Kaka yake shetani
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 5,771
- 14,733
Jana Mahakama Kuu ya Tanzania, imesema kwamba Polisi haijawashikilia Deus Soka na wenzie wawili (Frank Mbise na Jacob Mlay) wanaodaiwa kutekwa maeneo ya Yombo Buza, na watu wenye silaha kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Wilson Dyansobera ambaye alisema Mahakama imejiridhisha kuwa vijana hao watatu hawapo Polisi na hivyo kutaka Polisi iwatafute.
Hukumu hii imeleta simanzi kubwa kwa ndugu wa vijana hawa, na wapenda haki wote nchini. Lakini pia imeset "precedence" kwa matukio ya utekwaji na watu kupotea;
1. Hukumu hii inamaanisha ukifuatwa mtaani na watu wasio na sare za Polisi, vitambulisho na arrest warranty usikubali kwenda. Pambania uhai wako, bora wakuulie hapo ulipo kuliko wakupeleke huko wanakotaka. Kwa lugha rahisi bora ufie nyumbani ndugu zako watakuzika, kuliko ukafie pasipojulikana na ndugu zako wasione hata maiti yako.
2. Hukumu hii inamaanisha baadhi ya Polisi wenye "nia ovu" wanaweza kukukamata na baadae wakakanusha sio wao na usiwe na la kufanya. Na mahakama itakosa ushahidi wa kuwatia hatiani.
Pia soma: Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea
3. Hukumu hii inamaanisha kwamba Tanzania kuna genge la kuteka watu ambalo sio sehemu ya jeshi la Polisi. Kama Mahakama inakubali kuwa akina Soka "walitekwa" lakini sio na polisi, it means mahakama inakubali genge la utekaji lipo. Je genge hilo limeundwa na nani? Linamtumikia nani? Kwa maslai gani?
4. Hukumu hii inamaanisha kuwa vyombo rasmi vya ulinzi vipo dhaifu kiasi kwamba raia wanaweza kutekwa kwenye nchi yao na "genge la watu wasiojulikana" na Polisi wasiweze kuzuia.
5. Hukumu hii inamaanisha usalama wa wakosoaji wa serikali upo mashakani. Hivyo basi usitembee peke yako. Kama wewe ni mkosoaji wa serikali hakikisha hukai kifala.
NB: Ni bahati mbaya haya yote yanafanyika katika nchi inayojinasibu kuheshimu uhuru wa maoni na utawala wa sheria. Ni bahati mbaya zaidi kuwa Waziri wa mambo ya ndani anajisifia kuwa nchi ipo salama wakati kuna watu wanadaiwa kutekwa na kupotezwa na hakuna hatua za maana zinazochukuliwa kukomesha vitendo hivi!