Wasaudi si wa kuwaongoza Waislamu


Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Messages
9,944
Likes
7,536
Points
280
Age
31
Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2013
9,944 7,536 280
Sio chakula tu hata Mafuta ghafi ya diesel na petrol
 
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Messages
3,352
Likes
4,176
Points
280
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined May 14, 2017
3,352 4,176 280
Mwandishi anazungumzia umuhimu wa haki za wanawake na demokrasia! Tangu lini uislam ukapigia chapuo haki za wanawake au demokrasia kupigiwa chapuo tena kwa kampeni kwa namna hii? Ina maana mwandishi anataka huruma kutoka kwa wapigania haki za wanawake na demokrasia?
tapatalk_1513794795968-jpeg.949958
 
S

Shaka-Zulu

Member
Joined
Nov 20, 2018
Messages
50
Likes
75
Points
25
S

Shaka-Zulu

Member
Joined Nov 20, 2018
50 75 25
Yaani mashehe huwa mnanifurahisha sana yakiwabumia wa kwanza kumlaumu Ni USA hivi mnataka USA awe analiwasha chakula mdomoni?

Mbona marekani ndiye anayeongoza kuzalisha duniani? Jaribu kusoma usiwe unaamini kila unachoambiwa
Soma na tafakari wewe mwenyewe! Sio uandike irrelevant things. Marekani kuongoza kwenye uzalishaji chakula duniani inahusu nini na maada?!!! Ukweli ulio wazi ni kwamba Utawala wa Saudi Arabia umebaki kwa sababu ya Marekani. Silaha zote wananunua kutoka Marekani na washirika. Hata leo Trump anasita kuishutumu Saudia kwa mauaji ya Kashoggi akisema Saudia ni mshirika wake muhimu!!!
 
M

man kiney

Member
Joined
Nov 13, 2018
Messages
11
Likes
5
Points
5
M

man kiney

Member
Joined Nov 13, 2018
11 5 5
Mwandishi anaonekana ni Mshia au ameathiriwa na fikra za Kishia. Haoni baadhi ya nchi za kiarabu/kiislamu zilivyoparanganyika kwa kuwatoa watawala kwa nguvu? Mafunzo sahihi ya Uislamu ni kuwa watawala wanapokuwa waovu mnatakiwa mfanye subira juu ya uovu huo na mrejee kwa Allah ukweli wa kurejea, kinyume cha hivyo ndio tunaona leo fikra za kigaidi zinavyosumbua ulimwengu. Kila mtu leo ni shahidi jinsi gani ugaidi ulivyowaathiri watu duniani hasahasa Waislamu wenyewe. Mwisho naomba watu tuusome uislamu sahihi, na huwezi kupata kuujua isipokuwa kupitia kwa SALAF SWAALIH
Unajua kuna watu wanadhana kuwa ilan ni serikali ya kiisilamu wakati ni mashia sasa hili jambo litawatafuna sana tumuombe Allah atuongoze na atufanyie wepesi ktk kuendea dini hii hasa kwa kushikamana na manhaj salafy swaaleh
Watu wengi wanaipiga daawatsalafiyya kwasababu ya chuki na ujinga waliona na simu wanazosambaza wanaharakati kama
Hizb ut tahrir genge lililo anzishwa na TAQIUDDIN AL-NABHAN Mwaka 1953,na makundi mengine wakiwemo wenyewe mashia ,maibadhy masufy makhawarij na makundi mengine ambayo daawa yao ni mbovu na yenye hasad ndani yake ndio wanasamabaza fikrakama hizi na baadhi ya waisilamu wakaingia bila kufahamu IMA kwa ujinga

Allah atuongoze kuifuata manhaj salafy
 
Jackal

Jackal

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
3,982
Likes
3,066
Points
280
Jackal

Jackal

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2012
3,982 3,066 280
Saudi Arabia imewashtukia wavaa pedo watu wenye roho katili kutwa kucha kujilipua na kuua binadamu wengine kwa kisingizio cha dini,mkiwabatiza jina baya la makafiri!
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
58,859
Likes
23,964
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
58,859 23,964 280
Inaonesha mwandisha umeandika makala yako kwa chuki bila hoja za kisheria zinazothibitisha unachokizungumza


Makala ndefu lakini umejaza tuhuma badala ya ushahidi wa like uachokisema pia uitakiwa ufahamu kwanza uisilamu kisha uje kuandika makala vuzuri

Ktik mambo uiyiyagusa unasema serikali ya saudia inatumia Mali za Saudi kueneza uwahaby hapo ninaswali kidogo

UWAHABY MAANA YAKE NINI ?
Mleta mada kako pi na kupesti tu lakini kashindwa kuelezea hivyo.
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
58,859
Likes
23,964
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
58,859 23,964 280
Unajua kuna watu wanadhana kuwa ilan ni serikali ya kiisilamu wakati ni mashia sasa hili jambo litawatafuna sana tumuombe Allah atuongoze na atufanyie wepesi ktk kuendea dini hii hasa kwa kushikamana na manhaj salafy swaaleh
Watu wengi wanaipiga daawatsalafiyya kwasababu ya chuki na ujinga waliona na simu wanazosambaza wanaharakati kama
Hizb ut tahrir genge lililo anzishwa na TAQIUDDIN AL-NABHAN Mwaka 1953,na makundi mengine wakiwemo wenyewe mashia ,maibadhy masufy makhawarij na makundi mengine ambayo daawa yao ni mbovu na yenye hasad ndani yake ndio wanasamabaza fikrakama hizi na baadhi ya waisilamu wakaingia bila kufahamu IMA kwa ujinga

Allah atuongoze kuifuata manhaj salafy
= Iran

Kuweni Waislam.
 
S

Shaka-Zulu

Member
Joined
Nov 20, 2018
Messages
50
Likes
75
Points
25
S

Shaka-Zulu

Member
Joined Nov 20, 2018
50 75 25
Makka wao ndio waitunza wangetaka kuudhoofisha uislamu si wangepiga marufuku waislamu kwenda kuhiji makka
Mkuu, kama mahujaji wasingeingiza mabillioni ya dola wakati wakuhiji, basi hawa makafiri wangepiga marufuku Hija. Hata hivyo leo hii mahujaji kutoka mataifa kama Iran na Qatar wanazuiliwa kuhiji kwa sababu ya kisiasa. Kitu cha kwanza waislamu wanapaswa kufanya ni kuondoa miji mitukufu kutoka himaya ya Utawala huu.
 
Jeceel

Jeceel

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2018
Messages
205
Likes
252
Points
80
Jeceel

Jeceel

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2018
205 252 80
Mleta mada ni shia na anajaribu kuwachafua ma sunni
 
Heron

Heron

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2013
Messages
832
Likes
471
Points
80
Heron

Heron

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2013
832 471 80
Na Ahmed Rajab

SAYYID Aydarus bin Abdullah bin Sumayt, au Habib Aydarus kama wengi walivyozoea kumwita, alikuwa mcha Mungu wa kupigiwa mfano. Akipendwa mno na wenyeji wenzake wa mji wa Tarim, huko Hadhramawt, kusini mwa Yemen.

Bwana huyu alikuwa na unyenyekevu uliomfanya asiweze kumtweza hata nzi. Pamoja na kuwaongoza watu katika mambo ya dini alikuwa pia tabibu.

Hakuna aliyemwendea kwake, si mwenyeji si mgeni, aliyemfukuza au aliyemuondosha njiani. Na hakuna aliyeikanyaga Tarim asiende nyumbani kwake ubavuni mwa Masjid al-Mihdhar, moja ya misikiti mikubwa na ya kale mjini humo. Kwa miaka mingi alikuwa imamu wa msikiti huo, unaosemekana kujengwa na Sayyid Omar al-Muhdhar Abdulrahman Saggaf, aliyeishi Tarim katika karne ya 15..

Watu wakimuendea Habib Aydarus kumtaka ama awaombee dua ili wapate matilaba yao au awatibu.

Kama ilivyokuwa ada yake alfajiri ya Ijumaa ya Machi 2, mwaka huu, alisali sala ya jamaa katika msikiti wa al-Mihdhar kisha akarudi nyumbani kwake. Baada ya muda, mlango uligongwa. Ulipofunguliwa alidhihiri kijana aliyemtaka amsomee aya za Qur’an kwa sababu alisema alikuwa mgonjwa.

Habib Aydarus alimkaribisha ndani lakini alimwambia asubiri kidogo amalize kusali sala ya sunna ya dhuha. Akaingia chumba kingine na akaanza kusali.

Yule jamaa alimfuata akampiga risasi. Habib Aydarus, aliyekuwa na umri wa miaka 82, alikata roho akiwa juu ya msala, mauti yake yakishuhudiwa na mkewe.

Utajiuliza ni Mwislamu wa aina gani atayethubutu kumuua hivyo Mwislamu mwenzake, tena aliye juu ya msala akielekea Makkah akiwa ndani ya sala?

