Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Kwa kweli kauli za mkulu zina ukakasi sana. Wamwandikie hizo speech awe anasoma. Yani nawaza tu ikiwa sisi wengine tunamwona kwenye tv tu tena sio kila siku tumechoka na kauli zake ngumu,je mkewe aliyeishi naye miaka yote hii sijui kachokaje!!!?
 
Ney wa mitego ktk song lake anamuuliza we mtu gani hutaki kushaurika
Alafu akacheka kicheko cha dharau eti mkuu anajifanya mdogo wake yesu

Nadhani jumatatu huyu msanii atakuwa pale kwa kamanda siro
 
Je ni vema kusema washauri hawamshauri Raisi wetu? Labda wanajua hawawezi kusikilizwa au wanashauri lakini uamuzi wa kuchukua ushauri ni wake anayeshauriwa! Issue ya Makonda wa kwanza kumsaidia Raisi alikuwa awe Makonda mwenyewe kwa kuamua kwa dhati ya moyo kwamba najidhuzuru ingekuwa ni heshima kubwa kwa Raisi! Cha pili kama ni uongo angetoa vyeti kuthibitisha ukweli wa yeye kutokupata zero! Matokeo yake ni kwamba ujasiri wa kutaja majina ya watuhumiwa wa madawa ikageuka ndiyo uthibitisho wa cheti; ambazo ni maada mbili tofauti! Ni hoja zisizofungamana! Pamoja na makonda kufanya uthubutu lakini amekosa uadilifu na upendo kwa Raisi! Ukweli ni msingi wa njema zote za binadamu na bila ukweli hakuna maendeleo yoyote yanaweza kupatikana hapa duniani na ahera!
 
Pasco, washauri wameshindwa kuendelea na kazi hiyo maana mkuu wao hashauriki na hilo ameliweka wazi mara nyingi tu. Ushauri alioutoa Dr Bisimba ndiyo uluobaki kufanyiwa kazi!
 
Mkulu alishasema hapangiwi sasa tufanyeje?
```Naye akawajibu "Msinililie Mimi, jililieni ninyi na kura zenu, kwa maana hakuna aliyewalazimisha mpange foleni siku ile." Basi wakainamisha nyuso zao kwa huzuni, wala wasiweze kumjibu. Naye akiisha kusema hayo akapita katikati yao akaenda zake bandarini``` (Watanzania 5:20)
 
Kabisa mayalla hata mimi nimeona huo mjadala wa jicho letu kutoka star tv, ni kweli habari kubwa ilikuwa Waziri kutishiwa silaha na sio kutembelea bandarini kwa mheshimiwa.
 
Ameshawaambia yeye ni rais anayejiamini.. Sasa sijui anafikiri kupokea ushauri ni aina ya kutokujiamini!

Hilo mimi sijui.. Ila ndivyo inavyoonekana.
 
Wanaanzaje kumshauri mtu anaejua kila kitu? Yuko juu ya yote na kashasema ukimpangia ndo unaharibu kila kitu

Kwani Nape alikosa nini mpaka akatenguliwa uwaziri? Si ameingilia uhuru wa JPM,mtu kashasema msimuingilie utaharibu kila kitu.
 
IMG_20170324_195515.jpg
 
W
Hii nchi inahitaji uongozi wa kiamri..uongozi wa mashauriano ulishafeli..wacha twende na huu maana unaonyesha njia..siku zote maendeleo ya nchi huletwa na uthubutu wa wachache..na wengi huachwa nyuma kama ilivyokuwa kwa nape na wenzie..
Ushawahi kusikia hii methali..ukitaka kufika haraka tembea peke yako..lakini ukitaka mbali tembea na wenzako..au kimombo if you want to go faster go alone if you want go far walk with others.
 
Hivi kipi cha muhimu " uhai wa mtu " au "kutembea bandarini",
1. Nape ametishiwa kuuawa kwa bastola....sasa unategemea mtu aliyetishiwa kuuawa kwa namna nyingine tunaweza kusema ingefyatuka je. Sasa waandishi waache kutetea uhai wakufuate wewe kwenye kukurupusha bandarini. Na mawaziri uliowapanga uwaamini hadi uende wewe.
2. Makonda issue ni ile ile, kavamia na bunduki. ..Maana yake kaenda liwalo na liwe, hata kuua sawa. Swala ni UHAI.
3. Huyo Pombe kama ulivyosema anakosa Washauri. Au wanamwogopa kumwambia unaharibu na kubaki kuinamisha vichwa ndio mkuu. Wakati wanajua kaboronga. Ni kumwambia ajue hii ngoma hamna wai kuitoa.
4. Nakumbuka kwenye hotuba zake za kuomba kura alisema "tulimwambia Rais mkapa mtu huyu hafai akang'ang'ana" sasa yeye kaingia madarakani na anafanya issue ile ile ya kutosikia sauti. Amekaza uso kama gume gume. Hadi ajue atakuwa kachelewa
 
W

Ushawahi kusikia hii methali..ukitaka kufika haraka tembea peke yako..lakini ukitaka mbali tembea na wenzako..au kimombo if you want to go faster go alone if you want go far walk with others.
Sasa si umeshafika ulipotaka kwenda..umeshasema umefika..mi nataka kwenda kariakoo..nimefika..mbagala nifate nini..?? Nikitaka kwenda mbagala nitajiandaa kwenda mbagala..usigeuze haramu kuwa halali
 
Back
Top Bottom