Wasamaria wema waokoa Sh. bilioni 11 za kodi

Makini

Senior Member
Dec 23, 2014
154
59
Utaratibu wa kuwazawadia wananchi wanaotoa taarifa za ukwepaji wa kodi umeokoa Sh. 11, 084,166,416 baada ya wasamaria wema 62 kutoa taarifa za vitendo vya ukwepaji kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo, alisema utaratibu huo ni moja ya mipango iliyobuniwa na mamlaka hiyo kudhibiti ukwapaji kodi na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali.

"Shabaha kubwa ya mkakati huu ni kuwafanya wasamaria wema kufichua wakwepa kodi na kuhakikisha serikali inakusanya mapato zaidi yatayosaidia kuharakisha maendeleo ya Watanzania," alisema.

Alisema chini ya mpango huo wasamaria wema 62 wamefaidika kwa kuzawadiwa Sh. 193,857,720 kwa kutoa taarifa ambazo zimesaidia kuokoa mabilioni ya fedha zilizotolewa na TRA katika kipindi cha mwaka 2014/2015.

"TRA inawashukuru wote waliofanikisha kuokoa kiasi hiki kikubwa cha kodi kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu ambao kwa makusudi hukwepa kodi na kulipotezea taifa mapato," alisema.

Kayombo alisema TRA ilianzisha utaratibu wa kuwazawadia wananchi wanaotoa taarifa za ukwepaji wa kodi kwa kuwazawadia asilimia tatu ya kodi iliyookolewa na kiasi cha zawadi kinatakiwa kisizidi Sh. milioni 20.

"Katika mpango huu taarifa za ukwepaji kodi zinazotolewa huchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu na kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kuhakikisha kwamba ni za ukweli na mtoa taarifa hubaki kuwa siri ya TRA," alisema.


Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusu vitendo vyovyote ambavyo vinasababisha mapato ya serikali kupotea ili kuweka uwiano sawa wa kila anayestahili kulipa kodi alipe kwa mujibu wa sheria.

"Mwananchi yeyote mwenye taarifa za ukwepaji wa kodi anashauriwa kupiga simu namba 2137638 au 0784 210208 au anaweza kufika TRA Idara ya Uchunguzi wa Kodi, baada ya hapo hatua stahiki zitachuliwa na mamlaka," aliongeza kusema Kayombo.

Chanzo: Nipashe
 
Kumbe dili kuchongeana!!
Na tulivyo hatupendani sisi wabongo,wengi wataenda na rungu.

Hivi unajuaje kama anakwepa kodi?
 
Mbona hayo alikuwa hayasemi kabla Dk.Magufuli hajakamata usukani wa kuongoza Taifa letu??

Binafsi nina imani kubwa na Dk.Magufuli katika harakati zake za kuwadhibiti wakwepaji kodi wakubwa,ingekuwa bora zaidi kama angefumua TRA na kuisuka UPYA kuanzia kwa Mkurugenzi mkuu wa hivi sasa mpaka wakuu wote wa idara mbali mbali,ikiwezekana walio kaa muda mrefu kwenye vitengo hivi wahamishiwe Wizara nyingine, Mkurugenzi mkuu anapaswa kupitishwa kwenye tanulu la wasahili walio bobea, haipendezi watu kuteuliwa teuliwa kienyeji au kwa kujuana/pigiwa debe tu.

Alternatively TRA waige mbinu za Wizara ya mambo ya ndani wahakikishe wafanya kazi wa ngazi za juu hawakai sehemu moja ya kazi kwa muda mrefu wawe wanahamishwa mara kwa mara ili wazizoeleweke.
 
Duh hebu tupeni vigezo vya dalili ya mtu asiyelipa kodi tuchangamkie fursa hiyo tugawane utajiri
 
Mmh, sasa hawa jamaa si wanaweza wakajimegea 3% hovyo hovyo kwa kisingizio kodi iliyolipwa ilitaka kukwepwa wakati sivyo
 
Back
Top Bottom