Wasanii msitunge nyimbo za kutundika darini

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Mfano, Cosmas Chidule aliimba nyimbo nzuri kuhusu makao makuu Dodoma, lakini aliiharibu kwa kuitaja CCM kwakuwa wakati anaitunga nchi ilikuwa ya chama kimoja. Ziko nyimbo za furaha, huzuni na matukio ambazo wasanii wetu wanafanya kazi kubwa ya kuzitunga lakini zinageuka big G baada ya muda mfupi, hazidumu.

Nyimbo zote zinazotaja mwaka na majina ya watu, vyama vya siasa na vitu lazima uwe mwangalifu sana. Mfano, kama unatunga wimbo kuusifia mti wa mbuyu pale mbuyuni, itakuwaje kwa wimbo wako kama ule mbuyu ukikatwa au kuanguka na kutoweka kabisa pale?
 
Mkuu, hujawaelewa, hawa wa sasa wanaimba ili kupata attention ya mkuu au Chama kile, sio kwa ajili ya usanii, wanalipwa pia.
 
Mkuu, hujawaelewa, hawa wa sasa wanaimba ili kupata attention ya mkuu au Chama kile, sio kwa ajili ya usanii, wanalipwa pia.
Mkuu msanii kwenye wimbo wake unamsikia akisema jiji la Makamba, ghafla jiji linakuwa LA makonda, huo wimbo utakuwa umeishia hapo pia

Wenzao wanawaimbia watu baada ya kupokea hela nyingi kutoka kwa wahusika. Gulamali alimlipa pepe kale ili atunge wimbo wake wa Yanga na kumtaja gulamali.

Msanii anapaswa kuimba wimbo wa maombolezo utakaopigwa kwenye maombolezo ya msiba wowote
 
Mkuu msanii kwenye wimbo wake unamsikia akisema jiji la Makamba, ghafla jiji linakuwa LA makonda, huo wimbo utakuwa umeishia hapo pia

upo sahihi lakini wao wale wanaoimba siasa ni kwa ajili ya pesa hawalengi kesho, ila ushauri wako ni mzuri kwa hawa wanaotaka kazi zidumu
 
Sasa hivi nauona nyimbo za kampeni wanamtaja Mhe Magufuli, sasa baada ya 2025 itabidi mgombea ajaye atungiwe nyimbo zake.
Wakati huo huo nyimbo za captain Komba zinabaki kuwa universal maana alikuwa hamtaji mtu
 
Nyimbo za komba zinaonekana mpya kila mwaka wa uchaguzi, alikuwa makini sana. Nyimbo za hawa wengine Mara utasikia Chato, Mara msoga.
 
Back
Top Bottom