Wasaidizi wa Rais waseme ukweli

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Habari za Asubuhi wana Jamii!

Ni matumaini yangu, Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema katuamsha salama, na kwa wale wenzetu wana changamoto za afya tunawaombea wapone haraka na warudi kwenye majukumu yao ya kila siku!

Leongo la uzi huu, wasaidizi wa Rais wamekuwa na tabia yakusema jambo au mambo ambayo sio ya kweli. Kwa mfano ulio wazi kabisa! Jumamosi ya tarehe 27.02.2021, kulikua na kikao cha Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kilifanyika kwa njia ya mtandao!

Kwenye kile kikao, Madam Makamu wa Rais ndiyo alituwakilisha sisi Watanzania! Na hata kwenye ile video clip, ambayo, karibu wa kila mtu kaiona kwamba Rais wa Kenya, Mh Uhuru Kenyatta, akimkaribisha Madam Makamu wa Rais, na Madam Makamu wa Rais, alisema kabisa kwamba anamwakilisha Rais Magufuli, jambo ambalo halina shida kabisa!

Lakini taarifa ikaja, Mh Magufuli Rais wetu ndiyo kahudhuria kile kikao! Sasa swali langu, wasaidizi wa Rais, mbona wanadanganya Watanzania, wanafanya vile kwa faida ya nani? Hawaoni kabisa kua, Wao ndiyo chanzo cha kumugombanisha Rais na Raia wake? Je, Madam Makamu wa Rais, anajisikiaje? Kazi afanye yeye, apewe credit mwingine? Je, Wakuu wa Nchi, Jumuiya ya Afrika Mashariki,wanatuonaje sisi Watanzania? Kwamba kwenye kikao alikuwa Makamu wa Rais,taarifa ikatoka kwamba kikao kilihudhuliwa na Rais Magufuli!

Mh Rais kama unaweza jenga mahusiano mazuri na wananchi wako, ni bora watu wanaopotosha uwe unawafukuza kazi!

Nashangaa hadi sasa hivi Bwana Gerson Msigwa hajaomba samahani kwa Watanzania kujutia kosa lake au hata kuwajibika kwa kuachia madaraka yake haraka!
 
Teh teh wanasikitisha sana yaan kuanzia juzi wanahangaika kuhakikisha kiwa amini walichokisema.

Yaan imekua kama vile no dhambi Mh kuwakilishwa? Mbona mara kibao tu anamtuma Bi Samia SADC, UNGA?
 
Bwana Mangungu wewe ulikuepo kwenye hicho kikao?

Mimi nashauri jishughulishe na mambo yanayokuhusu.
 
Amka toka ukatafute maisha ya watoto wako, mapema asubuhi unaamka na majungu yatakusaidia nini sasa kwenye maisha, maisha ya watu wewe ushupaze shingo.
 
Rais alikuwepo. Alishiriki via video akiwa ikulu ya dar. Taarifa za habari zote zilimuonesha akishiriki.
 
Back
Top Bottom