Wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri 2017

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,731
2,000
Habari wanajamvi...Ni matumaini yangu mu salama!!
Mwaka 2017 umekua mwaka wa mafanikio makubwa sana kwenye tasnia ya burudani nchini Tanzania hususani kwenye industry ya MUZIKI ukilinganisha na ile ya filamu.Vijana wengi wametengeneza maisha lakini pia pesa nyingi tu kupitia huu muziki ambao umetoa ajira kwa wengi sana.Ni wazi na inaonekana kila siku kwa jinsi ambavyo vijana wengi wanajiingiza kwenye hii tasnia.Sio wote wanaofanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini habari njema ni kuwa wengi wao wanafanikiwa tena si haba!
Tofauti na ilivokuwa zamani kidogo;Sikuhizi ni rahisi sana kwa msanii kutoka na kuwika.Sikuhizi media zipo allover.Studio nazo pia ni nyingi na ziko affordable.Vijana pia wanakaza si haba na mashabiki wana-show love sio kidogo!!
Hebu nirudi kwenye mada;Kama nilivosema awali 2017 ukilinganisha na miaka ya nyuma utagundua huu mwaka umetoa nafasi nyingi sana za kuwafanya wasanii wetu kutoka Tanzania kutamba Africa na worldwide.Mimi nina list yangu ambayo nadhani ndio wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri na kuiwakilisha vyema Tanzania kwa mwaka 2017 nikiwa nimezingatia vigezo mbalimbali:
Nb:Hii ni list iliotokana na mawazo yangu inaweza ikawa tofauti na yako!
  1. Diamond Platnumz:Ni wazi kwamba huyu jamaa huu mwaka umekuwa mwaka mzuri kwake toka january mpaka hapa tunapoelekea kumalizia mwaka.Amefanya mengi ambayo yananifanya nimuweke namba moja kwenye list yangu (Labda kwako anaweza kuwa wa mwisho au wa pili,whatever huu ni mtazamo wangu kwa vigezo nilivyozingatia.)Nikianza na Collabo zake na international artists kama Rick Ross..Morgan Heritage...Patoranking na wengine wengi.Deals nyingi ambazo amefanya kubwa na maarufu ni ile ya kuwa ambassordor wa Belair kwa Africa lakini pia matangazo mengi tu anayoyafanya ndani na nje ya nchi.Achilia mbali hizo pia fursa alizotoa WCB...Kupitia yeye vijana wengi wameajiriwa ambao labda wangekua wezi au mateja huku mtaani (Hakuna anaelipinga hili).Shows & products zake(Chibu perfume..Diamond Karanga....Wasafi na zingine tusizozijua) zake pia zinathibitisha kuwa jamaa ana mafanikio.Hizi ni chache kati ya vigezo nilivozingatia mpaka kumuweka namba moja kwenye list yangu.Kubwa zaidi anaipeperusha vyema bendera ya nchi yetu!!
  2. Rayvanny:From nothing to a hero...Msanii kutoka Tanzania pekee mwenye tuzo ya BET!!Hii ni archievement kubwa(Wengine hawatajua.)ukilinganisha na kazi chache alizofanya!!Pia atengeneza fanbase kubwa tu kwa muda mchache sio Tanzania tu ila Africa na nchi zingine nyingi tu...Amewekeza vyema kwenye studio(Suprise) na kumkabidhi RashDon,Kila mtu analiona hili.Studio imefanya kazi nyingi mfano ni "NGARENARO" ya Dogo janja,"OMULILO" ya Saida karoli,"NANII" ya Gaza na Madee ambazo zote zina-bang kitaa.Mafanikio sio kumiliki FERRARI au BUGHATTI so far namuweka Rayvanny namba mbili kwenye list yangu ya wasanii wenye mafanikio kwa mwaka 2017!!Kubwa zaidi anaipeperusha vyema bendera ya nchi yetu.
  3. Harmonize:Haha...Mimi ni blood fan wa huyu jamaa!!Nimejikuta nasema tu.Anyways namuweka Harmonize nafasi ya tatu kwa sababu tatu za msingi:Moja ikiwa ni sawa na ile ya Rayvanny huyu jamaa ametengeneza fanbase kubwa sana mwaka huu!!Kwa taarifa yako hakuna kitu kinachomfurahisha msanii au mtu yeyote kama anapoongeza fanbase yake na kuiona inakua siku hadi siku.Hii ipo wazi Harmonize anakua siku hadi siku.Kitu kingine na njia zilizofunguka kwake upande wa Collabo na wasanii wakubwa tu Africa akiwemo;Korede bello,Sarkodie,Mafikizolo,Jah prayzah na wengine ambao bado hawajawekwa hadharani.Sababu ya tatu huyu is the talk of town,We all know that!!Kubwa zaidi anaipeperusha vyema bendera ya nchi yetu.
  4. Aslay:As i said earlier msanii furaha yake kubwa ni pale tu fanbase yake itakapokuwa kubwa na ndipo kuna siri ya mafanikio yake..Aslay anakua kadri siku zinavokwenda (sio kiumri ila ki-muziki)Mwaka 2017 umekua mwaka wake.Kiukweli ametamba!!Asilimia 80 ya nyimbo zake zinabamba and shows pia anafanya na i estimate huyu jamaa hata mauzo yake kwenye platforms ni makubwa....Anamiliki X6 ambayo kainunua mwaka huu(Ni Mafaniko pia).Kwa vigezo hivi nampa Aslay nafasi ya 4!!Kubwa zaidi anaipeperusha vyema bendera ya nchi yetu.
  5. ..................Nisaidieni kuishusha list mpaka mwisho,Hao niliowataja hapo juu ni wale ambao kwa mtazamo wangu mwaka 2017 ulikua mzuri kwao tuongeze na wengine ambao labda sifahamu hatua walizopiga!
Nawasilisha!!
 
Ni X3,Typing error!!
 
kitalembwa

JF-Expert Member
Jul 12, 2014
1,727
2,000
sasa mkuu si useme tu WCB wamefanya vizuri ? nini unauzunguka mmbuyu ? what a shame unajitekenya na kucheka mwenyewe.......huu ushabiki maandazi utatuuwa, ingefaa heading yako iwe hivi WCB wamefanya vizuri sana 2017, content yako ndio uwapake rangi na nakshi zote.
 
Rainbow Veins

JF-Expert Member
May 24, 2017
9,491
2,000
Aiseee maandishi marefu kama hayo uwe unaacha space ili mtu avutike kusoma,
Mf,
1.Diamond______________

2.Rayvanny_____________

3.Harmonize_____________

4.Aslay__________________
Nakadhalika.

Anyway kwa mtazamo wangu hapo namba moja ni Diamond, namba mbili ni Ali kiba na namba tatu ni Aslay.
 
Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,056
2,000
ukiacha muziki wa kishabiki na ukauweka muziki wa kiki pembeni bhasi hizi pipo ndo ziliumiliki huu mwaka kwa mtazamo wangu

1. Aslay
2. Nandy
3. beka flavour
4. Ditto
5. Timbulo
6. lavalava
8.young killer
9.rosa lee
10. maua sama
11. rostam
12. barnaba
13.country boy
14. rich mavoko
 
Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,731
2,000
sasa mkuu si useme tu WCB wamefanya vizuri ? nini unauzunguka mmbuyu ? what a shame unajitekenya na kucheka mwenyewe.......huu ushabiki maandazi utatuuwa, ingefaa heading yako iwe hivi WCB wamefanya vizuri sana 2017, content yako ndio uwapake rangi na nakshi zote.
Ushabiki maandazi????I said earlier sijaandika huu uzi sababu ya ushabiki ila nimeiweka hio list nikitaja na sababu za kupanga hivo!!Kama unabishana na hii hoja weka point zako kukanusha.
 
Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,731
2,000
ukiacha muziki wa kishabiki na ukauweka muziki wa kiki pembeni bhasi hizi pipo ndo ziliumiliki huu mwaka kwa mtazamo wangu

1. Aslay
2. Nandy
3. beka flavour
4. Ditto
5. Timbulo
6. lavalava
8.young killer
9.rosa lee
10. maua sama
11. rostam
12. barnaba
13.country boy
14. rich mavoko
List yako ipo vizuri it seems Aslay yupo vizuri zaidi kwa maana anajirudia rudia!!
 
Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,731
2,000
Aiseee maandishi marefu kama hayo uwe unaacha space ili mtu avutike kusoma,
Mf,
1.Diamond______________

2.Rayvanny_____________

3.Harmonize_____________

4.Aslay__________________
Nakadhalika.

Anyway kwa mtazamo wangu hapo namba moja ni Diamond na namba mbili ni Aslay.
Sawa will take care of your advice....Lol
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,176
2,000
ukiacha muziki wa kishabiki na ukauweka muziki wa kiki pembeni bhasi hizi pipo ndo ziliumiliki huu mwaka kwa mtazamo wangu

1. Aslay
2. Nandy
3. beka flavour
4. Ditto
5. Timbulo
6. lavalava
8.young killer
9.rosa lee
10. maua sama
11. rostam
12. barnaba
13.country boy
14. rich mavoko
Naunga mkono hoja ,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom