Wasafirishaji Madawa ya Kulevya Watano Wanyongwa Iran | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasafirishaji Madawa ya Kulevya Watano Wanyongwa Iran

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wanaume watano waliopatikana na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya nchini Iran, wameuliwa kwa kunyongwa.
  Wanaume hao ambao majina yao wala nchi wanazotoka hazikutajwa, walinyongwa jana kwenye jela ya Khoramabad katika mji wa Lorestan, magharibi mwa Iran.

  Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran, Aftab, wanaume hao walikamatwa na madawa ya kulevya wakati wakijaribu kuyasafirisha na kuyasambaza madawa hayo ya kulevya.

  Tangu kuanza kwa mwaka huu, ndani ya wiki mbili jumla ya watu 41 wamenyongwa nchini Iran.

  Watu wanaopatikana na hatia ya makosa ya mauaji, kuzisaliti ndoa zao, ubakaji, ujambazi au kusafirisha madawa ya kulevya, huhukumiwa adhabu ya kifo.
   
 2. m

  makeke Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa unataka nini? wache wauliwe hao madrug dealer kwa kuwa wao wanaua wengi.
   
Loading...