Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Asilimia karibu zaidi ya 90 wasanii wa bongo flavour hujikuta wote wanaimba nyimbo nyiingi zinazofanana mlengo,na hii hutokea kwa sababu KARBU WOTE HUIMBA KUHUSU MAPENZI..na huwa wakiulizwa wanadai eti wanaangalia sisi hadhira tunapenda nini.
Lakini ukweli ni kuwa sio kweli kuwa hadhira sisi tunapenda nyimbo za mapenzi tu bali nyimbo zinazogusa nyanja zote za maisha ya binadamu ilimradi tu uguse hisia za mwanadamu wimbo huo utapendwa tu..
Jifunzeni na someni nyakati Angalia kwa mfano wimbo huu wa NEY PAMOJA NA KUWA NA LUGHA KALI KIDOGO LAKINI NDIO HALI ILIYOPO KWA SASA KWANINI USIPENDWE?..
Watu kama
LUCKYDUBE,MICHAEL JACKSON nk HAWAKUIMBA MAPENZI SANA LAKINI HADI LEO WAMEKUFA KIMWIILI KIMUZIKI BADO WAKO HAI.
INAPENDEZA SANA KUSIKILIZA WIMBO WA MAREHEMU AKIWA AMEIMBA MAMBO Mema NA SIO MAPENZI huwa nyimbo zingine zinawahukumu wasanii wenyewe..
Jifunzeni ili mje muishi pamojana vizazi vijavyo kimuziki..