Wasafiri kuchimba dawa ktk karne hii si sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasafiri kuchimba dawa ktk karne hii si sawa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kimatire, Jul 10, 2009.

 1. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hilo nalo linaniacha hoi hasa nikisafiri na mabasi yetu yaendayo Mikoani!!Kwamba , imezoeleka kuwa basi lisimame porini abiria washuke kwenda kuchuma dawa.Kwa wale ambao hawafahamu msemo huo ni kwenda kujisaidia haja ndogo na kubwa porini!!Karne hii ya uharibifu wa mazingira,maradhi lukuki ya kuambukiza,kipindu pindu,kichocho na wenzake bado watanzania tunajisaidia porini kuwaachia wengine maradhi ilimradi wasafiri tumefika salama???Jamani hakuna uwezekano wa kuwa na vituo vyenye vyoo katikati ya mapori yetu hata kama ni vya kulipia wasafiri wakavitumia kuliko neno hilo linalotumika kwenda kuchuma dawa?.Bado karne hii tuko kwenye maisha ya ujima kiasi hicho??JF hebu tuwe mawakili katika kupinga uchafuzi huu wa mazingira yetu.
   
 2. B

  Bananzego New Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda Wabunge wamekusikia, tena niongeze kusema kuwa wanawake wanadhalilika sana wanapochimba dawa safarini, utakuta huyu kachuchumaa, mara yule kasimama na kashusha mtindo wa bhong'o na kibaya zaidi baada ya kuchuma hiyo dawa no soap no water!
   
 3. F

  FRANKLIN Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekubari swala la kuchimba dawa ni baya sana kwasababu sio tu uchafuzi wa mazingira nipamoja na kuongeza kasi ya utekajinyara kwenye mapori.abiria wanapo shuka kwenda kujisaidia wanasimama na majambazi hupata nafasi ya kuwateka na kuwanyang'anya kilakitu walichonacho. Hivyo ujengaji vyoo pamoja na kuweka vituo vya polisi ilikuongeza usalama wa raia wa Tanzania.
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hivi nyinyi mnaelewa maana ya kitu kuitwa HAJA? Au mnaongea tu? Haja ndiyo maana ikaitwa hivyo. Haingalii wakati au utashi wako. Inakuja tu, na inapokuja inakutaka utekeleze amri yake. Usikaidi inaweza kukuadhiri. Inajichukulia madaraka na kupasua njia.

  Kujenga vyoo njiani si mbaya. Lakini ujue kuna wakati haja haitakusubiri mpaka ufike kituoni. Itakutaka hic et nunc. Kumbe tujenge vyoo, lakini tujue kwamba bado tutalazimika wakati fuani "kuchimba dawa" kwa lazima.

  Mi nafiri njia nzuri zaidi ni kuanza kuingiza mabasi yenye vyoo. Nchi zingine wanayo magari ya aina hii. Kumbe mtu akiwa na shida anaenda kumaliza shida zake bila shida.
   
 5. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bado hili halijapata ufumbuzi
   
 6. GP

  GP JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hii staili ndio nzuri bana.
  kwanza ukichimba dawa pale porini unakua umeweka mbolea
  teh teh teh teh
   
 7. S

  Salehe Ndanda Member

  #7
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua 'KITU HAJA' Inawezekana ujawahi kushikwa na haja. Haja ukizidiwa kweli kweli haina adabu popote inatoka hata kama umesimama kwenye lieso itatoka tu.Kuchimba dawa umekukuta na utakuacha 'WALIOZIDIWA WATAENDELEA KUCHIMBA DAWA KAMA KAWAIDA' wote waliozidiwa waendelee kuchimba dawa RUKSA, hakuna anayefanya kusudi ili acheleweshe safari.Usifikili wanao safiri wote wapo ok, unaujua ugonjwa wa kisukari?
  unajua maradhi mbali mbali? unaweza kujisaidia al jazira kabla ujafika Iringa ukajisikia kujisaidia je utajisaidia kwenye gari au vipi? je utamuomba konda mfuko ujisaidie au utakuwa umepanda na mfuko wako? it's very terrible. ANAYEOMBA KUCHIMBA DAWA NI MMOJA AU WAWILI LAKINI WENGINE ADVANTAGE.

  WAKATI UMEFIKA WAKUPATIWA MABASI YA KISASA YENYE CHOO NDANI
  SIO KUCHUNGULIA AU KUCHEKA ESPACIALLY YA MIKOANI.


  MBONENYAI.
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni swala njeti sana. Kwa kweli atu akili zinamruka kabisa pale anaposhikwa kisawasawa na haja. akili itarudi pindi pale atakapo chimba dawa.
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nimewahi kuambiwa na mtu mmoja kuwa mkojo wa asubuhi ni dawa ya macho na maradhi mengine (sikumuuliza magonjwa gani) kama utakuwa unakunywa kila siku asubuhi(yeye huwa anakunywa).Na ukija kwenye haja kubwa nasikia pia(sina uhakika) wachina huwa wanahifadhi na wanatumia kama mbolea.
  kama hayo ni kweli na ukizingatia ni porini inawezekana ni vema tu mbolea iongezeke kwa mimea ya asili.Lakini ikija kwenye swala la usalama kwa vitu hatari kama nyoka na majambazi kuna haja ya kutafuta ufumbuzi wa suala zima la kuchimba dawa.
   
 10. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Ni kawaida ya wasafiri wa safari ndefu kusimamisha basi porini na kujisaidia maarufu kama kuchimba dawa. Sitaki kukubali kwamba ni stahili ya msafiri kundelea kuchimba dawa katika karne hii, kwa mfano safari ya mbeya kuanzia tarehe 1 Sept 09 ni zaidi ya masaa 14 sababu ya speed limit ya 80km/phr na mizani na ukaguzi kila katika mji mdogo. Hii maana yake kila mtu atahitaji japo mara moja kuchimba dawa.

  Kama kawaida bongo hakuna anayehusika lakini inadhalilisha sana utu wa wasafiri, manake wake kwa waume, wakubwa na watoto vichakani tena mnaonana sababu mmebanwa hakuna anayejali. Wanasiasa na waandishi wako busy na mafisadi lakini kuendelea kuona watu wakijisaidia vichakani si sawa, kwanza ni hatari sana kwa magonjwa ya milipuko na uharibifu wa mazingira, kwa mfano mbele kidogo ya njia panda ya mzumbe kuna sehemu wanauza nyama choma halafu ndio hapo hapo abiria wanachimba dawa na wamepewa dk 10 na konda. ingekuwa mafua ya nguruwe kutoka nje mpango mkakati ungetengenezwa kukabiliana na mlipuko lakini hii abiria anachukua time na kuugulia aendako. Yote tisa kumi hizo hotel ambazo zina matundu yasiyozidi manne ya choo nje kuna basi zaidi ya 10 na abiria anapewa dakika 10 kula na kujisaidia.

  Binafsi ningetoa wazo kwa wajasiria mali humu jamvini, kama kuna mtu anamtaji au anaushawishi katika mifuko ya hifadhi za jamii basi asisite kuwekeza katika vyoo njiani, manake wachina katika olimpiki walitengeneza magorofa kwa ajili ya vyoo tu. Choo na faragha ni muhimu katika maisha ya binadamu wa leo. Taasisi za kutetea haki za kinamama na mazingira ningetegemea wangekuwa mstari wa mbele kupinga utaratibu wa kuchimba dawa, mbona kuna vyoo katika ndege ili watu wajisitiri wakiwa safarini katika mfumo wa kiungwana zaidi.

  Nawasilisha kwa mawazo mapya tufanyeje ili tusiendelee kuchimba dawa safarini, ni hatari kwa afya na uharibu wa mazingira ukichukulia kundi kubwa la watu kwa mara moja watu hawana maji au toilet paper za kujifutia na wanarudi vitini. Tukumbuke barabara zetu ni za kimataifa na watu kutoka mataifa mbali mbali wanapita na kutushangaa na kushangaa hii style yetu isiyostaharabika na kukubalika.
   
  Last edited: Sep 7, 2009
 11. F

  FM JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mjomba akiwa safarini anapenda kuona kuona miti ikirudi nyuma na kipindi cha kuchimba dawa, sijoajua ni kwaa sababu gani. Lakini kwa vyovyote vile huu utaratibu sio mzuri. Kipindi fulani kampuni ya Scandinavia waliwahi kwa na mabasi yenye huduma ya choo, naamini huu ulikuwa utaratibu mzuri sina hakika kama bado unaendelea. Ningeshauri ofisi zinazohusika na masuala ya mazingira kwa kushirikiana na wizara ya afya kuandaa muswada wa sheria itakayolazimisha mabasi yote ya safari ndefu kuwa huduma ya choo, full stop!.
   
 12. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Scandinavia walijaribu japo kwa Paradiso class lakini wanaonekana wako hoi sasa na ni mabasi machache sana na gharama ni kubwa kwa wananchi wengi, ukweli basi roli (Mabasi yanayoundwa kwa chasis za maroli) bado yako mengi na hata mabasi yanayofunika scania marcopolo mengi design yake sio kwa safari ndefu kama Dar -Mbeya/Kyela/Tunduma/Nzega/Shinyanga/Arusha au Arusha-Mbeya au Dar-Songea.
   
 13. K

  Kamuna JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 297
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Swala la choo kwa wasafiri ni mada nyeti sana ijapokuwa hatuliongelii. Ni aibu mabasi kusimama vichakani, wakati mwingine unasafiri na wazazi, wakwe na watoto. Nadhani swala hili halijapewa uzito unaostahili na wadau pamoja na serikali. Kwa mtazamo wangu serikali kupitia wizara kadhaa inaweza kufacilitate utaratibu wa kuwa na vyoo vinavyoeleweka. Kwa nchi za wenzetu ni kosa la jinai kujisaidia vichakani kama tunavyofanya sie. Naungana na mtoa maada kwamba something should be done, and it can be done by wadau if the government does not care.Yes, we can!
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,372
  Likes Received: 22,234
  Trophy Points: 280

  kujiosha ni kimoyomoyo.
  Halafu wale wanaopenda yale mambo yetu yaleeee ya uvinza
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nchi za wenzetu mabasi yanasimama kwenye petrol station ili watu wajisaidie, niliona hivyo Norway. Hili kwetu tunashindwa nini? Mbona wakati wa kula chakula wanasimama sehemu maalumu? Hii issue ni kupiga marufuku tu na kuwaambia madereva hakuna kusimama porini kwa ajiri hiyo, lakini wasimamishe gari kwenye petrol stations ambazo kawaida zina vyoo
   
 16. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2017
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Haya mambo ya kuchimba MAKINIKIA porini yamefikia wapi?
   
Loading...