema kufiata sheria ki baya ni kwamba kama tunafiata sheria kweli viongozi wa kichama kama katibu mwenezi, katibu mkuu na makamu wa chama cha mapinduzi wasingekuwa ha haki ya kwenda na kutoa maagizo kwa wafanyakazi wa serikali wasio wa kisiasa. Pamoja na kuteuliwa na raisi haina maana viongozi wa utendaji wanatakiwa kisheria kuagizwa vitu kisiasa halafu unakuja kusema uchaguzi wa haki. Raisi wa nchi kuwaagiza wakurugenzi wasitangaze upinzani huwezi kusema uchaguzi ni wa wazi na ndiyo maana yametokea vile serikali za mitaa kwasababu ni maagizo ya kiongozi wa nchi!. Nashangaa kwa nini unakuwa na fantasy kwamba demokrasia ipo wakati hakuna ushahidi wowote wa hilo kuanzia 2016. Hivyo Magu anataka kuua upinzani Tanzania nia yake sio kushindana kwa sheria na kushinda.

Magufuli anataka kuwa Kagame hero wa Tanzania ambaye ndiyo baba lao na mwenye maanuzi yote kama mfalme. Na njia atakayotumia atasema anaomba miaka mitano tu! Na wote walianza hivyo hivyo. Kagame na Museveni nao walisema wataondoka miaka zaidi ya kumi sasa. Hii ndiyo sababu ya kutaka 100%. Kibaya ni kwamba hamjui vizuri huyu jamaa. Kama hamuamini mtaona. Tutaponea kwa njia chache (1) Kutokee watu ndani ya chama hasa wazee na kuona na kukataza hili lakini wanaonekana hawajali na ni wazee sana.Kikwete hamuogopi wengine wamezeeka na watakuwa wazee sana baada ya miaka mitano (2) Shinikizo la nchi za Dunia ya kwanza na hii ndiyo wanaoenda mbali wameongea na viongozi. Msiojua hata Raisi wa Kenya alizungumzia hili kwenye mkutano na Trump maana wanapata wasiwasi (3) Wananchi kuonekana hawaungi mkono (4) Afya ya Magu. Afya yake sio stable sana sana ingawa technologia imeongezeka ana moyo weak sana na juzi alivyosema alizimiaga ni kwasababu ya moyo. Lakini ana stents ambayo zinasaidia kurekebisha mapigo ya moyo. Hili tatizo analo toka akiwa na miaka 28. Hivyo sijui kama akiwa 65+ ataweza mikiki kiki ya uraisi. Lakini kwasababu ya technologia inawezekana.
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,856
2,000
Wengine watakao palilia Magufuli ang'ang'anie ni hao wanao pokea ratibu na kutekeleza utekaji na mauwaji, hawa watu watataka aendelee ili awahakikishie usalama wao.
 
Aug 12, 2019
88
125
Nakusalimu boss..

Kama ujipambanuavyo humu kwa mada zako za "kiuchunguzi" ,

sidhani kama haujawahi kuiona/kuziOna barua za makatibu wa wilaya(ccm) kwenda kwa makatibu wa kata(ccm) katika chaguzi ndogo zilizopita kuwataka wachukue nafasi hizo kwa 100% huku wakiwahakikishia kila kitu huko juu washakiratibu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom