Washa vifaa vya umeme kwa SMS ya simu

Washa vifaa vya umeme kwa SMS ya simu

Jaribu kujitangaza pia kupitia TV na redio,watu wengi watataka hii huduma
 
****DHUMUNI LA MFUMO****


1. Kuwasha/ kuzima vifaa vya umeme mf: taa, a/c, friji , feni, kwa kutumia SMS ya simu yako, uwe nje/ndani ya mkoa/nchi.


2. Kuweza kupata feedback SMS baada ya taa kuwaka/kuzima.


3. Kuweza kupata listi ya vifaa gani vimewaka/zima kwa kutumia SMS.


4. Kuweza kuseti mda gani taa iwake au izime yenyewe automatically kwa kutumia SMS.

mfano: unaseti 19:00 taa iwake saa moja usiku, 06:00 izime saa 12 asubui, kila siku


5. Mfumo huu hutumia SMS tu , hautumii INTERNET.


6. Simu aina YOYOTE inaweza kufanya control mf: Nokia ya Tochi, Smartphone, n.k


7. Mfumo huu hutumia line ya simu ya mtandao wowote ULE kukamilisha adhma zima.

ie: utachagua mtandao ambao una Excellent Signal Quality kwa eneo uliopo.


8. Mfumo huu ni wa njia 8 utachagua vifaa vipi viungwe katika mfumo.


mathalani: njia1 = friji , njia2 = A/C , njia3 = feni , njia4 = taa za nje , njia5 = taa za sitting room , n.k , vyote vikiwa HAVITEGEMEANI


9. Mfumo huu pia hukuwezesha kutumia swichi zako za ukutani kama kawaida pale utakapoishiwa na SMS katika simu. (2 WAY CONTROL TO ENHANCE FLEXIBILITY)


10. Mtumiaji ana uwezo wa kuseti Security Preferences , namba zipi ziruhusiwe kufanya control ili kuzuia 'Hacking'.





**PRODUCT/SERVICE PRICING**


> Kwa nyumba ya kawaida ( isiyozidi mita 35 x mita 35 ) ni Tshs. **800,000/-** ( Complete package + Installation + Android App )- NEGOTIABLE

> Kwa nyumba iliyozidi kipimo tajwa hapo juu , maongezi yatafanyika kupata package maalum.

> Kwa pricing iyo (800,000/-) unaunganishiwa njia zote 8 pamoja na kupewa App special (kwa watumiaji wa Android watakaopenda)

> Hii App ni kwa watumiaji wa Smartphone , kama huna Smartphone utatumia mfumo wa kawaida wa kutuma SMS.



NOTE: > Ikumbukwe mfumo huu hutumia SMS tu na si INTERNET.

> Aina yoyote ya simu itatumika sio lazima SMARTPHONE.

> Huduma ya kuwasha na kuzima kwa SMS ni pahala popote/umbali wowote ule.

> Garantii ya mfumo mzima ni MIAKA 2.






Kwa Mawasiliano zaidi tafadhali


0625 598 055 Call and SMS


0712 163 248 WhatsApp


Automation Engineer


Tunapatikana Dar Es Salaam , Makumbusho


KARIBUNI



View attachment 515099 View attachment 515099
Daah, kweli jf is the home of great thinkers.
Hongera sana brother ngoja tushee na wenye uhitaji kwa sasa mfanye kazi.
 
Ntashukuru sana, usinielewe vibaya lakini mimi hapa nilikuwa natoa angalizo - kama umesomeshwa bure ni Taifa hili una wajibu wa kuwasaidia Watanzania wenzako - pata faidi kiasi siyo ya kuvuka mipaka uzalendo una matter zaidi kuliko kitu chochote - je makampuni yamitandao wakisema hawataki mpitishe mawasiliano ya vifaa hivyo kwenye network zao mtakuwa wageni wa nani, je mtatumia VPN ili mitandao hisijuwe kinacho endelea nyuma ya pazia na kwa gharama gani kwa vifaa vyenyewe kujaribu ku-tinker around navyo - will it be worthy it? Je, mtanunua radio zenu za kusambaza mawasiliano kwa mfumo wa GSM/LTE/CDMA, je,TCRA inaweza kuwapa liseni kweli? Bottom line is: kazi yenu ni ndogo sana i.e mna install/configure lakini the Donkey job inakuwa facilitated/wezeshwa na makampuni ya simu Nchini consequently mnapaswa kuwa fair kwenye charges zenu. CHEERS.
Mkuu una Point Kiasi fulani hio price ya 800K ni kubwa mno hio Project ukiwa na Basic knowledge ya microcontroller na Programming haiwezi cost ata Laki moja kwa Hardware mfano izo Arduino au Gsm ni bei za kutupwa huko Ebay au aliexpress Jamaa aangalie kidogo umuhimu wa kuminimize cost walau 300K mana the whole project nafikikili ina cost kama 100K ivi
 
Acha wivu na roho mbaya bro! Post kubwa umeweka hapo juu..lakini hujatupa hizo details you claim. Learn to appreciate nguvu za wenzako. Hivi waTanzania tukoje jamani..kila siku kukatishana tamaa? Mpaka inakera! No wonder kila siku ulalamishi wa maisha magumu hauishi! Ni wa sababu ya watu kama nyinyi. Personally huu uzi umenibariki sana.

Mkuu keep up the good job. People like you are the true future of Tanzania and Africa. Usikatishwe tamaa na wenzetu waliozoea kulalamika bila solution za maisha.

Mda muafaka ukifika nitawatafuta. I suggest muanzishe hata website yenye information za kutosha kusudi iwe rahisi hata kwa wale wasioweza kuja hapo ofisini kupata huduma.

Wivu gani, are you normal? Muhusika mbona amenielewa - wewe kwa kuwa uelewa wako kuhusu nyanja hizi ni mdogo sana ndiyo maana unazungumza kinacho kujia kichwani - mimi kumshauri Mtanzania mwenzetu kwamba ajaribu kuwa realistic katika bei ya vifaa husika na ufungaji wake ili Watanzania wengi wafaidike/nufahike - wewe badala ya kutafakari ninacho maanisha unalipuka tu like unguided missile - kwa taarifa yako bei alisi ya vifaa hivyo tunazijua first hand lakini hatutaki kusema mengi - ndiyo maana tunatoa ushauri kwa mwenzetu afanye marekebisho - hatuna tatizo naye sisi.
 
Hii huduma ni lazima uwe eneo husika? Kama ndio jitahidini ifanye kazi mtu akiwa hata mbali na nyumbani aweze washa taa zake hususani pale anapochelewa kurudi nyumbani na anaishi peke yake
Tafuta kifaa kinaitwa sensor ufunge kwenye taa zako, zitajiwasha zenyewe giza linapoingia na kuzima kunapopambazuka.
hii huwasha na kuzima socket husika, socket ya friji, a/c kulenga hasa kupunguza bills za umeme pale unapotaka kuzizima remotely
mf: umeme umekatika na a/c ilikua on, umeme ukirudi na pia uko kazini , waweza tuma sms kuizima
friji, apa kuweza ku adjust on/off time ya friji pale unapotaka bana matumizi ya umeme , kwa kutumia sms,
ni kweli non-linear devices kama laptop, desktop zisihusishi maana zina couple of few steps katika uwashaji/uzimaji


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ww Engineer...hii kitu ni pamoja na wiring ya nyumba nzima kama mtu hajafanya wiring au vp?

Je mnapatikana wapi?

JPM KAMATA WEZI
 
Ww Engineer...hii kitu ni pamoja na wiring ya nyumba nzima kama mtu hajafanya wiring au vp?

Je mnapatikana wapi?

JPM KAMATA WEZI
kama unaitaji kuweka nyumba nzima, wiring tunakufanyia pamoja na kukufungia huo mfumo(njia 8) kwa bei tajwa juu apo (isiyozidi 35m x 35m), ila kama ushafanya wiring tunakufanyia 250,000/- (njia 2 + kukufungia +app)
 
Tunapatikana makumbusho karib na stend ya daladala
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom