Wasanii wetu kweli mmeshindwa kuziba pengo la marehemu Kanumba?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Hakika Marehemu Kanumba kaondoka na wasanii walibaki wameshindwa kabisa kuziba pengo lake.Kumbe Marehemu Kanumbi ndio aliibeba tasnia ya filamu.Nilitegemea kina JB, Ray , Wema na wengineo wangeendeleza mema yote aliyoyaacha Marehemu Kanumba , badala yake wamekuwa wapiga debe kwenye vyama vya siasa ambavyo navyo vimewatupa sijui watafanya kazi gani.
 
Kigezo cha kuwa bongo movie lazima uwe na msambwanda ulionona. Hapo ndipo shida inapoanza.

Wahusika ni wale wale bila kujali maudhui na muktadha wa filamu.

Waigizaji wanashindwa kuvaa uhusika kikamilifu badala yake filamu inageuka genge la maigizo. Inakosa mvuto.

Sijui shida ni kwamba hawana hela???
 
Bongomovie ni kimbilio la vilaza wakati wenzetu wanasomea kabisa sanaa, unakuta mwingizaji ana hadi degree 3 za sananaa
 
KWA BONGO MOVIE HAWA WANAKILILIA CHAMA CHA MAZOMBI KWA KUWATOSA KAMPENI NA KIONGOZI WAO STIV KUJICHUBUA DUME zima lina lilia kutoswa kampeni 2020 dadeki wote lazma tuimbe kugha moja shenzi
 
Kila Kitu na wakati wake, Zama za bongo movie zilishapita Hata angekuwa Kanumba hai.

Angalia tu Hata Nigeria movies zimeshuka Sana mvuto.
 
Kila Kitu na wakati wake, Zama za bongo movie zilishapita Hata angekuwa Kanumba hai.

Angalia tu Hata Nigeria movies zimeshuka Sana mvuto.
Mkuu Nollywood haijashuka hata kidogo.Sema waTanzania ndo wameacha kuzifuatilia. Hivi karibuni Nigeria ndo wakwanza Africa kununuliwa movie yao na NETFLIX. Kila kitu kinawakati wake ndio lakini kumbuka filamu ni maisha na itaendelea kuwepo as long watu wanaishi.Watu wameanza maigizo tangia enzi za akina aristotle huko mkuu mpaka leo. Bongo movie inakosa directors wenye vipaji,waandishi wabunifu wa kuandika script,na budget finyu. Waigizaji wapo wazuri sema nao hawajajitambua na wanashindwa kujiongeza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom