Ni kweli magufuli ni mtu mzuri sana katika uongozi hilo halipingiki. maana tumemuona akiweza kuongoza wizara kadhaa.
Pia ni mzuri wa kucheza na vyombo vya habari kuhakikisha lengo na dhamila yake inajulikana kwa walengwa ambao ni watanzania.
Kuna kitu kikubwa sana ambacho mimi nazani anakosa, nacho ni busara ya kuwa rahisi licha ya kuwa ni mzuri katiaka ungozi ya ngazi ya uwaziri.
mimi najua kiongozi mzuri(ngazi ya urais) ni yule anaweza kutumia watu wake (viongozi wa chini yake) kuhakikisha anafikia malengo yake kwa ukamilifu bila kupotoshwa, kiongozi mzuri ni yule anaweza kutoa kauli na ikafuatwa na watu wote bila kinyongo wala malalamiko kutokana na yale anayosisitiza ndio anayotenda.
Mgufuli ananipa wasiwasi kama kweli atatufaa, maana mambo yote anayosifiwa ni yale ambayo tumeona katika vyombo vya habari akiwa katika eneo la kazi anafokea mapungufu aliyoyaona( unprofessional actions ) kwa mtu anaejua ni rahis kuficha ukweli, pia ni ishara kwamba viongozi wa chini yake walikuwa na nafasi nzuri ya kuripoti kwake.
Pia atueleze ile kesi ya samaki( alimaarufu samaki wa magufuri) nini hatima ya wale wezi, nini tanzania imenufaika kutokana na lile tukio.pia angalau atulizishe kwa kutuambia ukweli kausikaje na uuzaji wa nyumba za nationa house. kumbuka tunataka kumpa maisha yetu na watoto wetu atuongoze kwa muda mrefu, ni lazima tuwe na uhakika na tunacho fanya.
Pia nitafurahi akituakishia watanzania ni nini atakifanya ndani ya siku 90 akiwa rahisi kwa mafisadi wote ambao wanajulikana na ushaidi umesha tolewa
Nikiwa kama mtanzania wa kawaida nisiokuwa na masirahi binafisi na chama chochote zaidi ya utanzani, nivizuri nikajua. pia kwa maongezi haya haimaanishi kuwa naunga upande wa pili, kadili muda unapo ruhusu pia kuna mambo mengi napenda lowassa chini ya mwanvuli wa ukawa nitapenda anipatie ufafanuzi