Ingawa nimekupa hoja ya 2 wakorinto 3:6,kuhusu agano jipya,1wakorinto 10:25 na Luka 10:8 kuhusu kula umepotezea. Haya soma wagalatia 3:10-14. Kwa hy wasabato mmechagua matendo ya sheria kwa hy mko chini ya laana kwa maana imeandikwa amelaaniwa kila mtu asiyedumu ktk kitabu cha torati ayafanye,sisi tumepata neema kwa imani,nyinyi mnatafuta haki kwa sheria,je Yesu hakufanya kazi siku ya sabato? Hakuponya? Kama alifanya kazi siku ya sabato kwa nn msifuate nanyi?
aisee!Uwe unasoma biblia kwa kutafakari, biblia siyo magazeti!!! Hebu tuyachunguze maandiko hapa:
umetoa
2wakorintho 3:6
jibu lako:
Waebrania 8:8-12
[SUP]8 [/SUP] Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;
[SUP]9 [/SUP] Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.
[SUP]10[/SUP] Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.
[SUP]11[/SUP] Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
[SUP]12[/SUP] Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.
Nafikiri ukisoma kwa kutafakari utaelewa mwenyewe. Hilo ndo agano jipya analoliongea.
Mungu anapoongea agano jipya hamaanishi uandishi wa biblia kabla ya Yesu na wakati wa Yesu.Hapa kinachokusumbua ni kiswahili tu nafikiri watafsiri walishindwa kupata neno kama la kiingereza au lugha zingine.
Katika kiingereza AGANO LINALOONGELEWA HAPA INAMAANISHA COVENANT na hilo la uandishi ambalo wewe pia umepotea kwalo linaitwa OLD TESTAMENT kwa agano la kale(yaani biblia iliandikwa kabla Yesu hajafanyika mwili) na NEW TESTAMENT kwa agano jipya(yaani biblia wakati Yesu amefanyika mwili)
Umetoa
1 Wakorintho 10:25
Jibu soma
1 Wakorintho10:23-33
23 Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.
24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.
25 Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;
26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.
27 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.
28 Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.
29 Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?
30 Ikiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho?
31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
32 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu,
33 vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.
Rafiki, kama nilivyokwisha sema huko mwanzoni, usisome biblia mstari mmoja kwa nia ya kuhalarisha kilicho haramu. twende pamoja:
Majibu yamekuwa wazi sana katika fungu la 27,28 ambapo sasa shida kubwa iliyokuwepo Korintho wakati wa uingizaji wa injili ya Yesu imetajwa wazi katika mafungu hayo.Elewa kwamba Injili ya Yesu ilipoingia wale waliopokea bado hawakuwa tayari kushirikiana na wale wapagani ambao waliendelea kuamini na kufanya matambiko ya miungu yao. Hivyo basi wale waongofu wapya badala ya kuonyesha kwamba Mizimu ya wapagani haina nguvu kwao, badala yake walipofika sokoni walianza kuuliza kama ile nyama iliyouzwa mle sokoni ilikuwa imechinjwa kwa ajili ya ibaada ya mizimu(sanamu) au la. Na walipoambiwa ilichinjwa kwa ajili ya ibaada ya (sanamu) waliacha kununua. Ndipo Paulo akawaandikia barua hiyo akiwaambia wasiulize ulize ila wanunue wakale tu maana wao wamekuwa viumbe wapya katika Kristo Yesu. Pia uelewe kwamba katika suala zima la ibaada iwe ya Kikristo au ya Wapagani, mnyama aliyechinjwa ni kondoo, usijefikiri walichinja nguruwe. Kwa hiyo rafiki hakuna vyakula najisi vilivyoruhusiwa kuliwa. Najisi ni najisi hata Kristo arudipo!!! Halafu mbona hukuongelea fungu la 31,32?
Umetoa
Luka 10:8
Jibu: Hili fungu linakuhusu wewe na wenziyo ndo maana usiku mwingi huu sijalala najaribu kukufunulia mambo haya usiyoyaelewa!
Wagalatia 3:10-14
Hili limejibiwa na
Basluma Original sihitaji kuongeza!