Hadi sasa aliyemuua hajapatikana. Hata hivyo, kuna kundi la Waislamu waliokuwa na sababu mbili kuu za kumuua.

Sababu ya kwanza, ni kwamba alikuwa sufi na, kwa hivyo, wakimzulia mambo kama wanavyozuliwa masufi wengine kwamba wanaingiza mambo ya uzushi (ya bidi‘a) na ya kumshirikisha Mungu katika Uislamu.

Sababu ya pili ni kwamba kwa vile alikuwa tabibu aliyepata umaarufu kwa kuwatibu wagonjwa, wakimsingizia kwamba eti alikuwa mchawi na, kwa hivyo, akenda kinyume na Uislamu.

Hizo ni hoja zinazopendwa kutolewa na Waislamu wafuatao mafundisho ya Kiwahhabi yenye chimbuko lake Saudi Arabia.

Wanawashutumu masufi kuwa wanamshirikisha Mungu ilhali ni wao wenye kumshirikisha Mungu kwa namna “wanavyowaabudu” watawala wa Saudi Arabia, kana kwamba watawala hao si binadamu wasiofanya kosa.

Kwa hakika, kutokana na vitendo vya hivi karibuni vya mwana wa mfalme Mohammed Bin Salman, ambaye ndiye mrithi wa mfalme, huu ni wakati muwafaka wa kuitafakari dhima ya Saudi Arabia, tukiwa na maana ya watawala wake katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kuna sababu kadhaa zinazowanyima watawala hao sifa za kuwa viongozi wa Waislamu, hasa wa madhehebu ya Sunni. Nitazitaja chache tu. Ya kwanza ni kwamba hii aila au ukoo wa al-Saud, uliojipachika ufalme baada ya kuua na kuiita nchi iliyoiteka kwa jina lake ni ukoo uliofurutu ada katika maovu mengi na unaoonekana dhahir ukenda kinyume na maslahi ya Waislamu.

Pili, ufalme wao si halali. Wamejipachika baada ya kuibuka washindi katika vita vya kikabila katika maeneo ya Nejd na Hijaz ya Uarabuni. Ukoo huu umetokea eneo la Nejd, lililo sehemu za kati za nchi ijulikanayo leo kama Saudi Arabia. Huko pia ndiko alikozaliwa mwanzilishi wa itikadi ya Kiwahhabi, Mohamed bin Abdulwahab (1703-1792).

Lakini, hata ingalikuwa ufalme huo ulipatikana kwa ridhaa ya watawaliwa, taasisi ya ufalme haimo katika uislamu.

Tatu ni kwamba tangu mwanzo wake, ukoo huo umekuwa ukitawala kimabavu ukishirikiana na mashekhe wao wa kiwahhabi.

Ma al Saud wana utajiri mkubwa, usiosemeka, wanaoutumia kwa ubadhirifu. Utajiri wenyewe wameupata kwa njia za haramu, za wizi wa mali ya taifa. Wanajiona kwamba wao ndio wenye haki ya kuimiliki Saudi Arabia nzima na utajiri wake wote.

Wana haki ya kufanya watakacho katika taifa la matajiri wachache na maelfu kwa maelfu ya mafukara.

Tangu miaka ya mwanzo ya 1960, watawala hao wamekuwa wakiutumia utajiri wa Saudi Arabia kwa kuisambaza itikadi ya kiwahhabi kwingineko duniani, ikiwa pamoja na Afrika. Wamefanya hivyo ili kuzivunja nguvu itikadi za kimaendeleo zisizojikita juu ya dini. Waliziona itikadi hizo kuwa ni zenye kuhatarisha tawala za kifalme za Mashariki ya Kati.

Moja ya itikadi walizokuwa wakizipiga vita ni ile ya uananchi wa Kiarabu iliyokuwa ikipigiwa debe na waliompindua Mfalme Farouk nchini Misri 1952, wakiongozwa na Gamal Abdel Nasser.

Itikadi nyingine waliyotaka kuishinda ni ile ya uBa ‘ath, iliyoanzishwa na wasomi wa Syria kina Michel Aflaq, Salahal Din al Bitar na Zaki al Arsuzi. Itikadi hiyo pia ilijikita juu ya Uarabu. Ndiyo iliyokuwa ikifuatwa Iraq enzi za Saddam Hussein na Syria (ilipokuwa chini ya Rais Hafez al Assad na sasa ikiwa chini ya mwanawe Bashar).

Na tangu apinduliwe mfalme wa Iran, Shah Mohammad Reza Pahlavi Februari 1979 na vuguvugu la Kiislamu, Saudi Arabia imezidi kuingiwa na kiwewe na imeshiriki katika njama za kuuangusha utawala wa kiislamu nchini Iran. Wameitumia itikadi yao ya kiwahhabi kuwakufurisha mashi‘a na kuleta fitna na mgawanyiko katika umma wa Kiislamu. Kuwagawanya Waislamu sio sifa ya kiongozi wa Waislamu. Hiyo ni sifa ya adui wa Waislamu.

Watawala hao wamekuwa wakiwatumia mashekhe kama Abdulrahman asSudais na Abdulaziz al Rays kuwatetea. Mashekhe hao ambao ni maimamu wa msikiti mkuu wa Makkah wamekuwa wakiwatetea katika khutba zao za Ijumaa.

Wamekuwa wakihoji kwamba ni wajib wa Waislamu wote kumuunga mkono na kumtii mfalme wa Saudi Arabia. Inasikitisha kuwasikia mashekhe hao wakihubiri hivyo huku wakitambua kwamba watawala hao hawana uadilifu wa kustahiki kutiiwa na Waislamu si wa ulimwengu mzima na wala si wa huko kwao.

Mashekhe hao na wana wenzao katika nchi zetu za Afrika ya Mashariki wameshindwa kuwakemea watawala wa Saudi Arabia kwa walivyomuua kinyama mwandishi Jamal Khashoggi. Wameshindwa kutanabahisha kwamba Shari‘a ya Kiislamu inaharamisha kabisa kitendo cha “muthla” yaani cha kuikatakata maiti kama ilivyokatwa ya Khashoggi. Hata wafiwa wa mtu aliyeuliwa na maiti yake kukatwakatwa hawaruhusiwi kumsamehe aliyefanya unyama huo.

Wamekaa kimya waislamu wenzao wenye asili ya Palestina wanavyonyimwa viza, kwa sababu za kisiasa, za kuingia Saudi Arabia kufanya ibada za hijja au umra.

Badala ya kuujenga na kuupa nguvu Uislamu, watawala wa Saudia kwa vitendo vyao wamekuwa wakiuvunja nguvu Uislamu.

Wameliharibu jina la Uislamu ulimwenguni na ndani ya nchi yao wamezibomoa kabisa turathi za Kiislamu zilizo karibu na msikiti mkuu wa Makkah na msikiti wa Mtume Muhammad huko Madinah.

Mohammed Bin Salman ameanzisha vita Yemen; matokeo yake ni kuuawa kwa maelfu ya wanawake na watoto. Asitosheke akaigeukia Qatar na kuipiga pande kwa sababu nchi hiyo haikukubali kukaliwa kichwani naye Bin Salman. Kuna tetesi kwamba alifika hadi hata ya kujaribu kuivamia kijeshi Qatar.

Halafu kuna kadhia ya Saad Hariri, waziri mkuu wa Lebanon, aliyetekwa Riyadh, Saudi Arabia, na akaamrishwa na Bin Salman ajiuzulu.

Ndani ya nchi kuna hali ya woga mkubwa.

Kamatakamata ilianza kwa nguvu tangu Juni, 2017 alipoteuliwa Bin Salman awe mrithi wa Mfalme. Maelfu ya watu wametumbukizwa jela kwa sababu wana fikra zenye kupingana na zake.

Miongoni mwa hao wafungwa wa fikra ni wanaharakati, mashekhe, makadhi, maimamu wa zamani wa msikiti mkuu wa Makkah na mahakimu. Wengi wa hao waliokamatwa haijulikani wamefungwa jela gani. Kwa mujibu wa taarifa, mashekhe na wanazuoni 60, maprofesa 50 na zaidi ya mawakili 10 wametiwa korokoroni.

Wanaharakati wanaozidi 20 nao pia wako ndani kwa kutetea haki za binadamu. Kadhalika, wanahabari 25 na waandishi 40 wamekamatwa pamoja na watu wasiopungua 60 wenye shahada za juu za uzamivu (PhD).

Watu hao mashuhuri na mahashumu si wahalifu wa sheria. Wanazipinga tu baadhi ya hatua za Bin Salman. Kati yao ni Sheikh Bandar bin Aziz Bilal, Sheikh Saleh al-Talib na Sheikh Salman al-Awdah ambaye mshtaki wa serikali ametaka apewe hukumu ya kifo.

Kuna mmoja, mchumi Essam al-Zamil, aliyefungwa jela bila ya mashtaka tangu Septemba mwaka jana kwa sababu alijaribu kuishauri serikali isiliuze shirika lake la mafuta la Aramco, kama alivyotaka kufanya Bin Salman.

Mwaka huu wanaharakati wengi wa haki za wanawake walijikuta nao wametumbukizwa gerezani.

Wengine wamekamatwa kwa sababu wamekuwa wakipendekeza kuwa mfumo wa ufalme wa nchi hiyo ubadilishwe na uwe wa ufalme wa kikatiba. Si kwamba wanataka ufalme uondoshwe kabisa ila wanataka urekebishwe ili uruhusu chaguzi za kidemokrasia.

Baadhi ya wafungwa wameteswa na wamefariki gerezani. Kati yao ni Sheikh Suleiman Daweesh. Wengine kama Sheikh Nimr al Nimr, shekhe wa kishi‘a, walifunguliwa mashitaki ya uwongo na wakahukumiwa kifo.

Mashekhe wenzao wenye kuwatetea watawala hawakuwatetea. Al Rayes, kwa mfano, amethubutu kuhoji kwenye mhadhara kwamba hata ikiwa mtawala wa Saudia “ataonekana anazini hadharani kwenye televisheni kwa nusu saa kila siku, bado unatakiwa uwafanye watu wamuunge mkono mtawala huyo, na sio uwachochee wawe dhidi yake.”

Muumini yeyote atajua kwamba huu ni uzandiki wa kujipendekeza kwa watawala wa Saudi Arabia wasiostahiki kutawala kwao wala kuwaongoza Waislamu duniani kote.
Nimeona Pumba nyiiingi sana, point ni kama ka paragraph kamoja tu,
Kanakoelezea ubaya wa koo la kifalme na wanayoyafanya.
Ila sehem kubwa ya uzi wako ni wewe kuchukia sunna. Na wewe lazma utakuwa Raafidhwa ama SUUFI tena sufi asiya hata na elmu.
Sijaona ila kila pahala unamzungumzia kwa ubaya sheikh Abdul wahaab.
 
Mccarrick

Mccarrick

Member
Joined
Jul 29, 2018
Messages
97
Likes
71
Points
25
Mccarrick

Mccarrick

Member
Joined Jul 29, 2018
97 71 25
Ningependa kukubaliana na makala yako kivingine. Wananchi wa Saudia Arabia ni Waislam kama Waislam wengine duniani, lakini watawala wa Saudi Arabia (Ukoo wa Ibn Saud) sio Waislam kabisa. Hawana tofauti na mchwa wakivamia mbao.
 
Beira Boy

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Messages
13,957
Likes
13,898
Points
280
Age
21
Beira Boy

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2016
13,957 13,898 280
Acha wehu wewe katika dini ya mnyazimungu ukikufuru au kumtakana Allah adhabu tunakukata kichwa mjinga wewe. Uislam ndo dini ya haki lazima tuwakate vichwa makafir wote Wanaoenda kinyume na Allah
 
titimunda

titimunda

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2014
Messages
6,873
Likes
8,023
Points
280
titimunda

titimunda

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2014
6,873 8,023 280
Mi siongozwi na hao wahuni.Naongozwa na Mwenyezi Mungu,Mtume (rehma na amani iwe juu yake) na Qur an tukufu.
 
jebs2002

jebs2002

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Messages
5,753
Likes
3,650
Points
280
jebs2002

jebs2002

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2008
5,753 3,650 280
Kinachowalinda watawala wa Saudia ni utajiri wao wa mafuta, biashara ya mabilioni ya dola ya silaha kutoka Marekani na nchi za magharibi hivyo hata wafanye unyama watavumiliwa tu.
Umemaliza..
Ila ya ngoswe mwachie ..... sisi wacha tupambanane na TZ...
 
Kitulo

Kitulo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
2,377
Likes
2,620
Points
280
Kitulo

Kitulo

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
2,377 2,620 280
Naomba mnieleweshe kuna tofauti gani kati ya Shia na suffi.
Pia inakuaje muislamu anakuwa Shia au Sunni mf.wakristo Mara nyingi kuwa RC,Anglican au mlutheri inatokana na kurithi kutoka kwa wazazi.
 
The 13

The 13

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2018
Messages
440
Likes
204
Points
60
The 13

The 13

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2018
440 204 60
Acha wehu wewe katika dini ya mnyazimungu ukikufuru au kumtakana Allah adhabu tunakukata kichwa mjinga wewe. Uislam ndo dini ya haki lazima tuwakate vichwa makafir wote Wanaoenda kinyume na Allah
Kwa nni msimwachie mungu awakate vichwa mwenye we huko mbinguni
 

Forum statistics

Threads 1,237,175
Members 475,465
Posts 29,280,291