Wasanii kutekwa waziri Mwakyembe amesema nini?

PastorA

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
361
275
Habari zenu jamani, hili wimbi la watu aina ya wasanii kutekwa na watu wasiojulikana, na hata vituo vya polisi hawapo vipi, waziri mwenye dhamana amesha sema chochote au kushirikiana na Waziri wa mambo ya ndani juu ya hili?

Na mbona wasanii wengine hamuonyeshi umoja wa kulifuatilia jambo, kama ni majambazi au watu gani waliowateka hao wakina loma? Ushirikiano wenu na umoja wa wasanii upo wapi?

USHAURI.
Toeni taarifa kwa jeshi la polisi na kuomba msaada wa kuwatafuta hao wenzenu muache ubinafsi, unawezaje kufanya sherehe kwenya maukumbi ya starehe na wenzenu wametekwa Mungu awaamshe nyie wasanii.
 
Wasanii mmelala sana,umoja wenu uko wapi?? basata inawasaidiaje?? Waziri mwenye dhamana yuko wapi??
 
Wasanii wako instagram.... Ni unafiki wa kiwango cha lami... Wanashare picha tu.

Ila babu tale nafkiri ndo kaonyesha tofauti kidogo..
 
Screenshot_20170407-115248.png
 
jamani waziri anamambo mengi..hivi mnazani yeye atafanya kazi zoote hizo? hebu fikirieni
1.. kuingiza mashairi mazuri kwenye remix ya ya ney (inabidi mtu ajifungie peke yake kutunga mashairi si chini ya masaa 24)
2...kuwapatanisha kiba na dai (na mnajua bifu la hawa wawili so si kazi ndogo mjue)
n.k, n.k
hao watarudi tu tuwe wavumilivu kidogo ndugu zangu
 
Siku hizi mtu akipotea haina haja ya kwenda polisi kufungua mashtaka rasmi bali kulia lia instagram na kusingizia serikali imemteka jamani. Sasa roma nae atekwe na serikali kwa nguvu gani alizonazo kisiasa?
 
Huyu waziri ameshajua kuucheza mziki unaopigwa pale magogoni! kina February walishaujua mapemaaaaa! yaani hapa hakuna cha hapa ni kazi tu wala nini , Bali ni usanii kwa kwenda mbele ili mradi siku hazigandi na mwisho wa mwezi unaendelea kuja!
 
Back
Top Bottom