Wasafirishaji mnafanyaje hii biashara??

-Hilo gari una uhakika wa abiria wa Kahama tuuu!
Jibu ni hapana. Hivyo,hesabu hiyo kwa siku huwezi kuipata.
-unajua maintenance ya gari?
-umeshaweka gharama utakazoibiwa?
Je, baada ya wiki likipata ajali?

Kwenye hesabu za biashara ukilenga faida bila kukumbuka na hasara utalia. Sema kwa hesabu zako,anaongezea kidogo anapata za mchina 2, hesabu itakayolala ndo hiyo hiyo
Ndio maana sijapigia siku 365 mkuu. Lengo ni kuweka hizo unforeseen events zote.
 
Biashara ya Gari:

Phase One: Inaingiza: Haili kabisa(Garage)—Ndio kipindi cha kukusanya hasa hela. PROFIT 95%

Phase Two: Inaingiza: Garage kidogo—Bado unakusanya kingi, ila sio kama phase one. PROFIT 80%
Phase One & Two just two years.

Phase Three: Inaingiza: Inakula kiasi kikubwa (Garage 50-60% of Running Cost). PROFIT 40-50%
Huu ni mwaka wa Tatu.

Hapa unapeleka njia ya pori, inafanya kazi kiangazi tu sababu abiria ni wengi, hawachagui gari, ni wavumilivu kwa delays tofauti na wamjini, mizigo mingi na abiria unabeba upto 50% zaidi ya uwezo—hence big revenue; So cash flow ni kubwa. MAY to OCTOBER.

Business model hii ndio inafanya kampuni kama Allys imedumu sana kwenye biashara. Nguzo ya Allys ni upcountry routes.
Huu ni mwandiko wa mtu mzima mwenye akili zake
 
Just imagine milioni 700+ afu unapakia abiria 50 kwa elfu 50 Dar Kahama, unalipa wafanyakazi, engine kubwa inanyonya mafuta kama walevi wa KASKAZINI.

Bado ukodi ofisi, trafiki, Latra etc!!
Mnapigaje hapo???View attachment 2854877
50×50=milioni mbili na nusu
Siku hizi mabasi yanabeba sana vifurushi na mizigo na vinaingiza hela nyingi sana
Jumla safari moja inaweza kupatikana milioni tatu
Mafuta=milioni
Wafanyakazi na mengineyo=milioni
Boss=milioni
Mara miaka miwili boss ananunua chuma mpya
Anakuwa nazo mbili
 
Scania kwa 710 Mil = wachina wawili, na kama wakiacha kuweka vile vitaa vya rangirangi nyingi wanavyochanganyikiwa navyo waluguru, basi ni wachina watatu
 
Katika iyo 50,000 Kuna Kodi zaidi ya 25% pia,,Kuna zaidi ya 25% Tena kama gharama za uendeshaji,biashara ina faida kwa Hali tata sana mpaka uingie ngomani ucheze ndio utaelewa utamu wa mchezo,,mfanyabiashara anataka ukwasi au wanaita CASHFLOW au tuseme EQUITY ili aweze kufanya mambo mengi kwa mapana hapo ndio anapoweza kutengeneza faida kwa haraka haraka utaona kama anapoteza au hapati faida lakini kwa uhalisia anapata faida maradufu.
Kodi za bus kama sijakosea n milion 3, flat rate
 
hio 2.5 jumlisha na fungu lingine la mizigo kama kama kamilioni plus hivi kamejificha humo
 
-Hilo gari una uhakika wa abiria wa Kahama tuuu!
Jibu ni hapana. Hivyo,hesabu hiyo kwa siku huwezi kuipata.
-unajua maintenance ya gari?
-umeshaweka gharama utakazoibiwa?
Je, baada ya wiki likipata ajali?

Kwenye hesabu za biashara ukilenga faida bila kukumbuka na hasara utalia. Sema kwa hesabu zako,anaongezea kidogo anapata za mchina 2, hesabu itakayolala ndo hiyo hiyo
Mkuu,
Kwa mawazo yako huwezi kuwekeza maana hata sisi binadamu mwisho wetu Ni kifo

Wekeza Kama kesho haipo
 
Ili upige hesabu sahihi za biashara unahitaji kujua umbali wa kutoka point A-to-B

Bei ya bus

Durability (longevity) lina uwezo wa kwenda miles ngapi kuanzia jipya (au uliponunua), hadi kuwa mkangafu (ili uweke na hela ya kununua lingine).

Siku ngapi kwa mwaka litakuwa barabarani

Idadi ya viti kwenye bus

Uwezo wa bus kula mafuta ya litre moja per mile, bei ya mafuta kwa litre.

Unafanya full services kila baada ya miles ngapi na gharama zake.

Matairi yana uwezo wa kwenda miles ngapi kabla ya kutakiwa kubadilishwa.

Bei ya tairi moja

Asilimia ngapi ya administration costs za ofisini unataka basi libebe

Fees za serikali kwa mwaka

Insurance cover kwa mwaka

Mshahara wa madereva, konda na mhududumu kwa mwaka.

☝️Hizo info unaweza fanyia hesabu za cost ya kuendesha basi kwa mile 1, wewe sasa uamue kiasi gani cha faida uongeze kila miłe moja kwa kiti.
 
50x50,000 = 2,500,000 hii ni kwa siku.

2,500,000 x 280 = 700,000,000 (tume assume lina fanya kazi siku 280 tu kwa mwaka).

Chukua 700,000,000 x miaka 3 unakua hujarudisha hela ya kununulia? Yani hapo weka na hizo gharama zote kuanzia matengenezo nk nk!
Kuna pesa inapatikana kwenye mizigo pia.
 
Ili upige hesabu sahihi za biashara unahitaji kujua umbali wa kutoka point A-to-B

Bei ya bus

Durability (longevity) lina uwezo wa kwenda miles ngapi kuanzia jipya (au uliponunua), hadi kuwa mkangafu (ili uweke na hela ya kununua lingine).

Siku ngapi kwa mwaka litakuwa barabarani

Idadi ya viti kwenye bus

Uwezo wa bus kula mafuta ya litre moja per mile, bei ya mafuta kwa litre.

Unafanya full services kila baada ya miles ngapi na gharama zake.

Matairi yana uwezo wa kwenda miles ngapi kabla ya kutakiwa kubadilishwa.

Bei ya tairi moja

Asilimia ngapi ya administration costs za ofisini unataka basi libebe

Fees za serikali kwa mwaka

Insurance cover kwa mwaka

Mshahara wa madereva, konda na mhududumu kwa mwaka.

☝️Hizo info unaweza fanyia hesabu za cost ya kuendesha basi kwa mile 1, wewe sasa uamue kiasi gani cha faida uongeze kila miłe moja kwa kiti.
Ungeiwekea namba huu ufafanuzi nadhani ndiyo jibu sahihi la thread hii..
 
Ungeiwekea namba huu ufafanuzi nadhani ndiyo jibu sahihi la thread hii..
Binafsi sina biashara ya bus

Sijui bei ya bus

Kila bus manufacturer anashauri wake ufanye full services baada ya miles elfu kadhaa

Sijui umbali wa Dar-Kahama

Administration costs za ofisi

Mfanyabiashara ana ma-bus mangapi ili hizo administration azigawe kwa mabasi

Sijui kutoka Kahama mpaka Dar bus lina madereva wangapi, mshahara wao ni kwa trip au kwa mwezi

Ulaji wa mafuta la bus husika, etc na info zingine nilizoweka hapo kama insurance, license fees na tozo zingine.

Hizo ni info unazohitaji kufanyia services costing ya bus upate unit cost per mile kwenye biashara ya usafirishaji wewe sasa uamue uongeze faida kiasi gani.

Weka details nikupigie hesabu
 
Back
Top Bottom